ORODHA YA WALICHAGULIWA AMUCTA (SAUT-TABORA) HII HAPA

Chuo Kikuu Kishiriki Archibishop Mihayo cha Tabora (Tawi la SAUT) kimetoa majina ya waliochaguliwa kujiunga na kozi za shahada mwaka wa masomo 2016/2017.

👉MAJINA YAPO HAPA BOFYA👈

SELECTED STUDENTS TO JOIN UNIVERSITY OF ARUSHA (BACHELOR DEGREE PROGRAMMMES)

Chuo Kikuu cha Arusha kimetoa majina ya waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho kwa kozi mbalimbali za Shahada kwa mwaka wa masomo 2016/2017. Waliochavuliwa wanatakiwa kuripoti chuoni hapo kuanzia Oktoba 9.

 BOFA HAPA KUANGALIA MAJINA

YAFAHAMU HAYA KUTOKA BODI YA MIKOPO (HESLB)

Jana katika kipindi cha Dakika 45 ambacho hurushwa kila Jumatatu saa 3 usiku kupitia ITV/Radio One, Sam Mahela mtangazaji wa kipindi hicho alipata nafasi ya kufanya mahojiano na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo, Mh. Abdul Razaq Badru ambaye ameteuliwa na Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako kufahamu mambo fulani kuhusu HESLB.

Mkurugenzi huyo alianza kwa kubainisha kuwa tangu kuanzishwa kwake HESLB imekopesha watu laki tatu na ishirini na nne (300,024). Aliongeza kuwa makato ya fedha kwa wale ambao walinufaika na mikopo ya elimu ya juu yanaendelea. Pia alibainisha kwamba kumekuwepo na dosari katika kuwakata watu 200 ambao hawakuwahi kunufaika na mikopo ya elimu ya juu na kusisitiza kwamba kama kuna mtu anakatwa na hakukopeshwa na bodi hiyo atoe taarifa katika Ofisi zilizojirani naye. Lakino pia alidai kuwa waliokatwa kimakosa watarudishiwa fedha zao.

Mkurugenzi aliongeza kuwa Bodi imekopesha jumla ya Tsh. Trilioni 2.4 (waliowahi kukopeshwa na wanaondelea na masomo kwa mwaka 2015/2016) na kwamba kiasi kilichorejeshwa ni Tsh Bilioni 284 na zilizokusanywa ni kiasi cha Tsh Bilioni 105. Mkurugenzi alibainisha kuwa kwa mwaka wa masomo/fedha 2015/2016 ilitakiwa mkopo jumla utolewe Tsh Bilioni 400 na kiasi kadhaa lakini Rais Magufuli alipoingia madarakani aliongeza kiasi cha Tsh Bilioni 132. Ikumbukwe kwamba fedha hizi ni zile za kujikimu, vitabu na maktaba, ada ya chuo pamoja na gharama ya mafunzo kwa vitendo.

Kuhusu kukatwa fedha kwa wafanyakazi walioajiriwa katika taasisi binafsi Mkurugenzi alidai kuwa elimu inatolewa kwa waajiri kuhusu kukata fedha hiyo kwa mujibu wa sheria. Aidha Mkurugenzi aliongeza kwamba muda wa kurejesha mkopo huo ni baada ya miaka 10 toka mnufaika amalize masomo yake bila kujali ameajiriwa au la! Aliongeza kuwa inapopita miaka 10 bila mnufaika kujeresha kiasi hicho, kunakuwa na faini ya 6% kwa mwaka kwa jumla ya miaka yote ambayo mnufaika atakuwa amechelewa kurejesha mkopo.
Kuhusu mwaka wa masomo 2016/2017, Mkurugenzi alidai kuwa wanafunzi elfu themanini na nane 88,000 ndiyo wameomba kunufaika na mikopo hiyo na kwamba zoezi la kupitia wenye sifa za kukopeshwa bado linaendelea.

Lakini pia Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa mpaka sasa Vyuo vimerejesha kiasi cha Tsh Bilioni 1 na laki 2 (1,000,200,000/=) kati ya Tsh Bilioni 2 na laki 7 (2,000,700,000/=) fedha ambazo zilitumika kwa wanafunzi hewa. Hili alilibainisha alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Sam Mahela kuhusu kiasi cha Tsh Bilioni 14 (14,000,000,000) kutumika kuwalipa wanafunzi hewa.

