BIBI WA MIAKA 85 AKAMATWA KWA KUIBA HERENI

Bibi kizee mmoja mwenye umri wa miaka 85 raia wa Marekani na ambaye amekuwa akiiba vito vya thamani kwa zaidi ya miaka 60 amehukumiwa tena kwa kosa la wizi.

Doris Payne, anatuhumiwa kwa wizi wa herini ya thamani ya dola 690, kutoka katika duka moja la uuzaji wa vitu vya thamani la Saks katika kiunga kimoja mjini Atlanta-Marekani.

Wakili wake anatafuta namna ataachiwa huru kwa sababu ya kudorora kwa afya yake.

Payne, ambaye maisha yake ya wizi yaliwekwa katika filamu mwaka 2013, amewahi kufungwa jela mara kadhaa kwa makosa mengi tu ya wizi na uhalifu.

Wakuu nchini Marekani wanasema kuwa, ametumia majina 22 ya bandia tangu alipoiba almasi kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 23, na akaweza kukwepa kutiwa mbaroni.

Muungano wa Walinzi wa vitu vya thamani JSA, kampuni moja kubwa ya kibiashara, ilituma tahadhari kwa maduka yote yanayouza bidhaa na mapambo ya thamani kujihadhari na mwizi huyo sugu mapema miaka ya 70.
Rais wa kampuni hiyo kubwa alitaja tabia ya bi kizee huyo kama wizi au uhalifu wa aina yake.

Aidha anastaajabu kuwa angali anaiiba hata akiwa na umri huo mkubwa.
Akihojiwa na shirika la habari la Associated Press mwaka 2005, akiwa jela, bibi huyo Payne, alisema kuwa haibi kwa sababu ya pesa ila yeye hujikuta tu akiiba na haoni kama ataacha tabia hiyo, labda baada ya kufa.


Chanzo: BBC

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017