Posts

WALIOCHAGULIWA TEKU MAJINA YAPO HAPA

Image
Chuo Kikuu Theofilo Kisanji (TEKU) kimetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho ktk mwaka wa masomo 2016/2017. BOFYA HAPA KUANAGALIA MAJINA VENANCE BLOG ITAENDELEA KUSOGEZA SELECTION HIZO ZA VYUO MBALIMBALI KADIRI ZINAVYOTOKA.

SELECTION ZA TUMAINI MAKUMIRA NA UNIVERSITY OF IRINGA ZIPO HAPA

Image
Tumaini Makumira University of Iringa Chuo Kikuu cha Iringa na Chuo Kikuu Tumaini Makumira vimetoa majina ya waliochaguliwa katika vyuo hivyo. KWA TUMAINI MAKUMIRA BOFYA HAPA KWA UNIVERSITY OF IRINGA BOFYA HAPA Uangaliaji wa majina ktk vyuo hivi ni tofauti kwani wao hawatumii Index ya form 4 wala 6 ni majina tu, hivyo kama uliapply na unataka kuona jina tuma jina lako kwenda namba 0753400208. Huduma hii ni bure kabisa.

WALIOCHAGULIWA BUGANDO (CUHAS) MAJINA HAYA HAPA

Image
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Kikatoliki (Bugando) (CUHAS) kimetoa majina ya wanafunzi mbalimbali waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho. BOFYA HAPA KUANGALIA MAJINA Aidha unaweza kutuma jina lako na index ya form four au six bila kusahau kozi uliyoomba chuoni hapo kwenda namba 0753400208 na utaangaliziwa jina bure kabisa.

WALIOCHAGULIWA UDSM, DUCE NA MKWAWA BATCH 1 MAJINA HAYA HAPA

Image
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na matawi yake DUCE na MKWAWA (MUCE) kimetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kozi mbalimbali za shahada chuoni hapo kwa mwaka wa masomo 2016/2017. BOFYA HAPA KUANGALIA Unaweza kutuma jina lako, pamoja na namba ya kidato ya cha 4 au 6 kwenda namba 0753400208 na utaangaliziwa jina BURE . Kumbuka kutuma jina lako, index ya 4 au 6 na chuo unachotaka kuangalia hata kama ni zaidi ya kimoja. Mfano: Venance Gilbert s2509/0575/2012 (iv) au s0494/0141/2015 (vi) Mzumbe, MUHAS, SUA, UDSM, UDOM, SAUT n.k. kwenda 0753400208. Huduma hii ni BURE .

MAJINA YA WALIOCHAGULIWA UDOM BACHELOR DEGREE YAPO HAPA

Image
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho kwa mwaka wa masomo 2016/2017. Ili kuona matokeo haya kwa njia ya  simu hakikisha simu yako ina WPS Office, Polaris Office n.k. kisha  BONYEZA HAPA KUANGALIA MAJINA HAYO VENANCE BLOG IKO NA WEWE, UKISHINDWA KUANGALIA MAJINA HAYO TUMA UJUMBE MFUPI (SMS) UKIANDIKA JINA LAKO NA INDEX YA KIDATO CHA 4 AU 6 KWENDA NAMBA 0753400208 UTAANGALIZIWA JINA LAKO BURE KABISA KUPEWA MAJIBU.

WALIOCHAGULIWA KOZI ZA SHAHADA CBE KAMPASI YA DAR ES SALAAM

Image
Chuo cha Elimu ya Biashara kimetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho kwa mwaka wa kwanza wa masomo 2016/2017. Majina yapo hapa. Kumbuka hili ni toleo la kwanza (First Batch).  BOFYA HAPA KUANGALIA

WALIOCHAGULIWA KOZI MBALIMBALI ZA SHAHADA IFM

Image
  Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM) imetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kusoma kozi mbalimbali za Shahada katika fani mbali mbali chuoni hapo. Majina hayo yako hapa.  BOFYA HAPA KUONA MAJINA HAYO

