Skip to main content

UDAHILI WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2022/2023 UMEFUNGULIWA


BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (NACTVET)
limefungungua rasmi dirisha la uombaji wa nafasi za masomo kwa mwaka 2022/2023 ngazi ya Astashahada (Certificate) na Stashahada (Diploma), katika ujumbe huo tangazo linasomeka kama ifuatavyo:


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU WAOMBAJI WA UDAHILI WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2022/2023

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi linapenda kuufahamisha umma kuwa Udahili wa wanafunzi kwa Ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa kozi/programu zote zinazotolewa na Vyuo mbalimbali umefunguliwa rasmi kuanzia tarehe 24 Mei, 2022 hadi tarehe 30 Julai, 2022 katika awamu ya kwanza.


Wahitimu wote wa Elimu ya Sekondari na Vyuo wenye sifa za kujiunga na kozi za Astashahada na Stashahada, wanashauriwa kufanya maombi yao kwa umakini ili kupata nafasi ya kujiunga kozi/programu wanazozipenda na ambazo wanatimiza vigezo/sifa za kujiunga nazo kwa mwaka wa masomo 2022/2023. Maombi ya kujiunga na kozi/programu mbalimbali yatumwe moja kwa moja kwenye vyuo husika.
 

Aidha, waombaji wa programu za Afya na Sayansi Shirikishi kwa Vyuo vyaSerikali na Visivyo vya Serikali - Tanzania Bara, wanapaswa kuwasilisha maombi yao kupitia Udahili wa Pamoja (Central Admission System - CAS) katika tovuti ya NACTVET (www.nacte.go.tz).
 

Wanafunzi waliopangiwa nafasi za masomo katika vyuo mbalimbali vya elimu na mafunzo ya ufundi na Ofisi ya Rais-TAMISEMI wanajulishwa kuwasiliana na wakuu wa vyuo ili kuthibitisha au kupata maelezo ya namna ya kujiunga na vyuo husika. Wanafunzi ambao hawajaridhika na machaguo yao wanashauriwa kuomba moja kwa moja programu/kozi au vyuo wanavyopenda kuanzia tarehe 24 Mei, 2022.

Baraza linasisitiza kuwa wanafunzi waliopangiwa nafasi za masomo na Ofisi ya Rais-TAMISEMI wafanye mawasiliano moja kwa moja vyuoni au OR-TAMISEMI kwa maelezo zaidi. Masomo yataanza tarehe 18 Oktoba, 2022.

Baraza pia, linawashauri waombaji, wazazi na walezi kuhakikisha kuwa wanaomba kwenye Vyuo ambavyo vimeorodheshwa kwenye Kitabu cha mwongozo wa Udahili kwa Mwaka wa Masomo 2022/2023 (Admission Guidebook for 2022/2023 Academic Year). Mwongozo wa Udahili unapatikana katika tovuti ya Baraza (www.nacte.go.tz).


IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI
(NACTVET) 

TAREHE: 24/05/2022

Comments

Popular posts from this blog

BAADHI MAMBO AMBAYO HUKUYAFAHAMU KUHUSU BARA LA AFRIKA

Ramani ya Afrika. Karibu tena mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa VENANCE BLOG. Leo katika safu yetu ya Fahamu napenda kukufahamisha mambo kadhaa ambayo huenda hukuyafahamu yote kuhusu bara la Afrika. Na tuanze sasa kuyahesabu mambo hayo: 1. Karibu nchi zote za Afrika zilitaliwa na wakoloni isipokuwa nchi mbili tu: Ethiopia na Liberia. 2. Kabla ya Ukoloni, Afrika ilikuwa na tawala zilizokaribia 10,000 (Kingdoms/Empire/State) na tawala hizi zilijiongoza kila moja kivyake zikiwa na lugha tofauti na mila na desturi tofauti tofauti. 3. Lugha ya kiarabu inazungumzwa na watu takribani milioni 170 ikifuatiwa na lugha ya kiingereza inayozungumzwa na watu zaidi ya milioni 130, Kiswahili kikiwa na wazungumzaji zaidi ya milioni 100, Kifaransa takribani wazungumzaji milioni milioni 115. Pia, kuna wazungumzaji wa lugha ya Xhosa wakiwa milioni 50. Kireno kinakadiriwa kuwa na wazungumzaji milioni 20 huku Kispanyola kikiwa na wazungumzaji wanaokadiriwa kuwa milioni 10. Vilevile takriba...

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

Nicki Minaja haishiwi vituko vya kupost picha mtandaoni akiwa uchi kabsa ama nusu uchi. Tazama hiyo picha hapo juu inayoonesha matako yake yakiwa wazi. Picha nyingine hii hapa japo amevaa nguo lakini mmmh!! Kwa wanaume so conducive kabisaaa. Cheki jinsi tako lilivyobinuliwa hapa hivi eti njiani anakopita kwa mavazi haya hawapi wanaume shida!!! Haya yote yanakuja wakati Nicki anajiandaa kuachia Album yake mpya ya Pink Friday Print. Album hiyo inapatikana kwenye iTune pia. Picha hizo ziko katika akaunti yake ya Instagram @nickiminaj.  WASILIANA NAMI:  Facebook: VENANCE BLOG  Twitter: @Venancetz  Instagram: venancegilbert  Asante kwa kutembelea VENANCE BLOG © 2014

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

Lugha ya Kiswahili inazungumzwa katika nchi za Afrika Mashariki. Kiswahili hutumika nchini Tanzania, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Msumbiji na Rwanda. Zaidi ya watu milioni 1 5 katika bara hili huitumia lugha hi i kama lugha ya kwanza na wazungumzaji wengine wakiitumia kama lugha ya pili au ya tatu. Ni lugha rasmi ya M uungano wa Afrika. Hii inafanya bara hili kuwa na idadi inayozidi milioni 100 ya wazungumzaji wa lugha hii. Kiswahili ni miongoni mwa lugha kumi zinazoongoza kwa kua na idadi kubwa ya wazungumzaji barani Afrika. TANZANIA Kiswahili nchini Tanzania ni lugha rasmi na lugha ya Taifa. Ni lugha ya utambulisho kwa Mtanzanianainatumika kama lugha ya kuimarisha uelewano, ushirikiano na umoja wa kitaifa. Katika kuiendeleza, juhudi za usanifishaji zimefanyika kwa kuwatumia wataalamu wa fasihi na isimu, wadau wengine na wachapishaji vitabu. Taasisi mbalimbali zimebuniwa kuhusu lugha hii kama vile BAKITA, BAKIZA, Taasisi ya Elimu, UWAVI...

CELEBRITY WA SIKU: PAUL WALKER

Leo katika kipengele cha Celebrity wa siku tunaye Paul Walker ambaye kwa sasa ni maremu. Kwa nini Paul Walker leo? Kwa sababu leo ni tarehe ambayo alizaliwa mwaka 1973 huko California. Na tuangalie historia yake ili kumfahamu zaidi. KUZALIWA Paul Walker alizaliwa Septemba 12, 1973 huko Glendale, Calfornia nchini Marekani.  ELIMU Alipata Elimu yake katika Village Christian School. KAZI Paul Walker alikuwa muigizaji nchini Marekani ambapo alianza kazi hiyo katika televisheni mbalimbali kama vile katika vipindi vya The Young and the Restless na Touched by an Angel. Alipata umaarufu katika movie za vijana kama vile She's All That na Varsity Blues. Walker alipata umaarufu zaidi katika movie za Brian O'Conner ambapo zinahusisha uendeshaji wa magari mitaani 'The Fast and the Furious'. Alishiriki pia katika filamu kama vile Eight Below, Timeline, Into the Blue, Joy Ride na Running Scared. Mbali na uigizaji, Walker pia alikuwa mtangazaji wa kipindi cha ...

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

KUANZISHWA KWA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA Mafanikio ya michuano ya mpira wa miguu ya Olimpiki ndiyo yalikua mwanzo wa  FIFA kutamani kuwa na michuano yake ya Kombe la Dunia kwa mchezo wa mpira wa miguu. Ikumbukwe kwamba kipindi hicho mpira wa miguu wa wanaume pekee ndiyo ulikuwepo. Maswali yalitumwa kwa wahisani wa FIFA ili kuona kama wanakubaliana na uanzishwaji wa michuano hiyo na kwa masharti yapi? Kamati maalumu ilichunguza maswali hayo chini ya uongozi wa  Rais wa FIFA wa kipindi hicho Jules Rimet akishirikiana na Katibu wa Shirikisho la Soka nchini Ufaransa kwa wakati ule Henri Delaunay. Rais wa FIFA Jules Rimet aliyeanzisha na kusimamia Kombe la Dunia la kwanza . Kufuatia uwepo wa muswada wa Kamati Tendaji ya FIFA, lilifanyika kongamano la FIFA Mei 28, 1928 jijini Amsterdam nchini Uholanzi likiazimia kuwepo kwa michuano ya mabingwa wa soka duniani ambayo ilipangwa na shirikisho hilo la mpira duniani na sasa nchi waandaji wa michuano hiyo zilitakiwa ...

