UCL: FAHAMU MACHACHE MECHI YA MAN CITY VS LYON
Mechi itachezwa saa 4:00 usiku saa za Afrika Mashariki katika dimba la Man City Etihad. Mwamuzi wa mechi hii ni Muitalia Daniele Orsato.
Hii ni mechi ya kwanza baina ya timu hizi. Mpaka sasa hakuna klabu ya Ufaransa iliyowahi kushinda ugenini dhidi ya Man City zaidi ya kuambulia suluhu 1 na kupoteza michezo 2.
Lyon imeshinda mechi 1 tu kati ya 8 ilizocheza na timu za Uingereza. Hii ilikua ni dhidi ya Liverpool katika dimba la Anfield Oktoba 2009.
Hii ni mara ya 8 mfululizo kwa Man City kushiriki katika ligi ya mabingwa Ulaya. Hii ni rekodi ya juu kwa sasa katika timu za Uingereza kushiriki idadi hii ya Man City ambayo mara nyingi imekua ikiondolewa katika mechi ya 5 ya michuano hii hatua ya makundi.
Katika mechi zao zote 42 walizocheza Man City hakuna mechi hata moja ambayo hawakufunga katika ligi hii.
Hii ni mara ya 15 kwa Lyon kushiriki michuano hii. Hii inaifanya kuwa timu pekee kutoka nchini Ufaransa kushiriki mara nyingi zaidi. Wamekuwa wakiondolewa katika hatua ya mtoano kuanzia msimu wa 2003/2004 hadi 2011/2012 na hawajawahi tena kufikia hatua hiyo.
Lyon wameshinda mechi 3 tu kati ya mechi zao 13 za mwisho katika ligi hii pamoja na kusuluhu mechi 3 na kupoteza mechi 7.
Lyon ilifunga magoli 5 tu katika mechi zao 5 za mwisho katika ligi hii. Magoli 2 yalifungwa nyumbani na magoli 3 ugenini.
Kocha wa Man City Pep Guardiola amewahi kufikisha timu zake katika hatua ya nusu fainali katika michuano 7 kati ya michuano 9 ya ligi hii aliyoshiriki kama kocha lakini hajatwaa ubingwa tangu alipotwaa mara ya mwisho 2011. Msimu huu atakua anawania kutwaa kombe hilo ili afikie rekodi ya Zinedine Zidane, Carlo Ancelotti na Bob Paisley ya kutwaa kombe hili mara 3.
Raheem Sterling ameifungia klabu yake ya Man City magoli 8 wakiwa nyumbani na kuisaidia kufunga magoli 6 katika mechi 15 alizoichezea klabu hake hiyo.
Mshambuliaji wa Lyon Moussa Dembélé ameifungia klabu hiyo magoli 3 katika mechi 4 za mwanzo katika klabu hii katika UCL. Awali ya Lyon aliwahi kuichezea Celtic ambapo aliifungia klabu hii goli 1 katika mechi 6 kwenye michuano hii.
Man City itaingia uwanjani bila wachezaji wake Benjamin Mendy, Danillo, Claudio Bravo, Kelvin De Bruyne, Sergio Kun Arguero, Eliaqim Mangala na Philippe Sandler ambao ni majeruhi. Kwa upande wa Lyon watakosekana Amine Gouiri na Fernando Marcal.
Comments
Post a Comment