LIST OF APPLICANTS SELECTED TO JOIN CUHAS-BUGANDO 2017/2018


The Catholic University of Health and Allied Sciences (CUHAS) commonly Bugando has announced the names applicants who have been selected to join for the academic year 2017/2018.

Their names can be accessed BY CLICKING HERE

WALIOCHAGULIWA CHUO KIKUU KISHIRIKI STELLA MARIS MTWARA 2017/2018

Chuo Kikuu Kishiriki Stella Maris, kimretangaza majina ya waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

Kuangalia majina, BOFYA HAPA

WALIOCHAGULIWA CHUO KIKUU CHA RUAHA 2017/2018

Chuo Kikuu Cha Kikatoliki Ruaha (RUCU) kimetangaza majina ya waliochaguliwa chuoni hapo.

Kuona majina hayo, BOFYA HAPA

MAJINA YA WALIOCHAGULIWA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI (MOCU) 2017/2017

Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU) kimetoa majina ya shahada ya kwanza tayari.

Download majina HAPA

WALIOCHAGULIWA CHUO KIKUU ARDHI KOZI ZA SHAHADA 2017/2018 MAJINA YAO HAYA HAPA

Chuo Kikuu Ardhi kimetangaza majina ya waliochaguliwa kujiunga kozi mbalimbali za Shahada ya Kwanza chuoni hapo kwa Mwaka wa masomo 2017/2018.

Kuangalia BOFYA HAPA

KUTOKA TCU: TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI AWAMU YA PILI

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)
TAARIFA KWA UMMA
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwa awamu ya
kwanza ya Udahili wa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na masomo ya
shahada za awali ulimalizika tarehe 30 Agosti 2017. Tume inawaarifu kuwa
imekamilisha zoezi la uhakiki wa majina ya waombaji wote walioomba
kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo wa 2017/18.
Hata hivyo kutokana na waombaji wengi kutochaguliwa kutokana na sababu
mbali mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa awamu ya pili
kuanzia tarehe 4 hadi 10 Octoba 2017 ili kuruhusu makundi yafuatayo kuomba
udahili:
• Waombaji watakaokuwa wamekosa nafasi kwenye awamu ya kwanza;
• Waombaji wa kidato cha Sita walioshindwa kuomba katika awamu ya
kwanza;
• Waombaji wenye vigezo vya Stashahada walioshindwa kupata Namba
ya Uhakiki wa Tuzo (AVN);
• Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya “Cambridge” mwaka 2017
na matokeo yao yameshatoka; na
• Waliokuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watakao kuwa na uthibitsho
toka vyuo vyao vya awali.
Aidha Tume inapenda kusisitiza kuwa utaritibu wa kutuma
maombi ni ule ule uliotumika katika awamu ya kwanza ya Udahili.
Imetolewa na
Prof. Eleuther Mwageni
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
4 Oktoba 2017

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

Jana nilikuletea orodha ya waigizaji 10 wa kiume wenye mvuto nchini Korea Kusini, leo tuangalie upande wa pili kwa akina dada ambao ni warembo zaidi.

#10. Han Ye Seul

 
Han Ye Seul alizaliwa chini Marekani japokuwa ana asili ya Korea. Anaigiza series na filamu za kawaida. Alionekana katika Nonstop 4 na pia ameigiza katika muvi kama vile Couple or Truble, Birth of a Beauty, Miss Gold Digger na Penny Pincher. Baada ya kupata umaarufu nchini Korea aliamua kufuta uraia wake wa Marekani na kuamua kuwa raia wa Korea Kusini.

#9. Song Hye Kyo

Song Hye Kyo alipata umaarufu katika tasnia ya muvi nchini Korea katika muvi kama vile Autumn in My Heart, All In, Full House, The World They Live In na nyinginezo. Ni mwenye furaha na amekuwa akiigiza muvi zake vizuri sana.

#8. Lee Da Hae

Lee Da Hae ni muigizaji maarufu nchini Korea Kusini. Ameigiza katika My Girl, Green Rose, The Slave Hunter, Miss Ripley na Hotel King. Ameigiza pia katika muvi za Kichina kama vile Actually Lobe na Best Couple. Ni muigizaji maarufu nchini China kwa kua ni miongoni mwa waigizaji wanaozungumza Kichina, Kijapani na Kiingereza.

