KUTOKA TCU: TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI AWAMU YA KWANZA 2017/2018



TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI 2017/2018

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia umma kuwa Awamu ya Kwanza ya kudahili wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na masomo ya shahada za awali ilimalizika tarehe 30 Agosti 2017. Katika awamu hiyo, kama ilivyoelezwa katika tangazo la Tume la tarehe 20 Julai 2017 wanafunzi watarajiwa walituma maombi yao moja kwa moja kwenye vyuo hapa nchini. Vyuo vilichakata maombi hayo na hatimaye kuyawasilisha Tume kwa ajili ya uhakiki.Tume inapenda kuuarifu umma kuwa imekamilisha zoezi la uhakiki wa majina ya waombaji wote walioomba kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo wa 2017/18. Matokeo ya uhakiki ni kama ifuatavyo:a) Jumla ya idadi ya majina yaliyowasilishwa toka vyuoni yalikuwa 180,640 (wanaume 109,399, wanawake 71,241). Hata hivyo majina haya yalikuwa na kasoro kadhaa kama vile kujirudia. Tume iliyahakiki na kubakisha majina 77,756 (wanaume 47,501 wanawake 30,255) ambayo ni jumla ya maombi yote.b) Jumla ya wanafunzi ambao wamechaguliwa na vyuo (kati ya
waombaji 77,756) ni 44,627 (wanaume 27,116 wanawake 17,511).


Hiyo ni sawa na asilimia 57.4 ya waombaji wote. Waombaji 33,129 

waliosalia (42.6%) hawakuchakuguliwa na vyuo kutokana na 
ushindani au kukosa sifa katika programu walizoomba.
c) Katika waombaji 44,627 ambao wamechaguliwa na vyuo, Tume 
imejiridhisha kuwa waombaji 20,247 (45.4%) wanaweza kujiunga na 
vyuo walivyoomba moja kwa moja (wanaume 12,396 wanawake 
7,851). Waombaji 16,584 (37.2%), wanaume 9,923 wanawake 6,661, 
wamechaguliwa zaidi ya chuo kimoja. Aidha waombaji 7,796 (17.4%), 
wanaume 4,797 wanawake 2,999, Tume imebaini kuwa hawana sifa 
za kujiunga na vyuo vilivyowapendekeza. Hii ina maana waombaji 
36,831 (wanaume 22,319 wanawake 14,512) wanatarajiwa kujiunga 
na vyuo katika Awamu hii ya Kwanza.
Taarifa kuhusu majina ya waombaji waliochaguliwa na wale 
waliochaguliwa zaidi ya chuo kimoja zimewasilishwa kwenye vyuo husika.
Hivi sasa Tume imefungua maombi kwa Awamu ya Pili kuanzia tarehe 4 
hadi 10 Oktoba 2017 ili kuruhusu makundi yafuatayo kuomba udahili:
a) Waombaji ambao wamechaguliwa zaidi ya chuo kimoja; waombaji 
hawa watatakiwa kuamua mara moja na kuchagua chuo kimoja tu na 
hatimaye kukiarifu chuo hicho
b) Waombaji ambao wamekosa nafasi kwenye awamu ya kwanza 
kutokana na ushindani au kukosa sifa katika programu walizoomba;
Aidha Tume imetumia fursa hii kuruhusu makundi yafuatayo kuomba 
udahili:
a) Waombaji wa Kidato cha Sita walioshindwa kuomba katika awamu ya
kwanza;
b) Waombaji wenye vigezo vya Stashahada waliochelewa kupata 
Namba ya Uhakiki wa Tuzo (AVN);
c) Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya “Cambridge” mwaka 2017 
na matokeo yao yameshatoka; na
d) Waliokuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watakaokuwa na uthibitisho 
toka vyuo vyao vya awali.
Tume inapenda kusisitiza kuwa utaratibu wa kutuma maombi katika 
Awamu ya Pili ni ule ule uliotumika katika Awamu ya Kwanza ya Udahili. 
Hii ina maana kuwa waombaji watatakiwa kuwasilisha maombi yao moja 
kwa moja vyuoni na siyo kwenye Tume (TCU).
Tume inawashauri waombaji wote kutumia fursa hii fupi kukamilisha 
maombi yao ili kuepuka kukosa udahili kwa mwaka wa masomo 2017/18. 
Aidha Tume inawataka waombaji wote kutembelea Tovuti za vyuo ili 
kufahamu hatima ya maombi yao. Kwa wale ambao wamechaguliwa zaidi 
ya chuo kimoja wathibitishe sawia chaguo la chuo kimoja tu ili kuepuka 
uwezekano wa kukosa udahili kwa mwaka wa masomo 2017/18. 
Prof. Eleuther Mwageni
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
5 Oktoba 2017

Unaweza kuipata taarifa hii kama PDF kwa KUBOFYA HAPA

Comments

Popular Posts

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

BIBI WA MIAKA 85 AKAMATWA KWA KUIBA HERENI

MAMBO YA MUHIMU KUFAHAMU NA KUZINGATIA KABLA YA KUCHAGUA KOZI (TAALUMA) CHUO KIKUU