Aidha Mkurugenzi huyo alisema kwamba kuhusu utoaji wa mikopo unafata vigezo kama muombaji anafaa. Hili alilibainisha wakati akijibu swali kuhusu kushuka kwa udahili wa waliosoma Diploma kutoka GPA ya 3.5 hadi 3.0 kama wanaweza kunufaika na mkopo kutoka HESLB. Mkurigenzi alibainisha kuwa watu wenye mahitaji mkubwa kama vile Yatima, Walemavu na Wale wanaotoka katika hali duni pamoja na Watakaosoma kozi za uhandisi, uhandisi wa mafuta na gesi, Ualimu wa Sayansi na Hisabati pamoja na Udaktari hao watapakuwa na kipaumbele kunufaika na mkopo wa Elimu ya Juu.

Mkurugenzi alipoulizwa kuhusu wanafunzi waliokuwa wakisoma Diploma maalum ya Ualimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma na kuhamishiwa katika vyuo vingine kama wanaweza kunufaika tena mikopo, alidai kuwa utaratibu maalumu utatolewa na Serikali panapostahili.

Mkurugenzi pia alibainisha kuwa Bodi ya Mikopo (HESLB) inafanya kazi kwa ushirikiano kabisa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na kwamba ili mwanafunzi apatiwa mkopo sharti adailiwe kupitia TCU kama kigezo cha kwanza kupata mkopo wa Elimu ya Juu na kuwatoa hofu wanafunzi, wazazi na wadau wa Elimu kuhusu kuwepo awamu mbalimbali za Udahili TCU kuwa hakutokwamisha suala la ukopeshwaji kwa wenye sifa stahiki.

Pia alibainisha kuwa kiasi cha fedha Tsh Bilioni Mia tano (500,000,000,000) zimetengwa na Wizara kuhudumia mikopo ya Wanafunzi wa elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

Chuo cha Mipango ama Institute of Rural Development Planning kimetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali za shahada (Bachelor Degree) chuoni hapo mwa mwaka wa masomo 2016/207.

BOFYA HAPA KUANGALIA MAJINA HAYO

IMPORTANT NOTICES TO SELECTED STUDENTS

The selected candidates must report at the Institute’s main campus Miyuji area on Monday 17
th October, 2016 ready for orientation program.
Joining instructions can be downloaded from the website www.irdp.ac.tz and can also be collected from the main campus admission office.
Tuition fees for Bachelor Degree courses 850,000/= Registration fee is 50,000/=, Students organization fee 20,000/= sports and games is 10,000/=
and NACTE Quality Assurance Fee 20,000/=. Students are required to pay atleast half of the tuition fee and 100,000/= for registration, students
organization, sports and games and NACTE Quality Assurance Fee. The payment should be made through CRDB Bank account no. 01J1082678600 before 17
th October, 2016. It should be noted that, any money
once deposited in the IRDP account shall not be refunded.
On arrival at the Institute, please bring your original certificates of your academic qualifications, birth certificate and bank pay in slip. Note that,
expired examination results slip will not be accepted.

HAYA HAPA MAJINA 10,027 YA WALIOKOSEA KATIKA UOMBAJI WA MKOPO HESLB 2016

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
(HESLB) imetangaza majina ya watu elfu kumi na ishirini na saba ambao form zao zimeonekana kuwa na dosari ktk suala zima la upitiaji wa fomu hizo.

Bodi inawataka waombaji na wadhamini ambao hawakusaini ktk fom hizo kufika ktk ofisi za bodi hiyo Plot 8, Block 46 Barabara ya Sam Nujoma Mwenge  DSM ili kutia saini ktk fomu hizo kuanzi Jumatatu October 3.

Kwa wale ambayo hawakuweka taarifa kama vile picha, picha ya mdhamini, taarifa za mdhamini kama vile kopi ya pasi ya kusafiria ama kitambulisho cha mpiga kura, ama wametima kopi ambazo hazijthibitishwa na kamishna wa vizazi na viapo wanatakiwa kutuma taarifa hizo wakionesha jina kamili la mwombaji mkopo pamoja na taarifa hizo na namba ya Kidato cha 4 na mwaka uliohitimu kwa mfano S3370.0004.2013 kisha watume taarifa hizo kwa njia ya EMS kwenda ktk anwani hii:

The Executive Director,
Higher Education Students’ Loans Board,
P. O. Box 76068,
DAR ES SALAAM.


Mwisho wa kusahihisha makosa hayo ni Ijumaa Oktoba 7, mwaka huu.

Aidha Bodi inakumbusha kwamba:

°Waombaji wanatakiwa kuwa makini na watu ambao watatumia mwaya huu kutaka kuwatapeli katika zoezi hili kwa kuwaomba fedha.

°Kusahihisha taarifa za mkopo hakaanishi kuwa mwombaji lazima apate mkopo wa Elimu ya Juu.

°Fomu ambazo zitakuwa hazijatimiza taarifa zote za uombaji mkopo hazitashughulikiwa hadi pale taarifa hizo zitakapokamilika kwa muda husika.