MAJINA YA WALIOCHAGULIWA CHUO KIKUU TUMAINI MAKUMIRA KAMPAS YA MBEYA HAYA HAPA

Image
Chuo Kikuu Tumaini Makumira kampus ya Mbeya kimetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Chuo hicho kwa kozi za Shahada ya Elimu na Sanaa (Bachelor of Arts with Education BA.Ed) na Shahada ya Elimu katika Sanaa (Bachelor of Education in Arts BED). Majina hayo yapo kwenye tovuti ya Chuo toka juzi Septemba 15. KUANGALIA BA.Ed BOFYA HAPA KUANGALIA BEd BOFYA HAPA Aidha taarifa zote za Chuo hiko unaweza kuzipata kwa  KUBOFYA HAPA VENANCE BLOG IKO NA WEWE KWA TAARIFA ZOTE ZA VYUO MBALIMBALI NCHINI. ENDELEA KUWA NAMI.

HILLARY CLINTON AMEREJEA KATIKA KAMPENI NA KUMSHAMBULIA TRUMP

Image
Mgombea wa chama cha Democratic katika kinyan'ganyiro cha urais nchini Marekani Hillary Clinton amerejea tena katika kampeni na kutoa kauli ya tahadhari dhidi ya mpinzani wake Donald Trump. Mgombea wa chama cha Democrats Hillary Clinton akiwahutubia wafuasi wake North Carolina Akizungumza katika mikutano miwili tofauti ya kampeni kwenye majimbo mawili, North Carolina na Washington, Hillary Clinton alisema amefurahi kurejea katika kampeni hizo baada ya hapo awali kushauriwa na madaktari kubakia nyumbani hadi atakapopata nafuu kutokana na maradhi ya homa ya mapafu yaliyokuwa yakimkabili. Hali ya afya ya Hillary Clinton ilidhoofika wakati wa kumbukumbu ya mika 15 tangu yalipofanyika mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani tarehe 11/9/ 2001. "Ni jambo jema kuwa nimerejea katika kampeni" alisema mgombea huyo wa chama cha Democratic huku akishangiliwa na wafuasi wake alipohutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika eneo la Greensboro, North Carolina...

MTU MMOJA AMEJITOA MUHANGA NA KUUA WATU 16 KATIKA MSIKITI WA MOHMAND PAKISTAN

Image
Takribani watu 16 wameuawa na wengine 35 kujeruhiwa katika swala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Mohmand huko Pakistan. Duru za habari zinasema kuwa mtu huyo aliyejitoa muhanga ameua watu 16 na wengine 35 kujeruhiwa walipokuwa wakihudhuria swala ya Ijumaa kaskazini mashariki mwa  Pakistan. Shambulio hilo limetokea katika kijiji cha Anbar Tehsil katika wilaya inayokaliwa na kabila la Mohmand ambapo jeshi la Pakistan limekuwa likipambana na kundi la Taliban. "Swala ya Ijumaa ilikuwa ikiendelea msikitini hapo wakati ambapo mshambuliaji huyo wa kujitoa muhanga alijilipua na kuua waumini 16 na kujeruhi wengine 35" kiongozi mmoja wa Mohmand aliliambia shirika la habari la AFP. Hakujatokea taarifa zozote kuhusu shambulio hilo, lakini kundi la Taliban linashutumiwa kuhusika na shambulio hilo kwa kuwa limekuwa likifanya mashambulio katika maeneo ya mahakama, shule na misikiti. Jeshi la Pakistan limekuwa likifanya operesheni toka Juni 2014 kuangamiza makundi yote ya kigaidi yal...