#7. Hai Ji Won

Hai Ji Won ni miongoni mwa wadada wazuri wa Korea. Anafahamika zaidi stejini kwa jina la Jeon Hae-rim. Mbali na Korea anafahamika pia kimataifa. Anaigiza series na filamu. Yumo katika Hwang Jin, Secret Garden, Express Ki na nyinginezo. Hai Ji Won ni ni muigizaji wa Kike wa Korea anayeongoza kwa taarifa zake kutafutwa zaidi mtandaoni na mashabiki kutokana na kuigiza scene mbalimbali kama vile action, michezo, vichekesho n.k.

#6. Shin Min Ah

Shin Min Ah alianza kama mwanamitindo alipokuwa mdogo na baadaye akaanza kuonekana katika video mbalimbali. Anafamika kwa kuigiza katika matukio mbalimbali kwenye muvi. Amepata umaarufu kwa kucheza muvi za action. Yumo katika muvi kama vile A Girl to Kill, My Girlfriend Is a Nine-Tailed-Fox, Oh My Venus na nyinginzeo.

#5. Jun Ji Hyun

Jun Ji Hyun anafahamika pia kwa jina la Gianna Jun. Amekuwa maarufu katika My Sassy Girl. Ni miongoni mwa wadada wanaolipwa sana kwa kucheza muvi za vichekesho nchini Korea. Ameigiza katika Il Mare, Windstruck, The Thieves, My Love From Another Star na nyinginezo.

#4. Park Shin Hye

Park Shin Hye ni muigizaji, mwanamuziki, dansa na mwanamitindo. Alianza kuonekana katika tasnia ya uigizaji nchini Korea katika Stairway to Heaven. Aliigiza pia katika series ya Kikorea na Kijapan inayoitwa Tree of Heaven. Pia kaigiza katika You're Beautiful, Heartstrings, Flower Boys Next Door na nyinginezo.


#3. Han GA-In

Han GA-In alianza kuonekana katika Yellow Handkerchief na Terms of Endearment. Anafahamika zaidi katika tasnia ya mitindo pia. Ameigiza pia katika Moon Embracing na Architecture.

#2. Yoon Eun Hye

Yoon Eun Hye ni msaniii mwenye vipaji vingi ni muigizaji, mwanamuziki, muongozaji wa filamu, mburudishaji na pia mwanamitindo. Amewahi kushinda tuzo kama Muigizaji Bora wa Kike akiwa ni muigizaji mdogo wa kike kushinda tuzo hiyo. Ameigiza katika Princess Hour, Missing You, Mary Him If I Die na nyinginezo.

#1. Choi Ji Woo

Choi Ji Woo ni miongoni mwa waigizaji maarufu wa Korea miaka ya 2016-2017. Huyu ndiye muigizaji mrembo na mzuri sana kwa waigizaji wa Kike nchini Korea.Ameigiza katika Winter Sonata, Beautiful Girls, Stairway to Heaven na nyinginezo.



Una maoni yoyote? Usisite kuniandikia katika anuani zifuatazo:
Facebook: VENANCE BLOG
Twitter: @Venancetz
WhatsApp: +255 712 586 027
Instagram: @venanceblog
Barua pepe: venancegilbert@gmail.com

CLAIRE FOY KUPAMBA JARIDA LA MITINDO LA VOGUE MWEZI UJAO

Claire Foy ambaye ni muigizaji maarufu nchini Uingereza, ataonekana kwenye ukurasa wa mbele kabisa wa Jarida la Mitindo nchini humo la Vogue. Taarifa hii inakuja rasmi kabisa kutoka katika mtandao wa Vogue.

Claire alizaliwa April 4, 1984 huko Stockport Uingereza. Anafahamika kwa kuigiza vema kabisa katika "Season of the Witch" (2011), "Going Postal" (2010) na "Wreckers" (2011). Amefunga ndoa na Stephen Campbell More toka Desemba 2014 na wana mtoto mmoja katika ndoa yao.