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

Viongozi wa nchi tajiri zaidi duniani zinazounda kundi la G7 wanatarajiwa hii leo kutoa msimamo wa pamoja dhidi ya vitisho vya kiuslama vinavyoikumba dunia vikiwemo kitisho cha makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali hadi kile Rais wa Marekani Barack Obama amelaani na kuutaja kama uchokozi wa Urusi nchini Ukraine. Kwa mara ya tatu mfululizo, viongozi hao wamemtenga Rais wa Urusi Vladimir Putin kutoka mkutano huo ulioanza hapo jana na unaokamilika hii leo katika mji wa Elmau nchini Ujerumani na badala yake wamewaalika viongozi kutoka kwingineko akiwemo waziri mkuu wa Iraq Haider al Abadi na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ambao wote wawili wanakabiliwa na kitisho kutoka makundi ya wanamgambo. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Ufaransa Francois Hollande wanatarajiwa kuangazia masuala ya mazingira katika mkutano huo hasa kuongezeka kwa viwango vya joto duniani na athari zake. Chanzo: DW

MOVIE: X-MEN APOCALYPSE RELEASED TODAY

  Release date: May 27, 2016 Director: Bryan Singer Starring: James McAvoy Jennifer Lawrence Oscar Isaac Michael Fassbender Rose Byrne Sophie Turner Synopsis: In this comic-book adventure set in the 1980s, the X-Men are forced to confront an ancient mutant called Apocalypse (Oscar Isaac). After the resurrected beast recruits a super-team to take over the world and destroy hunmanity, Professor X (James McAvoy) and his charges must come to the rescue for the fate of the planet. The film co-stars Michael Fassbender, Jennifer Lawrence and Olivia Munn.

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

Chuo cha Mipango ama Institute of Rural Development Planning kimetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali za shahada (Bachelor Degree) chuoni hapo mwa mwaka wa masomo 2016/207. BOFYA HAPA KUANGALIA MAJINA HAYO IMPORTANT NOTICES TO SELECTED STUDENTS The selected candidates must report at the Institute’s main campus Miyuji area on Monday 17 th October, 2016 ready for orientation program. Joining instructions can be downloaded from the website www.irdp.ac.tz and can also be collected from the main campus admission office. Tuition fees for Bachelor Degree courses 850,000/= Registration fee is 50,000/=, Students organization fee 20,000/= sports and games is 10,000/= and NACTE Quality Assurance Fee 20,000/=. Students are required to pay atleast half of the tuition fee and 100,000/= for registration, students organization, sports and games and NACTE Quality Assurance Fee. The payment should be made through CRDB Bank account no. 01J1082678600 before 1...

DOWNLOAD AUDIO KUTOKA UPRISE MUSIC: JVP SQUAD-HUSTLE ZA KITAA

Ngoma imefanywa Uprise Music na producer Fragger. Ngoma inaitwa Hustle za Mtaa imefanywa na JVP Squad ndani kasimama Ng'itu the Hustler na Fizzo. Sikiliza na kudownload kisha toa maoni yako hapa.  BOFYA HAPA KUSIKILIZA NA KUDOWNLOAD  

MAMBO YA MUHIMU KUFAHAMU NA KUZINGATIA KABLA YA KUCHAGUA KOZI (TAALUMA) CHUO KIKUU

Picha kwa hisani ya Debt.org 1.0 UTANGULIZI Nilipokuwa mwanafunzi wa chuo kikuu nilisikia manung'uniko miongoni mwa wanafunzi wenzangu wengi wa vyuo vikuu ambayo yalitokana na taaluma wanazosoma. Kuna sababu kadha wa kadha zinazopelekea manung'uniko hayo miongoni mwa wasomi hawa tukiachilia mbali suala la ucheleweshwaji wa mikopo miongoni mwa wasomi hawa (kwa sasa changamoto hii inapungua kadiri siku zinavyosonga). Tatizo lingine ambalo linawasumbua wasomi hawa ni suala la uchaguzi wa taaluma gani akaisome Chuo Kikuu. Uchaguzi wa taaluma (career choice) ni jambo nyeti sana na la kuzingatia kwa muhitimu yeyote wa elimu ya kuanzia kidato cha nne. Jamii yetu ya Tanzania haifahamu kwa undani kuhusu umuhimu wajambo hili lakini huku ndiko msingi hundaliwa. Mtu anapohitimu kidato cha nne na kupata ufaulu wa kujiunga na masomo ya kidato cha tano ama ngazi ya astashahada (certificate) na stashahada (diploma) hapo ndipo uchanguzi wa taaluma huanza. Kwa kuandika makala haya ninakusudia ...