Skip to main content

Posts

MABAKI YA NDEGE YA MISRI YAPATIKANA

Mamlaka ya Misri inasema mabaki ya ndege ya EgyptAir ambayo ilianguka katika bahari ya Mediteranian mwezi uliopita ikiwa imebeba abiria sitini na sita yameweza kubainika yalipo. Katika maelezo yaliyotolewa na kamati husika ya uchunguzi wa ajali hiyo wanasema ,meli inayotafuta mabaki ya ndege ya EgyptAir imeweza kubaini maeneo kadhaa ambayo mabaki ya ndege ya A320 yapo na kutoa picha ya kwanza ya masalio hayo. Kwa sasa kikosi hicho cha wakaguzi walioko melini watachora ramani wakionesha vielelezo vya mabaki ya ndege yalivyoeneo. Ndege hiyo iliyopotea baada ya kutoonekana kwenye rada wakati ikiwa inatokea Paris kuelekea Cairo. Huku ikiwa inadhaniwa kuwa lilishambuliwa na bomu.Lakini hakuna kikosi chochote cha kigaidi kilichodai kuhusika na kuangusha ndege hiyo. Chanzo: BBC

MOVIE: X-MEN APOCALYPSE RELEASED TODAY

  Release date: May 27, 2016 Director: Bryan Singer Starring: James McAvoy Jennifer Lawrence Oscar Isaac Michael Fassbender Rose Byrne Sophie Turner Synopsis: In this comic-book adventure set in the 1980s, the X-Men are forced to confront an ancient mutant called Apocalypse (Oscar Isaac). After the resurrected beast recruits a super-team to take over the world and destroy hunmanity, Professor X (James McAvoy) and his charges must come to the rescue for the fate of the planet. The film co-stars Michael Fassbender, Jennifer Lawrence and Olivia Munn.

OBAMA AZURU HIROSHIMA JAPAN

Obama amekuwa Rais wa kwanza wa Marekani aliyeko madarakani kuzuru eneo la mji wa Hiroshima ambalo Marekani ilishambulia kwa kutumia bomu la kwanza la atomiki mwaka 1945 na kuua takriban watu 140,000. Baada ya kuweka shada ya maua katika bustani ya amani eneo la Hiroshima-Japan, rais Obama alitoa hotuba ya kumbukumbu ya mashambulizi hayo ya Hiroshima huku akisisitiza matumaini kuwa uhusiano kati ya Japan na Marekani utazidisha matumaini katika juhudi za kutupilia mbali matumizi ya silaha za atomiki. Obama amekuwa rais wa kwanza wa Marekani aliyeko madarakani kuzuru eneo la mji wa Hiroshima ambalo Marekani ilishambulia kwa kutumia bomu la kwanza la atomiki mwaka 1945 na kuua takriban watu 140,000. Obama amefanya ziara hiyo ya kihistoria baada ya mkutano wa viongozi wa nchi saba tajiri kiviwanda duniani ambapo viongzo hao wamekubali kuimarisha uchumi wa dunia. Upatanisho Shambulizi la bomu la kwanza la atomiki eneo la Hiroshima mwaka 1945 na pia Nagasaki lilisaba...

FURAHIA WIKENDI KWA KUANGALIA MUVI HIZI 5 KALI MPYA

JINA LA MUVI: KILL ZONE 2 STAR: TONY JAA (kutoka Ong Bak)  After his true identity is exposed, undercover cop Kit ( Wu Jing ) is sent to a corrupt Thai prison by the gang he infiltrated, while his police unit erases all evidence that he was ever an officer. There, a guard named Chai ( Tony Jaa ) discovers that Kit is a bone-marrow match for his daughter, who desperately needs a transplant. The unlikely partners must find a way to secretly escape from the brutal prison and save Chai's daughter. Pou-Soi Cheang directed this martial-arts action thriller. JINA LA MUVI: LAST DAYS IN THE DESERT This biblical drama follows Jesus Christ (here referred to as " Yeshua " and played by Ewan McGregor ) during the 40 days he spent fasting and wandering in the desert. He is approached by a demon (also McGregor ) during his travels, who challenges him to help a troubled family living in the wilderness. Ciarán Hinds , Tye Sheridan , and Ayelet Zurer co-star as the mem...

HEZBOLLAH YATAJA SABABU YA KUUAWA KIONGOZI WAO

 Kundi la Waislamu wa madhehebu ya Kishia la Hezbollah nchini Lebanon limetaja sababu ya kifo cha kiongozi wake wa ngazi ya juu wa kijeshi, Mustafa Badreddine kuwa kimetokana na makombora ya mizinga liliofanyika karibu na uwanja wa ndege wa Damascus nchini Syria.  Hezbollah lilitangaza  kifo cha Badreddine hapo jana na alifanyiwa mazishi ya kijeshi siku hiyo hiyo katika eneo la ngome la kundi hilo huko kusini mwa Beirut. Taarifa ya kundi hilo imesema mashambulizi hayo yamefanywa na kundi linaloitwa Takfiri. Takfiri ni neno linalotumiwa na kundi hilo la Kisunni kwa kuonesha msimamo mkali, kundi lenye kujihami na silaha, lililo na itikadi kali. Badreddine alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa kundi la Hezbollah walioshutumiwa mwaka 2005 kuhusika na mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri. Chanzo: Deutsche Welle (DW)