Claire amewahi kushinda tuzo za Golden Globes kama Muigizaji wa Kike aliyefanya vizuri katika maigizo kupitia series ya The Crown (2016), BAFTA/La Britania Awards kama Muigizaji bora wa mwaka nchini Uingereza (2017) na Screen Actor Guild Awards kama muigizaji bora wa kike (2017). Alitajwa pia katika tuzo za Primetime Emmy Awards, BAFTa Awards, Chritics Choice Television Awards, Broadcasting Press Guild Awards

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017

Uhali gani msomaji na mfuatiliaji wa VENANCE BLOG? Nakukaribisha katika darasa jipya la kufahamu mambo kadha wa kadha kama yanavyokuwa yakipigiwa kura na watu kutoka vyanzo tofauti kama vile tovuti, mitandao ya kijamii, watu wenye ushawishi, majarida n.k. Basi kwa kuanza leo nakuletea orodha ya waigizaji 10 wa kiume wenye mvuto nchini Korea. Vigezo vilivyotumika husemwa na mtandao husika unaotoa orodha hiyo. Ili kurahisisha kazi hii, mimi kama Blogger ntakuletea orodha hizi kila siku kwa lugha ya Kiswahili. Na tuanze sasa, tunaanzia Korea Kusini kuangalia waigizaji wa kiume wenye mvuto kwa mwaka 2017:

#10. Lee Byung-Hun

Lee Byung-Hyun ni muimbaji, mwanamitindo na muigizaji kutokea Korea ya Kusini. Anamiliki kampuni yake ya BH Entertainment. Ni muhitimu wa masuala ya filam na maigizo katika Chuo Kikuu Chung Ang. Anazungumza Kiingereza, Kifaransa, Kikorea na Kimandarin lakini pia ni mfuasi wa dini ya Budha. Alizaliwa Julai 12, 1972 katika jimbo la Gyeonggi Korea ya Kusini. Alianza kuigiza katika televisheni ya KBS katika baadhi ya matukio ya mchezo wa kuigiza "Asphalt My Hometown" Aliendelea kuigiza hadi mwaka 2000 alipoigiza muvi iliyompa umaarufu zaidi na kuuza sana nchini humo, muvi hiyo iliitwa "Joint Security Area" Lee ni mwanachama wa Academy of Motion Picture Arts and Science huko Hollywood Marekani.


#9. Jang Geun-Suk


Jang anapenda kutereza kwenye barafu, kuimba na kucheza. Ni muhitimu wa masuala ya filam na maonesho ya jukwaani katika Chuo Kikuu cha Yang Han nchini Korea Kusini. Alianza kuigiza mwaka 2008 katika Kdrama ambapo aliigiza katika "Beethon Virus" aliigiza pia mwaka 2009 katika "You are Beautiful" na mwaka 2010 "Marry Stayed Out All Night" yote akifanya Kdrama. Kwa sasa anafanya kazi kama muigizaji na muongozaji. Jang alizaliwa Agost 4, 1987 na ameonekana vyema katika maonesho zaidi ya 20 aliyowahi kuigiza. Jang anafahamika kama muigizaji anayejituma sana katika Kdrama. Mwaka jana 2016 aliachia albam zake kadhaa za muziki zikiwemo mbili za "Just Crazy" na "Lounge H". Mnamo Julai mwaka jana 2016 aifanya ziara yake ya kimuziki barani Asia ikiwemo Seoul nchini Korea Kusini, China na Japan ambako alipata mafanikio makubwa katika ziara yake hiyo ya "It's Show Time"  kwa sasa anashughilika na kipindi cha maisha halisi kinachoitwa "My Ear's Candy"


#8. Gong Yoo

Alizaliwa Julai 10, 1979. Ni muhitimu wa Chuo Kikuu cha Kyung Hee akiwa na Shahada ya Sanaa na Maonesho. Anafahamika zaidi kwa kucheza michezo ya Martial Art ya Urusi, pamoja na kupanda kwenye miamba kama alivyoigiza katika "The Suspect" (2013). Alitajwa kama muigizaji maarufu zaidi nchini Korea Kusini mwaka jana 2016. Amewahi kuigiza katika muvi ya mazombi "Train to Busan" alipoambiwa atoe maoni kuhusu muvi hiyo alisema "nilidhani muvi za mazombi na kupigana ni rahisi sana, nilihangaika mno"

