MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YATANGAZWA UPYA UFAULU WAONGEZEKA KWA 9%
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dr. Shukuru Kawambwa jana ametangaza tena kwa mara ya pili matokeo ya kidato cha nne ambapo amesema ufaulu umeongezeka kwa 9% kutoka 34% mpaka kufikia 43% . Matokeo haya yalifutwa na kupangwa upya baada ya kuwa ule utaratibu uliotumika mwaka jana katika usahihishaji haukutoa taarifa kwa Wanafunzi na Waalimu pamoja na wadau wote wa Elimu, hivyo kufutwa na kupangwa kwa viwango vya mwaka juzi 2011. Matokeo ya shule niliosoma mimi yanapatika kupitia kiungo cha http://196.44.162.33/csee2012/CSEE%202012/s3370.htm NAKOZA SECONDARY SCHOOL iliyopo NANSIO wilayani UKEREWE mkoani MWANZA.