TEGEMEA PAMBANO KUTOKA KWA MAYWEATHER NA CONOR McGREGOR

 Floyd Mayweather   Conor McGregor Mwanamasumbwi Floyd Mayweather amesema kuwa yeye ndiye aleanzisha uvumi wa kupambana na Conor McGregor ambaye anapambana kwa mtindo wa Mixed Martial Art (MMA). McGregor alipost picha kwenye mtandao wa Twitter  iliyomuonesha yeye na Mayweather wakwa uso kwa uso. Mayweather, mwanamasumbwi aliyestaafu mwenye miaka 39 amesema kuwa atahitaji kiasi cha fedha Dollar za kimarekani Milioni 100 sawa na Euro Milioni 69.3 kupambana na McGregor raia wa Ireland mwenye umri wa miaka 27. "Muwe makini kusikiliza, linaweza kuwa pambano kati ya mcheza boxing na MMA" Mayweather aliiambia fighthype.com "Ni pendekezo nililolitoa mimi, inaweza isiwe tetesi" aliongeza Mayweather. Baba yake Mayweather alisema kuwa mwanaye huyo (Mayweather) aliwahi kumwambia kuwa atapambana na mwanamasumbwi yeyote kutoka MMA ambapo McGregor aliiambia BT Sport kuwa anataka pambano la Dola Bilioni na Muamerika, Floyd Mayweather. McGregor, a...

ANGALIA VIDEO YA JENNIFER LOPEZ-AIN'T YOUR MAMA HAPA

Jennifer Lopez ameachia video ya wimbo wake Ain't your Mama May 6 ambapo mpaka sasa wimbo huo umetazawa na watazamaji zaidi ya milioni na laki saba. Kama bado hujapata nafasi ya kuangalia video hiyo tazama hapa kwa hisani ya VENANCE BLOG kisha toa maoni yako kuhusu video hiyo. Like Page yangu Facebook Nifuate Twitter Nifolo Instagram

DOWNLOAD AUDIO KUTOKA UPRISE MUSIC: JVP SQUAD-HUSTLE ZA KITAA

Ngoma imefanywa Uprise Music na producer Fragger. Ngoma inaitwa Hustle za Mtaa imefanywa na JVP Squad ndani kasimama Ng'itu the Hustler na Fizzo. Sikiliza na kudownload kisha toa maoni yako hapa.  BOFYA HAPA KUSIKILIZA NA KUDOWNLOAD  

UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA TANZANIA NA UGANDA SASA NI RASMI

BOMBA la mafuta ghafi kutoka Hoima katika Ziwa Albert nchini Uganda, sasa ni rasmi kwamba litapita katika ardhi ya Tanzania kwenda Bandari ya Tanga, ambako ndiko meli kubwa za mafuta, zitakapotia nanga kubeba mafuta hayo kwenda sehemu mbalimbali duniani. Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, imeeleza kuwa Serikali ya Uganda imetangaza rasmi uamuzi wake wa kutumia bandari hiyo. Kwa hatua hiyo, bomba hilo linalotakiwa kuwa limekamilika ifikapo 2018, litaingilia Mkoa wa Kagera kutoka nchini Uganda na kupita katika mikoa ya Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma hadi Bandari ya Tanga. Rais Museveni Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, ndiye aliyetangaza uamuzi huo wakati wa mkutano wa 13 wa Ushoroba wa Kaskazini uliomalizika jijini Kampala jana. “Ujumbe wa Tanzania uliokamilisha mazungumzo hayo na kushuhudia utangazwaji wa hatua hiyo, uliongozwa na Dk Augustine Mahiga, ...

MALAWI IMETEKETEZA TANI 2 ZA PEMBE ZA NDOVU KUTOKA TANZANIA

Malawi imeteketeza tani 2.6 ya pembe za ndovu ambazo zilinaswa na maafisa wa usalama zikitokea nchi jirani ya Tanzania. Meno hiyo 781 ya tembo ambayo inakisiwa kugharimu takriban dola milioni tatu ilipatikana baada ya operesheni dhidi ya ulanguzi na uwidaji haramu. Mkurugenzi wa idara inayosimamia mbuga za wanyama pori Bright Kumchedwa, amesema kuwa hiyo ni ishara ya kwanza na dhabiti kutoka kwa Malawi kuwa haitaruhusu tena ardhi yake kutumika kulangua bidhaa za uwindaji haramu. Hafla ya hiyo ya kihistoria ilifanyika katika eneo la Mzuzu kaskazini mwa nchi hiyo. Kenya inatarajiwa kutekeleza hatua kama hiyo mwishoni mwa mwezi huu. Kenya imekamata takriban tani 120 ya meno ya ndovu. Chanzo: BBC