#7. Song Joong-Ki

Song alianza kuigiza kama utani tu katika shindano la Kdarama ambalo lililenga kutafuta vipaji "Descendants of the Sun" Kuuigiza haikuwa chaguo lake. Amewahi kushiriki katika michezo ya kutereza kwenye barafu ngazi ya taifa lakini alishindwa kuendelea kutokana na majeraha ambapo alishindwa kushiriki Olympic. Mwaka 2010 aliandika kitabu cha "Beatiful Skin Project" Mwaka 2008 aliigiza katka "A Frozen River" japokuwa igizo lililompa umaarufu sana ni "Sungkyunkwun Scandal" Mwaka 2017 ameigiza katika "Battleship Island"

#6. Park Yoo-Chun

Park ni muigizaji mwenye tuzo nyingi katika tasnia hii ya filamu naa uigizaji nchini Korea Kusini. Anafahamika pia kwa jina la Micky Yoo-Chun, jina la kiingereza alilopewa alipokuwa Virginia nchini Marekani. Alizaliwa Juni 8, 1986 Seoul mji mkuu wa Korea Kusini. Ni mtuzi wa nyimbo, muimbaji na muigizaji, nyimbo zake zipo katika maadhi ya Kpop, rhythm naa blues. Amewahi kuwa mshiriki katika kundi la DBSK toka 2003 hadi 2009 na kwa sasa yupo ktk kundi la JYJ. Ameigiza katika "Sungkyunkwan Scandal", "Miss Ripley" na "Rooftop Prince" Anafahamika pia kwa jina la "Gland Slam" kutokana na kushinda tuzo kutoka SBS, MBC na KBS ambazo ni maarufu nchini Korea Kusini.

#5. Hyun Bin

Hyun ni mmoja kati ya washindi wa tuzo kadhaa nchini humo. Anapendelea mpira wa kikapu, kuogelea na kwenda maonesho ya filamu. Amezaliwa Septemba 25, 1982 Seuol Korea Kusini. Ni muigizaji katka Kdrama ambapo amekuwa maarufu kupitia "My Name is Kim Sam-soon" ambayo ilimpa umaarufu sana na kumfanya ashinde tuzo za MBC Drama, Top Excellence. Ameigiza pia katika "The Secret Garden" Mwaka 2010 aliachia wimbo wake "Dream In my Heart", mwaka 2011 alitoa "Cant Have You" na "That Man" Mwaka 2010 alishinda tuzo ya Netizen Popularity Award.

#4. Kim Woo-Bin

Kabla hajawa muigizaji katika Kdarama, Kim alikuwa ni mwanamitindo aliyekuwa anatokea katika maonesho ya Seoul Fashion Week nchini Korea Kusini mwaka 2009. Anapenda sana mitindo lakini aliambiwa ili aongeze uzuri katika kazi yake hiyo ashiriki katika uigizaji, alikubali. Aliigiza katika "White Christmas" na baadaye mwaka 2013 aliigiza katika "School 2013" na "The Heirs" ambazo zilifanya aanze kutazamwa na Netizen. Mwaka 2012 alionekana katika fiamu tano zikiwemo "The Con Artist" na "Twenty". Mwaka 2016 aliigiza katika filamu ya uhalifu ya "Master" kama Park Jong-goon.

#3. Lee Jong Suk

Yeye anapenda sana kucheza games. Katika muda wake wa mapumziko anapenda kucheza Taekwondo na kupiga piano. Amezaliwa Septemba 14, 1989 ni muhitimu wa Chuo Kikuu Konkum akiwa na shahada ya filamu. Alianza kazi zake katika tasnia ya burudani kama mwanamitindo akitokea katika Seoul Fashion Week mwaka 2005. Mwaka 2010 alionekana katika "Prosecutor Princess" na baadaye akaonekana pia katika "The Secret Garden" na "School 2013"


#2. Lee Min Ho

Lee Min Ho alizaliwa Juni 22, 1987, anapenda sana filamu, kucheza game, na kucheza soka la miguu. Alihitimu Chuo Kikuu Konkuk akisomea filamu, na pia ana mdogo mmoja wa kike. Kwa mujibu wa IMDB, Min Ho alipokua mdogo alikuwa na ndoto za kuwa mcheza soka mkubwa lakink ndoto hizo zilipotea baada ya kuumia katika mchezo huo. Ameanza kuonekana Kdeama mwaka 2006 katika "Secret Campus" Hakua maarufu sana mpaka alipoigiza kama Goo Jon Pyo kwenye "Boys Over Flowers", na hapo ndipo alipoanza kuwa maarufu katika tasnia ya maigizo. Mwaka 2009 alishinda tuzo kama chipukizi bora kwenye tuzo za KBS Drama Acting Awards. Mafanikio zaidi yalifuata alipoigiza "Personal Tatse", "City Hunter" na "Faith" mwaka 2016 alionekana katika "The Legend of the Blue Sea" pia ni mpiga piano mzuri na muimbaji mwenye voko zake.