°MAJINA YA WAOMBAJI AMBAO FOMU ZAO ZINA MAKOSA HAYA HAPA. BOFYA HAPA KUYAONA



VENANCE BLOG IKO NA WEWE KTK TAARIFA ZOTE ZA KIELIMU.

WALIOCHAGULIWA SUA MAJINA YAO HAYA HAPA

Chuo Kikuu Cha Kilimo Sokoine (SUA) Kimetoa majina yabwaliochaguliwa kujiunga chuoni hapo na kwamba wanatakiwa kuripoti mapema kwani mwaka wa masomo utaanza October 17.

BOFYA HAPA KUANGALI MAJINA HAYO

WALIOCHAGULIWA TEKU MAJINA YAPO HAPA

Chuo Kikuu Theofilo Kisanji (TEKU) kimetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho ktk mwaka wa masomo 2016/2017.

BOFYA HAPA KUANAGALIA MAJINA


VENANCE BLOG ITAENDELEA KUSOGEZA SELECTION HIZO ZA VYUO MBALIMBALI KADIRI ZINAVYOTOKA.

SELECTION ZA TUMAINI MAKUMIRA NA UNIVERSITY OF IRINGA ZIPO HAPA

Tumaini Makumira

University of Iringa

Chuo Kikuu cha Iringa na Chuo Kikuu Tumaini Makumira vimetoa majina ya waliochaguliwa katika vyuo hivyo.





Uangaliaji wa majina ktk vyuo hivi ni tofauti kwani wao hawatumii Index ya form 4 wala 6 ni majina tu, hivyo kama uliapply na unataka kuona jina tuma jina lako kwenda namba 0753400208. Huduma hii ni bure kabisa.

WALIOCHAGULIWA BUGANDO (CUHAS) MAJINA HAYA HAPA

Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Kikatoliki (Bugando) (CUHAS) kimetoa majina ya wanafunzi mbalimbali waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho.

BOFYA HAPA KUANGALIA MAJINA

Aidha unaweza kutuma jina lako na index ya form four au six bila kusahau kozi uliyoomba chuoni hapo kwenda namba 0753400208 na utaangaliziwa jina bure kabisa.

WALIOCHAGULIWA UDSM, DUCE NA MKWAWA BATCH 1 MAJINA HAYA HAPA



Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na matawi yake DUCE na MKWAWA (MUCE) kimetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kozi mbalimbali za shahada chuoni hapo kwa mwaka wa masomo 2016/2017.



Unaweza kutuma jina lako, pamoja na namba ya kidato ya cha 4 au 6 kwenda namba 0753400208 na utaangaliziwa jina BURE. Kumbuka kutuma jina lako, index ya 4 au 6 na chuo unachotaka kuangalia hata kama ni zaidi ya kimoja. Mfano: Venance Gilbert s2509/0575/2012 (iv) au s0494/0141/2015 (vi) Mzumbe, MUHAS, SUA, UDSM, UDOM, SAUT n.k. kwenda 0753400208. Huduma hii ni BURE.

MAJINA YA WALIOCHAGULIWA UDOM BACHELOR DEGREE YAPO HAPA


Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Ili kuona matokeo haya kwa njia ya  simu hakikisha simu yako ina WPS Office, Polaris Office n.k. kisha BONYEZA HAPA KUANGALIA MAJINA HAYO

VENANCE BLOG IKO NA WEWE, UKISHINDWA KUANGALIA MAJINA HAYO TUMA UJUMBE MFUPI (SMS) UKIANDIKA JINA LAKO NA INDEX YA KIDATO CHA 4 AU 6 KWENDA NAMBA 0753400208 UTAANGALIZIWA JINA LAKO BURE KABISA KUPEWA MAJIBU.

WALIOCHAGULIWA KOZI ZA SHAHADA CBE KAMPASI YA DAR ES SALAAM

Chuo cha Elimu ya Biashara kimetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho kwa mwaka wa kwanza wa masomo 2016/2017.
Majina yapo hapa. Kumbuka hili ni toleo la kwanza (First Batch). BOFYA HAPA KUANGALIA

WALIOCHAGULIWA KOZI MBALIMBALI ZA SHAHADA IFM

  Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM) imetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kusoma kozi mbalimbali za Shahada katika fani mbali mbali chuoni hapo.

Majina hayo yako hapa. BOFYA HAPA KUONA MAJINA HAYO

MAJINA YA WALIOCHAGULIWA CHUO KIKUU TUMAINI MAKUMIRA KAMPAS YA MBEYA HAYA HAPA



Chuo Kikuu Tumaini Makumira kampus ya Mbeya kimetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Chuo hicho kwa kozi za Shahada ya Elimu na Sanaa (Bachelor of Arts with Education BA.Ed) na Shahada ya Elimu katika Sanaa (Bachelor of Education in Arts BED). Majina hayo yapo kwenye tovuti ya Chuo toka juzi Septemba 15.

