Watu 12 wamekufa papo hapo na wengine zaidi ya 90 kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Korogwe, Tanga kwenda Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka. Ajali hiyo ilitokea jana saa 1.30 asubuhi kwenye barabara kuu ya Segera-Chalinze katika kijiji cha Kwalaguru kata ya Kwedizinga wilayani hapa. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe alithibitisha jana kutokea kwa ajali hiyo ya basi la Burudani namba T 610 ATR aina ya Nissan. Majeruhi walipelekwa katika hospitali ya wilaya ya Korogwe ya Magunga, kwa matibabu ya awali na miili ya marehemu, akiwamo dereva wa gari hilo, Luta Mpenda (35) imehifadhiwa hospitalini hapo. “Tukiwa tunakaribia kwenye kona ile, tulipishana na lori hilo likiwa kasi upande wetu, dereva wetu akajitahidi kulikwepa lakini kutokana na ile kona kuwa kali, gari lilimshinda na kupinduka,” alisema Bendera. Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo walisema walisikia kishindo kutoka eneo hilo wakaenda na kukuta gari limepinduka na baadh...
Comments
Post a Comment