#1. Kim Soo-yun

Kim soo-hyun alizaliwa Februari 16, 1988. Ni muhitimu kutoka Chuo Kikuu Chung-Ang. Alionekana kwa mara ya kwanza 2013 kwenye "My Love From Another Star" japokuwa haikua na mwisho mzuri lakini ndiyo hii iliyompa umaarufu katika tasnia hii. Amekuwa akifanya kazi mbali mbali katika tasnia ya burudani nchini Korea Kusini kama vile kuimba, kuigiza, kufanya matamasha na hata kuwa balozi kuiwakilisha nchi yake. Mwaka 2014 alikuwa Balozi wa Goodwill kwa jiji la Seoul. Ameshinda tuzo kadhaa kama vile SBS New Star mwaka 2010, KBS New Actor mwaka 2011, na tuzo ya Popularity and Best Couple Awards.



Chanzo: Trending Top Most

Je, una lolote ungependa kusikia kuhusu chochote kinachohusiana na haya? Niandikie kupitia moja ya njia hizi:
WhatsApp: +255 712 586 027
Facebook: VENANCE BLOG
Instagram: @venanceblog
Twitter: @Venancetz
Barua pepe: venancegilbert@gmail.com

MSHAMBULIAJI WA MANCITY SERGIO AGUERO AJERUHIWA KATIKA AJALI

Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero amejeruhiwa katika ajali ya barabarani mjini Amsterdam, saa chache baada ya kuhudhuria tamasha.
Raia huyo wa Argentina, mwenye umri wa miaka 29, anaarifiwa kuwa ndani ya taxi akielekea katika uwanja wa ndege baada ya kuhudhuria tamasha la muimbaji Maluma.
City imesema "alikuwa Uholanzi katika siku yake ya mapumziko na amepata majeraha".
Sergio Aguero
Image captionSergio Aguero
Aguero anatarajiwa kurudi Manchester Ijumaa na atakaguliwa na kikosi cha madaktari wa City kabla ya kuelekea kwa mchuano wa Premier League watakapokaribishwa na Chelsea Jumamosi.
Polisi Amsterdam wameithibitishia BBC kwamba watu wawili walikuwa ndaniya taxi iliyohusika katika ajali katika eneo la De Boelelaan mjini humo.

Chanzo: BBC

MTANDAO WA TWITTER KUONGEZA MANENO HADI 280

Mtandao wa Twitter kwa sasa upo katika majaribio ya kuongeza maandishi yake kutoka 140 hadi 280 hii ikiwa ni mara mbili ya hayo ya awali.

Sababu za kuongeza idadi hiyo ya maneno ni kwamba kuna wakati mtu unaweza kuwa na hoja fulani inayozidi ukomo wa maneno lakini ukashindwa kuiandika ama ukapunguza idadi ya maneno ambayo wakati mwingine huwa ni ya muhimu sana katika tweet husika.
Huu ni mfano wa vile tweet ya sasa ilivyo na vile ambavyo ongezeko litakuwa kwa maneno 280.

Afisa Masoko Aliza Rosen wa Twitter na Mhandisi wa Twitter Japan  Ikuhiro Ihara wamesema kuwa katika mchakato wa kuruhusu jambo hili watu wachache watachaguliwa kwa majaribio na pia watakuwa wakikusanya maoni na kupata mrejesho kutoka kwa watumiaji wa Twitter kabla hawajafikia uamuzi wa kuruhusu ongezeko hilo la maneno.

Jinsi tweet za Kiingereza na Kispanyola zinavyokuwa ukilinganisha na Kijapan.

Zipo lugha ambazo hazitahusika kabisa katika jaribio ambazo ni Kichina, Kijapan na Kikorea sababu ni kwamba karibia 0.4% ya watu wanaotweet kwa lugha hizo hasa kijapan ndiyo hufikia ukomo wa sasa uliopo wakati lugha kama Kifaransa, Kiingereza, Kispanyora na nyinginezo 9% ya wanaotweet hufika ukomo wa maneno 140 kwa hiyo wakaona umuhimu wa kuongeza maneno.

