ZIFAHAMU GAUNI BORA 20 ZA MWAKA 2017

Uhali gani msomaji wa VENANCE BLOG? Natumai u mzima, leo nakukaribisha kuzifahamu gauni 20 bora za mwaka 2017 zilizovaliwa na nyota wa fasheni na mitindo uli mwenguni.  Tuanze uchambuzi wetu.

Huyuy ni Natalie Potman. Muigizaji maarufu katika kiwanda cha filamu Marekani Hollywood. Huenda miezi tisa ya ujauzito huwa migumu sana lakini Natalie hakuchoka katika hilo. Gauni hili ni ubunifu wa Prada na alilivaa katika tuzo za Golden Globe Awrds, unaweza kuona gauni lilivo zuri na kumpendeza mjamzito na mimba yake hapo juu. Unapenda fasheni na mitindo? Basi hili litamfaa zaidi mjamzito.

Mwingine huyu. Anaitwa Brie Leson muigizaji mwingine kutoka kiwanda cha filamu Marekani. Brie alivaa gauni hili katika katika tuzo za 89 za Academy Awards. Ni ubunifu wa mwanamitindo Oscar de la Renta. Unaionaje gauni hiyo? Bila shaka kimpasuo hiko kidogo kinapendeza sana pamoja na mchanuo ule wa nyuma kama maua. Haya kazi kwako kupendeza na mtindo huu kwenye red carpet.

Huwezi kushindwa kumtambua mdada huyu mpenda fasheni na mitindo. Anafahamika kama Rihanna. Mtindo huu unafahamika kwa jina la Kawakubo. Nadhani unaona jinsi ulivyompendeza Rihanna pamoja na kiatu chake. Je, unaweza kuuvaa mtindo huu? Haya jibu liwe siri yako.

Mwanamitindo wa Uingereza Bella Hadid pia yupo katika orodha yetu. Mwanamitindo huyu alitimiza miaka 21 mwaka huu. Gauni hii imebuniwa na Ralph & Russo. Imekaaje hii gauni kwa upabde wako? Unaweza kuvaa? Bila shaka jibu lako ni ndio na mazingira yake pia unayafahamu.

Anaitwa Gigi Hadid. Huyu ni ndugu na mwanamitindo wetu hapo juu, Bella Hadid. Ana miaka 22. Ni ubunifu wa Mary-Kate na Asley Olsen. Haya kazi kwako mpenda fashion.

Anafahamika kama Isabelle Huppert. Kama unavyoona hapo katika red carpet, mdada huyu alipendeza katika gauni lake alipokuwa akifanya promo ya tangazo la Elle. Chukua nyingine hiyo.

Huyu ni Natalie Dyer. Unaambiwa vazi hili linafaa kwa mtoko na mpenzi wako. Ni vazi la mchanganyiko wa rangi za pinki na nyekundu. Unapotoka na mpenzi wako kwa mara ya kwanza kabisa baada ya makuba baada ya kukaa muda mrefu bila kutoka, gauni hili litakupendeza sana.

Wanafahamika kama The Dutches of Cambridge. Gauni hili ni ubunifu kutoka McQueen na lilivaliwa katika tuzo za Bafta. Nadhani unaona hapo rangi nyeusi inavyopendeza. Kiujumla couple hii ilipendeza sana.

Anaitwa Penelope Cruz. Huu ni ubunifu wa kampuni maarufu ya nguo duniani Versace. Penelope alipendeza katika red carpet ya British Academy Film Awards.

Unapenda gauni za kubana juu bila kuwa na mikanda ya kukushikilia kwenye mabega? Hii inakufaa sana. Rangi ya pinki nzuri sana kwa wadada. Anaitwa Lily-Rose Depp. Hkika gauni hii inapendeza sana sio siri. Ubunifu huu unaitea The Channel.

Muigizaji Kristin Scott Thomas pia alipendeza na ggauni hili. ilikuwa ni katika kusherehekea miaka 70 ya Cannee. Make up aliyofanyiwa siku hii pamoja na gauni lake vilimfanya apendeza sana.

