JUAN MATA ATIMIZA MIAKA 30 HII NI HISTORIA YAKE KWA UFUPI
Mata 2017/2018 |
JUAN MATA
Mata alizaliwa April 28, 1988 huko Burgos, Hispania. Leo anatimiza miaka 30. Ana urefu wa cm 70 na uzito wa kg 63. Amewahi kucheza michezo 82 akiwa na timu ya Chelsea 2011 hadi 2014 akiifungia klabu hiyo jumla ya magoli 18 katika misimu yote mitatu katika klabu hiyo kabla ya kujiunga na timu ya Manchester United Januari 24, 2014 kwa usajili wa Euro 37.1 milioni. Mpaka sasa Mata ameifungia klabu ya Man U jumla ya magoli 30. Alisaini mkataba ya kuichezea Manchester United Januari 24, 2014 na mkataba wake wa sasa utamalizika June 30, 2019.
Kabla ya Umaarufu
Mata alianza kujihusisha na soka katika klabu ya Real Madrid kuanzia mwaka 2006-2007 na baadaye alijiunga na klabu ya Valencia 2007-2011. Mwaka 2011 alijiunga na klabu ya Chelsea na mwaka 2014 alijiunga na klabu ya Manchester United.
Mata alipokua Chelsea. |
Nyongeza
Amewahi kuwepo katik kikosi cha timu ya taifa ya Hispania ambacho kilichukua kombe la dunia mwaka 2010.
Rekodi zake katika Ligi kuu ya Uingereza
Amecheza jumla ya mechi 219 akiwa na jumla ya magoli 48 na akiwa na jumla ya assist 47.
Pia, amewahi kuwa mchezaji wa mwezi katika ligi hii mezi Oktoba 2012
Nidhamu
Mpaka sasa Mata amepewa jumla ya kadi za njano 15 na kadi nyekundu 1 tu katika ligi hiyo ya Uingereza akicheza fouls 117 na na offsides 87.
Comments
Post a Comment