Aidha utafiti uliofanywa na mtandao huo unadai kuwa watu wengi wanakasirishwa na ukomo wa idadi hiyo ya maneno.

IRAN IMEFANYA JARIBIO LA KOMBORA LA NYUKLIA

Iran inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la Khorram-shahr.

Kombora hilo lilionyeshwa hadharani katika maonyesha ya kijeshi jana Ijumaa.

Iran imesema kuwa kombora hilo linaweza kusafiri mwendo wa kilomita 2,000.

Kituo cha runinga cha taifa hilo kilionyesha picha za sherehe hizo.

Kombora la kwanza la Khorram-Shahr lilirushwa angani Januari lakini likalipuka katikati ya mwendo.

Jaribio hilo lilifanywa siku chache baada ya Rais Trump wa Marekani kushambulia Iran katika hotuba yake katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Rais wa Iran, Hassan Rouhani, ametetea hatua ya taifa lake kuimarisha zana zake kwa lengo la kujitetea.



Chanzo

AUDIO | HUNTER & D FLEVA FEAT BARNABA-FURSA | DOWNLOAD


Ngoma mpya kutoka kwa Hunter & D Fleva wakimpa shavu Baarnaba Boy Classic. Ngoma imefanyika Combination sound ukiwa ni mono wa fundi Man Water. VENANCE BLOG inakupa nafasi ya kudownload na kusikiliza.

DOWNLOAD

KAMPUNI YA ACACIA KUPUNGUZA SHUGHULI NA WAFANYAKAZI NCHINI

Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia imesema itapunguza wafanyakazi na shughuli zake za migodini ikiwa ni sehemu ya athari ya uzuiaji wa usafirishwaji wa makinikia uliowekwa na serikali ya Tanzania mwezi Machi mwaka huu.

Kampuni hiyo inasema wakati baadhi ya shughuli ndani ya mashimo yake ya dhahabu zitasimama, ndani ya wiki nne, uchenjuaji wa makininia pia nao utasimama.

"Kwa masikitiko, mpango huu utapelekea kupunguzwa kwa ajira kati ya wafanyakazi 1,200 waliopo hivi sasa na wanakandarasi 800" kampuni hiyo imesema kwenye taarifa.

Hata hivyo Acacia hawajasema ni wafanyakazi wangapi hasa watakaopunguzwa kazini.

Kampuni hiyo ambayo imeorodheshwa katika soko la hisa la London nchini Uingereza inasema kusimamishwa kwa usafirishwaji wa makinikia kumekuwa kukiikosesha takribani $15 milioni (Dola milioni kumi na tano) kwa mwezi.

Acacia wanasema hali hiyo imesababisha uendeshaji wa siku hadi siku wa moja ya migodi yake mikubwa Bulyanhulu kuathiriwa kwa kiasi kikubwa.

Acacia imekuwa katika mgogoro na serikali ya Tanzania kwa takribani miezi sita sasa tangu serikali ya Tanzania izuie usafirishwaji wa makinikia ya kampuni hiyo nje ya nchi.

Lakini serikali ya Tanzania pia imekuwa ikiishutumu kampuni ya Acacia kwa kukwepa kulipa kodi inayostahili, tuhuma ambazo kampuni hiyo imezikanusha.

Mazungumzo yanayolenga kutatua mgogoro huu bado yanaendelea.

"Kampuni ina matumaini kwamba majadiliano yanayoendelea kati ya Barrick na serikali ya Tanzania yatatatua kuzuiwa kwa usafirishaji wa makinikia na kurudisha mazingira ya uendeshaji wa mgodi wa Bulyanhulu katika hali nzuri" inasema taarifa ya Acacia.

Mapema mwaka huu Rais John Magufuli aliamuru uchunguzi wa kina katika sekta ya madini nchini Tanzania huku akiamini kwamba Tanzania hainufaiki vya kutosha kutokana na sekta ya madini.


Chanzo: BBC

VIDEO | TAZAMA ROMA-ZIMBABWE WIMBO MPYA

Huu ni wimbo mpya wa Roma Mkatoliki. VENANCE BLOG inakupa nafasi ya kuutazama hapa chini: