KUTOKA TCU: TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI AWAMU YA TATU

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)

TAARIFA KWA UMMA

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwa Awamu ya Pili ya
Udahili wa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na masomo ya shahada za awali
ulimalizika tarehe 10 Oktoba 2017. Kutokana na waombaji wengi kutochaguliwa kwa
sababu mbali mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa Awamu ya Tatu
kuanzia tarehe 16 hadi 18 Oktoba 2017. Tume inapenda kusisitiza yafuatayo:
a) Awamu hii itawahusu waombaji waliokosa nafasi kwenye Awamu ya Kwanza na
ya Pili kutokana na ushindani au kukosa sifa katika programu walizoomba;
b) Waombaji waliochaguliwa zaidi ya chuo kimoja; wanatakiwa kuamua mara moja
kwa kuchagua chuo kimoja tu na hatimaye kukiarifu chuo husika;
c) Awamu hii haitawahusu waombaji wapya (ambao hawajawahi kutuma
maombi katika awamu mbili zilizopita);
d) Waombaji ambao hawatathibitisha uchaguzi wao au kujithibitisha zaidi ya chuo
kimoja hawatatambuliwa na Tume katika udahili wa mwaka 2017/18
e) Waombaji kuwasiliana moja kwa moja na mara kwa mara na vyuo husika kwa
masuala yote yanayohusiana na zoezi la udahili badala ya kuja TCU.
f) Waombaji wote kutembelea Tovuti za vyuo ili kufahamu hatima ya maombi yao.
Aidha, Tume inapenda kusisitiza kuwa utaratibu wa kutuma maombi na kuthibitisha
ni ule ule uliotumika katika awamu mbili zilizopita za Udahili.
Imetolewa na
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
16 Oktoba 2017


Unaweza kudownload taarifa hiyo kwa kubofya HAPA

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017