tume ya Vyo Vikuu nchini (TCU) imetoa tangazo kwa umma kuhusu zoezi la udahili awamu ya tatu. Dirisha la udahili liko wazi hadi Septemba 26, 2018. Maelezo zaidi bofya katika link hii HAPA
Viongozi wa nchi tajiri zaidi duniani zinazounda kundi la G7 wanatarajiwa hii leo kutoa msimamo wa pamoja dhidi ya vitisho vya kiuslama vinavyoikumba dunia vikiwemo kitisho cha makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali hadi kile Rais wa Marekani Barack Obama amelaani na kuutaja kama uchokozi wa Urusi nchini Ukraine. Kwa mara ya tatu mfululizo, viongozi hao wamemtenga Rais wa Urusi Vladimir Putin kutoka mkutano huo ulioanza hapo jana na unaokamilika hii leo katika mji wa Elmau nchini Ujerumani na badala yake wamewaalika viongozi kutoka kwingineko akiwemo waziri mkuu wa Iraq Haider al Abadi na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ambao wote wawili wanakabiliwa na kitisho kutoka makundi ya wanamgambo. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Ufaransa Francois Hollande wanatarajiwa kuangazia masuala ya mazingira katika mkutano huo hasa kuongezeka kwa viwango vya joto duniani na athari zake. Chanzo: DW
KUANZISHWA KWA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA Mafanikio ya michuano ya mpira wa miguu ya Olimpiki ndiyo yalikua mwanzo wa FIFA kutamani kuwa na michuano yake ya Kombe la Dunia kwa mchezo wa mpira wa miguu. Ikumbukwe kwamba kipindi hicho mpira wa miguu wa wanaume pekee ndiyo ulikuwepo. Maswali yalitumwa kwa wahisani wa FIFA ili kuona kama wanakubaliana na uanzishwaji wa michuano hiyo na kwa masharti yapi? Kamati maalumu ilichunguza maswali hayo chini ya uongozi wa Rais wa FIFA wa kipindi hicho Jules Rimet akishirikiana na Katibu wa Shirikisho la Soka nchini Ufaransa kwa wakati ule Henri Delaunay. Rais wa FIFA Jules Rimet aliyeanzisha na kusimamia Kombe la Dunia la kwanza . Kufuatia uwepo wa muswada wa Kamati Tendaji ya FIFA, lilifanyika kongamano la FIFA Mei 28, 1928 jijini Amsterdam nchini Uholanzi likiazimia kuwepo kwa michuano ya mabingwa wa soka duniani ambayo ilipangwa na shirikisho hilo la mpira duniani na sasa nchi waandaji wa michuano hiyo zilitakiwa kuchaguli
Lugha ya Kiswahili inazungumzwa katika nchi za Afrika Mashariki. Kiswahili hutumika nchini Tanzania, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Msumbiji na Rwanda. Zaidi ya watu milioni 1 5 katika bara hili huitumia lugha hi i kama lugha ya kwanza na wazungumzaji wengine wakiitumia kama lugha ya pili au ya tatu. Ni lugha rasmi ya M uungano wa Afrika. Hii inafanya bara hili kuwa na idadi inayozidi milioni 100 ya wazungumzaji wa lugha hii. Kiswahili ni miongoni mwa lugha kumi zinazoongoza kwa kua na idadi kubwa ya wazungumzaji barani Afrika. TANZANIA Kiswahili nchini Tanzania ni lugha rasmi na lugha ya Taifa. Ni lugha ya utambulisho kwa Mtanzanianainatumika kama lugha ya kuimarisha uelewano, ushirikiano na umoja wa kitaifa. Katika kuiendeleza, juhudi za usanifishaji zimefanyika kwa kuwatumia wataalamu wa fasihi na isimu, wadau wengine na wachapishaji vitabu. Taasisi mbalimbali zimebuniwa kuhusu lugha hii kama vile BAKITA, BAKIZA, Taasisi ya Elimu, UWAVI
