Rais wa Masharobaro, muimbaji na mtayarishaji wa muziki, Bob Junior amekanusha tetesi zilizokuwepo kuwa amerudiana na mke wake.
Akiongea na segment ya Inbox ya kipindi cha New Chapter cha Radio Free Africa, Bob Junior amesema mazoea ya kuwa na mke na kumuona mtoto wake kila siku yanamfanya awe na huzuni kubwa kuwa mbali nao. Junior amesema aliachana na mke wake na hajarudiana naye tena na hana mpango wa kuoa hivi karibuni.
Hivi karibuni kwenye Instagram Bob Junior alipost picha ya mwanae na kuandika:
Namshukuru Mungu kukupata wewe maisha yangu yote nguvu zangu zote Nitapigana hadi kufa ni kwaajili yako my son Rummy Raheem Rummy maisha yako huta jutia kupata baba kama mimi ila amini kilicho tokea……. ukija kukuua ipo siku utajua yote naishi kwenye maumivu mengi juu yako sana na hapa naandika text hii nalia sana kwa kuwa mbali nawewe sikuoni karibu my son ila jua i love u na kama mapenzi kupenda nasema nitakupenda na hata kuja yoyote kuzidi mapenzi yangu kwako mengine sisemi ila jua mwanangu nipo kwenye wakati mgumu wa kuto kuwa karibu na wewe i love u my son ( rummy ).”
KUANZISHWA KWA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA Mafanikio ya michuano ya mpira wa miguu ya Olimpiki ndiyo yalikua mwanzo wa FIFA kutamani kuwa na michuano yake ya Kombe la Dunia kwa mchezo wa mpira wa miguu. Ikumbukwe kwamba kipindi hicho mpira wa miguu wa wanaume pekee ndiyo ulikuwepo. Maswali yalitumwa kwa wahisani wa FIFA ili kuona kama wanakubaliana na uanzishwaji wa michuano hiyo na kwa masharti yapi? Kamati maalumu ilichunguza maswali hayo chini ya uongozi wa Rais wa FIFA wa kipindi hicho Jules Rimet akishirikiana na Katibu wa Shirikisho la Soka nchini Ufaransa kwa wakati ule Henri Delaunay. Rais wa FIFA Jules Rimet aliyeanzisha na kusimamia Kombe la Dunia la kwanza . Kufuatia uwepo wa muswada wa Kamati Tendaji ya FIFA, lilifanyika kongamano la FIFA Mei 28, 1928 jijini Amsterdam nchini Uholanzi likiazimia kuwepo kwa michuano ya mabingwa wa soka duniani ambayo ilipangwa na shirikisho hilo la mpira duniani na sasa nchi waandaji wa michuano hiyo zilitakiwa ...
Comments
Post a Comment