VIFAA VYA KUWATAMBUA WENYE UGONJWA WA EBOLA VYAINGIZWA NCHINI
Serikali imeanza kuingiza nchini vifaa vya kuwabaini watu wanaohisiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa homa kali ya ebola ambavyo vitawekwa kwenye viwanja vya ndege pamoja na baadhi ya maeneo ya mipakani. Jana Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Steven Kebwe alikabidhi mashine nne za kuwapima abiria wanaoingia nchini kupitia viwanja vya ndege bila kuwagusa. Vifaa hivyo vinabaini mtu kuwa na dalili za ebola kutokana na joto lake na abiria wanapimwa kwa kumulikwa machoni na kwenye masikio. Kwa kuanzia mashine hizo ambazo ni mfano wa kamera zitapelekwa kwenye viwanja vya ndege vya Mwanza, Kilimanjaro, Zanzibar na Dar es Salaam. Maeneo hayo kwa mujibu wa naibu waziri huyo ndiyo yanapokea wagonjwa wengi kutoka nje ya nchi. Dk Kebwe pia aliagiza shehena ya mashine zingine zitakazoingizwa nchini kuanzia leo zipelekwe kwenye viwanja vingine vya Mtwara, Kigoma na maeneo ya mipakani kuhakikisha kuwa kila abiria anayetoka nje ya nchi anapimwa dalili za ugonjwa huo hatari. Pia aliagiza wanadi...