Jana nilikuletea orodha ya waigizaji 10 wa kiume wenye mvuto nchini Korea Kusini, leo tuangalie upande wa pili kwa akina dada ambao ni warembo zaidi. #10. Han Ye Seul Han Ye Seul alizaliwa chini Marekani japokuwa ana asili ya Korea. Anaigiza series na filamu za kawaida. Alionekana katika Nonstop 4 na pia ameigiza katika muvi kama vile Couple or Truble, Birth of a Beauty, Miss Gold Digger na Penny Pincher. Baada ya kupata umaarufu nchini Korea aliamua kufuta uraia wake wa Marekani na kuamua kuwa raia wa Korea Kusini. #9. Song Hye Kyo Song Hye Kyo alipata umaarufu katika tasnia ya muvi nchini Korea katika muvi kama vile Autumn in My Heart, All In, Full House, The World They Live In na nyinginezo. Ni mwenye furaha na amekuwa akiigiza muvi zake vizuri sana. #8. Lee Da Hae Lee Da Hae ni muigizaji maarufu nchini Korea Kusini. Ameigiza katika My Girl, Green Rose, The Slave Hunter, Miss Ripley na Hotel King. Ameigiza pia katika muvi za Kichina kama vile Actually Lobe na
Leo nimekuandikia orodha ya marais 10 waliofariki wakiwa madarakani. Tuanze kuhesabu sasa: 10. Lansana Conte, Rais wa Guinea Baada ya miaka 24 Lansana Conte alifariki na ugonjwa usiojulikana akiwa na umri wa miaka 74. Alipambana na matatizo ya kisukari na maradhi ya moyo. Kuanzia Aprili 1984 mpaka kifo chake Desemba 2008 alikuwa ni rais wa pili kushika madaraka nchini Guinea. Mbali na matatizo ya afya aliyokuwa nayo aliweza kushinda uchaguzi. 9. Omar Bongo, Rais wa Gabon Saratani ya tumbo iliosambaa ndio iliyosababisha kifo cha R ais Omar Bongo June 2009 mjini Barcelona, Uhispania, baada ya kuwa rais kwa miaka 42 mfululizo. Alifariki akiwa na umri wa miaka 72 na pia alikuwa ni kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu katika historia na alikuwa akiongoza katika mambo ya rushwa. Bongo alijikusanyia utajiri mkubwa huku akiiacha nchi yake katika hali ya umasikini. 8. Joao Bernardo Vieira, Rais wa Guinea-Bissau Joao Bernardo Vieira rais w
Uhali gani msomaji na mfuatiliaji wa VENANCE BLOG? Nakukaribisha katika darasa jipya la kufahamu mambo kadha wa kadha kama yanavyokuwa yakipigiwa kura na watu kutoka vyanzo tofauti kama vile tovuti, mitandao ya kijamii, watu wenye ushawishi, majarida n.k. Basi kwa kuanza leo nakuletea orodha ya waigizaji 10 wa kiume wenye mvuto nchini Korea. Vigezo vilivyotumika husemwa na mtandao husika unaotoa orodha hiyo. Ili kurahisisha kazi hii, mimi kama Blogger ntakuletea orodha hizi kila siku kwa lugha ya Kiswahili. Na tuanze sasa, tunaanzia Korea Kusini kuangalia waigizaji wa kiume wenye mvuto kwa mwaka 2017: # 10. Lee Byung-Hun Lee Byung-Hyun ni muimbaji, mwanamitindo na muigizaji kutokea Korea ya Kusini. Anamiliki kampuni yake ya BH Entertainment. Ni muhitimu wa masuala ya filam na maigizo katika Chuo Kikuu Chung Ang. Anazungumza Kiingereza, Kifaransa, Kikorea na Kimandarin lakini pia ni mfuasi wa dini ya Budha. Alizaliwa Julai 12, 1972 katika jimbo la Gyeonggi Korea ya Kusini. Alianz
Waokoaji kutoka Australia wamefanikiwa kuwaokoa abiria 52 waliokuwa wamekwama katika meli ya Akademic Shokalskiy huko barani Antaktika toka tarehe 24 Desemba mwaka jana 2013 na helkopta inayomilikiwa na raia wa China aitwaye Xu Long. Meli hiyo ilikwama kutokana mlundikano wa barafu katika injini zake. Barafu hiyo ilisafirishwa na upepo mkali umbali wa netiko maili 1,500 kutoka katika mji wa Hobart jimbo la Australia. Kazi ya kuokoa abiria hao ilichukua dakika 45 kwa kila Wafanyakazi wa meli hiyo wanataraji kubaki katika meli hiyo kwa muda wa wiki moja mpaka pale barafu itakapoyeyuka. Aidha abiria hao waliokuwa wakisafiri kuelekea Tasmania hawatasafiri tena mpaka pale hali itakapokuwa shwari katikati ya mwezi huu. Jinsi barafu ilivyokuwa imeganga Jinsi barafu ilivyokuwa imeganga
Comments
Post a Comment