MTANDAO WA TWITTER KUONGEZA MANENO HADI 280
Mtandao wa Twitter kwa sasa upo katika majaribio ya kuongeza maandishi yake kutoka 140 hadi 280 hii ikiwa ni mara mbili ya hayo ya awali.
Sababu za kuongeza idadi hiyo ya maneno ni kwamba kuna wakati mtu unaweza kuwa na hoja fulani inayozidi ukomo wa maneno lakini ukashindwa kuiandika ama ukapunguza idadi ya maneno ambayo wakati mwingine huwa ni ya muhimu sana katika tweet husika.
Huu ni mfano wa vile tweet ya sasa ilivyo na vile ambavyo ongezeko litakuwa kwa maneno 280. |
Afisa Masoko Aliza Rosen wa Twitter na Mhandisi wa Twitter Japan Ikuhiro Ihara wamesema kuwa katika mchakato wa kuruhusu jambo hili watu wachache watachaguliwa kwa majaribio na pia watakuwa wakikusanya maoni na kupata mrejesho kutoka kwa watumiaji wa Twitter kabla hawajafikia uamuzi wa kuruhusu ongezeko hilo la maneno.
Jinsi tweet za Kiingereza na Kispanyola zinavyokuwa ukilinganisha na Kijapan. |
Zipo lugha ambazo hazitahusika kabisa katika jaribio ambazo ni Kichina, Kijapan na Kikorea sababu ni kwamba karibia 0.4% ya watu wanaotweet kwa lugha hizo hasa kijapan ndiyo hufikia ukomo wa sasa uliopo wakati lugha kama Kifaransa, Kiingereza, Kispanyora na nyinginezo 9% ya wanaotweet hufika ukomo wa maneno 140 kwa hiyo wakaona umuhimu wa kuongeza maneno.
Aidha utafiti uliofanywa na mtandao huo unadai kuwa watu wengi wanakasirishwa na ukomo wa idadi hiyo ya maneno.
Comments
Post a Comment