LEO SEPTEMBA 14 KATIKA HISTORIA

Image
Rapa Nas Escobar alizaliwa September 13, 1973. Leo ni Jumatano Septemba 14, 2016. Ni siku ya 258 katika mwaka 2016. Zimesalia siku 108 kuukamilisha mwaka 2016. MATUKIO 1960 - Iraq, Iran, Kuwait na Saudi Arabia ziliunda jumuiya ya OPEC. 1979 - Nur Muhammad Tarak, Rais na na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Afghanistan aliuawa katika mapinduzi ambapo Waziri Mkuu Hafizullah Amin alishika madaraka. KUZALIWA 1849 - Mwanasaikolojia wa Urusi, Ivan Pavlov. 1864 - Robert Cecil,  miongoni mwa waanzilishi wa Jumuiya ya Mataifa alizaliwa. 1879 - Margaret Sanger, wakili na muanzilishi wa Uzazi wa mpango. 1973 - Rapa Nas Escobar alizaliwa. 

NEW AUDIO: DOWNLOAD BARAKA DA PRINCE FT ALI KIBA-NISAMEHE MP3

Image
Baraka Da Prince akishirikiana na Ali Kiba wanakusikilizisha kitu hiki hapa kipya, wimbo unaitwa Nisamehe umefanyikwa kwa Imma the Boy. DOWNLOAD HAPA

TCU IMERUHUSU UDAHILI VYUO VIKUU AWAMU YA PILI

Image
Tume ya Vyuo Vikuu nchini Tanzania (TCU) imeruhusu awamu ya pili ya udahili kwa wanafunzi waliokosa vyuo kwa kukosa sifa katika udahili wa awamu ya kwanza na wale ambao hawakuomba kudahiliwa kabisa. Aidha TCU inakumbusha kwamba wale waliokwisha omba na hawakupangiwa kwa kukosa sifa stahiki za vyuo walivyopangiwa hawatatakiwa kulipia tena. Pia wadahiliwa wapya wanatakiwa kulipia kiasi cha fedha za kitanzania Tsh. Elfu Hamsini (50,000/=) kama gharama za udahili. Fedha hii huwa hairudishwi. Vilevile TCU inakumbusha kwamba kozi ambazo zimejaa tayari hazitaonekana kwenye mfumo wa Udahili (CAS). Aidha TCU inawakumbusha waombaji kuwa mwisho wa kutuma maombi ya udahili ni Septemba 23 na hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza kwa wale watakaoshindw kuomba vyuo katika muda huo ulioongezwa. MAELEZO ZAIDI  BOFYA HAPA

IGGY AZALEA ASISITIZA YEYE NA FRENCH MONTANA NI MARAFIKI TU

Image
Iggy Azalea amekataa kuwa na uhusiano na French Montana japo wameonekana mara kadhaa wakiwa sehemu za starehe pamoja. Rapper huyo wa kike ameuambia mtandao wa TMZ kuwa hana mpenzi kwa sasa hivyo yeye na French Montana ni marafiki tu. “We are Single, I’m single,” amesema Iggy. “just friends.” Wiki kadhaa zilizopita Iggy alidai kuwa yeye na French Montana kuna wimbo wamefanya ila hawana mahusiano yoyote lakini baada ya wiki moja wawili hao walionekana wakiwa wanakula bata pamoja huko Cabo San Lucas, Mexico. Walionekana pia wakibusiana.

LEO SEPTEMBA 13 KATIKA HISTORIA

Image
Tarehe kama ya leo Septemba 13' Tupac Shakur alifariki. Leo Septemba 13 siku ya 257 katika mwaka 2016, zimesalia siku 109 kuukamilisha mwaka 2016. MATUKIO 1759 - Vikosi vya majeshi ya Uingerza viliyashinda majeshi ya Ufaransa katija mapigano kwenye nyanda za Abraham huko Quebec. 1914 - Wanaharakati wa Ireland waliomba msaada kwa wajerumani. 1940 - Italia iliivamia Misri. 1945 - Vikosi vya majeshi ya Uingereza viliingia Japan kupunguza uwezo wa jeshi la Japan. 1993 - Mkataba wa amani kusitisha mapigano Israel na Palestina ulisainiwa. VIFO 1996 - Mwanamuziki 2Pac Shakur alifariki. KWA MSAADA WA MTANDAO.