Sienna Miller pia amehusika katika orodha yetu kwa gauni lake hili la ubunifu wa Gucci. Hii ilikuwa mapema sana mwezi Januari katika uzinduzi wa gauni la Alessandro Michelle. Gauni lake hilo lenye muundo wa mawimbi fulani na lipsi nyekundu vilimfanya apendeze sana.

Claire Foy pia anahusika katika orodha yetu. Gauni hili lenye mkia nyuma pamoja na utepe hapo kiunoni ilimfanya apendeze sana. Claire amekuwa moja ya waigizaji na wanamitindo aliypamba katika ukurasa wa mbele wa jarida maarufu la mitindo nchini Uingereza la Vogue. Ubunifu huu ni maarufu kama Erdem. Hii ilikuwa ni katika jukwaa maarufu la maonesho la The Crown.

Hakika red carpet inapendeza sana. Unamuoana Elle Fanning alivyopendeza? Ni katika anniversary ya Cannes. Gauni hili limetengenezwa kwa vito pamoja na material za almasi. Nadhani unafahamu kwamba madini ya almasi hung'aa sana.

Bila shaka unaona rangi hii sio ya kizungu zaidi. Anaitwa Ruth Negga ni muigizaji anaykuja vizuri katika tasnia ya filamu nchini Uingereza bila shaka na duniani kote. Muigizaji huyu ni raia wa Uingerza mwenye asili ya Ethiopia na Ireland. Bai gauni lake hili ni ubunifu wa Louis Vuitton. Hii ilikuwa ni katika tuzo za Golden Globe Awards. 

 Anaitwa Emma Stone. Ubunidu guu unajulikana kama Givenchy Haute Couture ambao ni hatimiliki ya mbunifu Riccardo Tisci. Ubunifu huu ulimfanya Emma awe na muonekano mzuri.

Unamuona Marion Cotillard, yupo katika ubunifu wa Halpern. Mwaka 2017 ni mwaka ambao Halpern amehitimu kutoka Central Saint  Martins ambako alikuwa akisomea mabo ya mitindo hasa hasa ubunifu wa kumpendezesha mtu kwenye red carpet. Gauni hili hili limewapa sifa mbunifu pamoja Marion kiasi cha kufanya mbunifu Halpern kuchukua tuzo yake ya kwanza katika masuala ya fashion.

Anaitwa Cara Delevingne. Huu ni ubunifu wa Iris van Heprn.Bila shaka unafahamu kwamba unapotakiwa kufanya tangazo la kitu chochote lazima uonekane vizuri. Hapa Cara alikuwa katika tangazo la Valerian.

Emma Watson alihitajika katika kutengeneza muvi ya Disney ambayo ina maudhui ya karne ya 21. Ili kupata vazi linaloendana na maudhui ya muvi iliwapa Emma na team yake kuandaa documentary ya The Press kwa ajili ya upatikanaji wa nguo hii ambapo alishinda mwanamitindo Emilia Wickstead kwa ubunifu huo unaouona hapo pichani.

Tumalize na Keira Knightley. Hii ni kutoka katika collection maarufu ya mavazi ijulikanayo kama Spring/Summer 2018 Colletion. Keira pia aliamua kupanda kwenye red carpet kwa gauni hili mapema mwezi hu. Gauni hili ni maarufu kwa jina la Valentino.

Kama una maoni kuhusu makala hii na mengineyo, nitumie kwa WhatsApp namba 0712586027, ama barua pepe venancegilbert@gmail.com, pia Facebook VENANCE BLOG pamoja na Twitter @Venancetz. Usisite kutembelea VENANCE BLOG wakati wowote.

MAKALA HII IMEANDALIWA KWA HISANI YA JARIDA MAARUFU LA MITINDO NCHINI UINGEREZA LA THE VOGUE NA KULETWA KWAKO NA VENANCE GILBERT. PICHA ZOTE NI KWA HISANI YA GETTY IMAGES.

Comments

  1. Helllo to every body, it's my first go too see of
    this blog; this weblog includes amazing and genuinely excellent stuff
    in support of readers.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017