KUANGALIA BA.Ed BOFYA HAPA

KUANGALIA BEd BOFYA HAPA

Aidha taarifa zote za Chuo hiko unaweza kuzipata kwa KUBOFYA HAPA

VENANCE BLOG IKO NA WEWE KWA TAARIFA ZOTE ZA VYUO MBALIMBALI NCHINI. ENDELEA KUWA NAMI.

HILLARY CLINTON AMEREJEA KATIKA KAMPENI NA KUMSHAMBULIA TRUMP

Mgombea wa chama cha Democratic katika kinyan'ganyiro cha urais nchini Marekani Hillary Clinton amerejea tena katika kampeni na kutoa kauli ya tahadhari dhidi ya mpinzani wake Donald Trump.

Mgombea wa chama cha Democrats Hillary Clinton akiwahutubia wafuasi wake North Carolina
Mgombea wa chama cha Democrats Hillary Clinton akiwahutubia wafuasi wake North Carolina

Akizungumza katika mikutano miwili tofauti ya kampeni kwenye majimbo mawili, North Carolina na Washington, Hillary Clinton alisema amefurahi kurejea katika kampeni hizo baada ya hapo awali kushauriwa na madaktari kubakia nyumbani hadi atakapopata nafuu kutokana na maradhi ya homa ya mapafu yaliyokuwa yakimkabili.

Hali ya afya ya Hillary Clinton ilidhoofika wakati wa kumbukumbu ya mika 15 tangu yalipofanyika mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani tarehe 11/9/ 2001.

"Ni jambo jema kuwa nimerejea katika kampeni" alisema mgombea huyo wa chama cha Democratic huku akishangiliwa na wafuasi wake alipohutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika eneo la Greensboro, North Carolina.

Hillary Clinton alitangaza kuendelea na mikutano ya kampeni katika majimbo ambayo mgombea wa chama cha Republican Donald Trump amekwishafanya mikutano yake ya kampeni ikiwa ni pamoja na jimbo la Florida ambalo kila mgombea anawania kulichukua.

Wakati suala la afya ya wagombea wote wawili likizua mjadala katika mikutano ya kampeni ya viongozi hao , Hillary Clinton alienda mbali zaidi kwa kutoa taarifa zinazohusiana na afya yake akisema ni mwenye afya njema na anaweza vema kutekeleza majukumu ya uongozi. Kwa upande mwingine wakati mgombea wa chama cha Republican Donald Trump akionekana kuwa na uzito mkubwa daktari wake alithibitisha kuwa mgombea huyo ana afya njema.
Hillary Clinton amshambulia Trump
Bildkombo Donald Trump und Hillary Clinton
Akizungumza katika mikutano hiyo ya kampeni Hillary Clinton hakusita kumshambulia kwa maneno Donald Trump kutokana na kauli ya awali aliyoitoa akikataa kusema iwapo ana amini kuwa Rais Barack Obama ni mzaliwa wa Marekani na pia kumkashifu mchungaji mwenye asili ya Afrika ambapo Trump alitembelea kanisa lake mjini Michigan wiki hii.

Kwa miaka kadhaa Donald Trump alikuwa akiendesha harakati akihoji kama Rais Barack Obama amezaliwa nchini Marekani na kutumia majukwaa kutangaza kuwa Rais huyo wa sasa wa Marekani alizaliwa nje ya nchi hiyo na kuwa hakusitahili kuwa Rais wa nchi hiyo kwa mujibu wa katiba ya Marekani.

Hapo jana wakati Trump alipohojiwa na gazeti la Washington Post iwapo ana amini kuwa Rais Obama alizaliwa mjini Hawaii, alishindwa kutoa jibu kwa mara nyingine akisema atajibu swali hilo wakati muafaka utakapowadia. Hata hivyo taarifa iliyotolewa baadaye na waratibu wa mikutano ya kampeni ya mgombea huyo ilisema Trump ana amini kuwa Rais Obama alizaliwa nchini Marekani.

" Baada ya kufanikiwa kupata cheti cha kuzaliwa cha Rais Barack Obama wakati wengine wameshindwa , Donald Trump sasa ana amini kuwa Rais Obama ni mzaliwa wa Marekani " ilisisitiza taarifa hiyo.

Aidha mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton alisema kitendo cha Trump kumshambulia mchungaji kinazidi kumnyima sifa Trump za kuwa Rais wa nchi hiyo na kuwataka wapiga kura kumkataa wakati wa uchaguzi wa mwezi Novemba.


Chanzo: DW