ROBOTI XINGHZE1 ATEMBEA KILOMITA 134 KUWEKA REKODI MPYA
Roboti aliyepewa jina la Xinghze No. 1 aliyetengenezwa nchini China, amevunja rekodi ya Dunia ya 'Guinness World Records' kwa kutembea kilomita 134.03 ambazo ni sawa na maili 83.28 (83.28 miles). Roboti huyo aliyetengenezwa na team iliyoongozwa na Profesa Li Qingdu kutoka College of Automation of Chongqing University of Posts and Telecommunications. Roboti huyo aina ya Quadruped ametengenezwa kwa mashine moja ambayo inaongozwa na program ya kompyuta au sakiti moja ya umeme. Pia, roboti huyo ameundwa kwa miguu minne (Four legs) isiyo na magurudumu (wheels). Mwongozo uliotolewa na Guinness World Records ni kwamba ili Roboti avunje rekodi ya Dunia kutembeanumbali mrefu, anatakiwa kuchajiwa mara moja au kutumia tanki moja la mafuta na pia anatakiwa atembee mfululizo kwa masaa takribani 54 na dakika 34 ili kuipiku rekodi inayoshikiliwa na jopo Chuo Kikuu cha Cornell Ranger Robot ambapo roboti wao alitembea umbali wa kilomita 65.18 sawa na maili 40.5, roboti Walker 1, aliv...