TETESI ZA UHAMISHO ULAYA: NANI WANATARAJIWA KUHAMIA KLABU MPYA JANUARI?
Ni wakati mwengine wa mwaka ambapo
uvumi utaanza kusambaa. Uhamisho wa mwaka uliopita haukuwa na changamoto
nyingi kutoka kwa timu sita bora katika ligi ya Uingereza huku timu
zote za ligi hiyo zikitumia £215m mwezi Januari.
Wakati huu itakuwaje, Je timu kubwa zitagharamika kununua wachezaji?
Barani Ulaya...
Dirisha
la uhamisho katika ligi tano kuu litafungwa kwa wakati mmoja. Dirisha
la uhamisho la klabu za Uingereza, Ufaransa , Ujerumani , Italia na
Uhispania litafungwa Desemba 31 mwaka huu
DIEGO LOPEZ (klabu: Espanyol; Safu: kipa; Umri: 36)
Anahusishwa na uhamisho wa :Crystal Palace.
Ni
kipa anayejulikana kwa kupigania nafasi ya kipa na Iker Casillas katika
klabu ya Real Madrid, alikuwa katika benchi wakati Reala Madrid
iliposhinda kombe la vilabu bingwa 2014 na amekuwa mchezaji wa Ziada wa
Espanyol kwa kipindi kirefu cha msimu. Pia aliichezea Villarreal,
Sevilla na AC Milan.
KEVIN TRAPP (Paris St-Germain; kipa; 27)
Anahusishwa na uhamisho wa : Crystal Palace, Borussia Dortmund, Liverpool.
Mkufunzi
wa PSG boss Unai Emery ana mpendelea sana kipa Alphonse Areola, na
kipa raia wa Ujerumani Trapp ameanza kukerwa kutokana na ukosefu wa
fursa ya kuiwakiulisha timu yake hususan wakati huu ambapo wachezaji
wanajianda kuziwakilisha timu zao za kimataifa katika kombe la dunia
DANIEL OPARE (Augsburg; Beki; 27)
Anahusishwa na uhamisho wa : West Ham, Stoke City, Everton, Swansea.
Mchezaji
huyo wa kimataifa wa Ghana ana uwezo wa kucheza kama beki wa kulia ama
kushoto na anasakwa na baadhi ya vilabu vya Uingereza.Amekamilisha
kandarasi yake na Augsburg na huenda klabu hiyo ya UJerumani inataka
kumuuza.
LEON GORETZKA (Schalke; kiungo wa kati ; 22)
Anahusishwa na uhamisho wa: Manchester United, Arsenal, Barcelona.
Alikuwa
katika kikosi cha Ujerumani kilichoshinda kombe la shirikisho ,Goretzka
anafananishwa na kiungo wa kati wa zamani wa Manchester United Paul
Scholes. Anakamilisha kandarasi yake mna yuko tayari kuondoka ili kupata
changamoto mpya.
STEVEN NZONZI (Sevilla; kiungo wa kati; 29)
Anahusishwa na uhamisho wa: Everton, Arsenal.
Mchezaji
huyo wa zamani wa Stoke na Blackburnalihusishwa na uhamisho wa kurudi
katika ligi ya Uingereza baada ya kudaiwa kuzozana na mkufunzi wa zamani
wa Sevilla Eduardo Berizzo, ambaye alifutwa kazi mnamo tarehe 22
Disemba. Uzoefu wake wa soka ya Uingereza kunaweza kumfanya kuwa kiungo
muhimu.
ARDA TURAN (Barcelona; kiungo wa kati ; 30)
Anahusishwa na uhamisho wa : Arsenal, Trabzonspor.
Mchezaji
huyo wa Uturuki hajaichezea Barcelona tangu mkufunzi Ernesto Valverde
kuchukua usimamizi wa klabu hiyo. Ametngaza wazi kwamba anataka kuondoka
Nou Camp mnamo mwezi Januari.
JEAN MICHAEL SERI (Nice; kiungo wa kati ; 26)
Anahusishwa na uhamisho wa : Barcelona, Manchester City, Liverpool.
Mchezaji
huyo wa Ivory Coast alikuwa akiwindwa na Barcelona katika dirisha la
uhamisho lililopita, lakini Nice ilikataa ombi la viongozi hao wa La
Liga . Nice imaimarika baada ya kupata matyokeo mabaya , na huku uwezo
wa klabu hiyo wa kufuzu kushiriki katika kombe la vilabu bingwa ukiwa
mchache , Seri anaweza kutaka kuondoka mwezi Januari.
JAVIER PASTORE (Paris St-Germain; kiungo wa kati mshambuliaji ; 28)
Anahusishwa na uhamisho wa klabu za: Liverpool, Sevilla, Inter Milan.
Mchezaji
mwenye kipaji ambaye hajathibitishiwa kuwa ataorodheshwa katika kikosi
cha kwanza cha PSG , Pastore alitajwa kuwa mchezaji bora duniani na
Eric Cantona, ambaye anasema angependelea iwapo Patore angesajiliwa na
man United .Mchezaji huyo wa Argentina anapigiwa upato kuwa mchezaji
muhimu katika kombe la dunia.
GELSON MARTINS (Sporting Lisbon; Winga; 22)
Anahusishwa na uhamisho wa : Liverpool.
Sporting Lisbon inahitaji kitita kikubwa , na Martins anasemekana
kuwa dau la kuondoka lakini mchezo wake katika ligi ya Ureno umevutia
maoni yasio ya kawaida.
THOMAS LEMAR (Monaco; Winga/kiungo wa kati mshambuliaji; 22)
Anahusishwa na uhamisho wa : Arsenal, Chelsea, Liverpool.
NI
miongoni mwa nyota wa klabu ya Monaco ilioshinda ligi msimu uliopita ,
na sasa ameorodheshwa katika kikosi cha Ufaransa ambapo amefunga mabao
mawili dhidi ya Uholansi katika mechi ya kirafiki mnamo mwezi Novemba.
Arsenal na Liverpool zilijaribu kumsajili katika dirisha la uhamisho lililopita.
HATEM BEN ARFA (Paris St-Germain; Winga/mshambuliaji /kiungo wa kati ; 30)
Anahusishwa na uhamisho wa : Leicester City.
Baada
ya msimu mzuri na Nice msimu uliopita 2015-2016, uhamisho wake hadi
PSG haikuingiliana. Soka yake imekwama chini ya usimamizi wa Emery,
ambaye haonekani kutakab kumpatia fursa ya kucheza katika kikosi cha
kwanza. Meneja wa Ben Arfa's katika klabu ya Nice alikuwa Claude Puel,
na huenda kuna uvumi kwamba huenda wakakutana tena katika klabu ya
Leicester.
MAKALA HII NI KWA HISANI YA BBC.
Comments
Post a Comment