Skip to main content

Posts

BIBI WA MIAKA 85 AKAMATWA KWA KUIBA HERENI

Bibi kizee mmoja mwenye umri wa miaka 85 raia wa Marekani na ambaye amekuwa akiiba vito vya thamani kwa zaidi ya miaka 60 amehukumiwa tena kwa kosa la wizi. Doris Payne, anatuhumiwa kwa wizi wa herini ya thamani ya dola 690, kutoka katika duka moja la uuzaji wa vitu vya thamani la Saks katika kiunga kimoja mjini Atlanta-Marekani. Wakili wake anatafuta namna ataachiwa huru kwa sababu ya kudorora kwa afya yake. Payne, ambaye maisha yake ya wizi yaliwekwa katika filamu mwaka 2013, amewahi kufungwa jela mara kadhaa kwa makosa mengi tu ya wizi na uhalifu. Wakuu nchini Marekani wanasema kuwa, ametumia majina 22 ya bandia tangu alipoiba almasi kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 23, na akaweza kukwepa kutiwa mbaroni. Muungano wa Walinzi wa vitu vya thamani JSA, kampuni moja kubwa ya kibiashara, ilituma tahadhari kwa maduka yote yanayouza bidhaa na mapambo ya thamani kujihadhari na mwizi huyo sugu mapema miaka ya 70. Rais wa kampuni hiyo kubwa alitaja tabia ya bi kizee huyo ...

DOGMATIC BLUSTERY WEATHER A POEM BY VENANCE GILBERT

Poem: Dogmatic Blustery Weather Poet:  Venance Gilbert Composed September 27, 2015 Published on October 21, 2015. The blustery weather blows wherever By a hair's breadth in the oceans and ponds Wind vane regularly measure the breeze. The blustery weather has now turned to policies Particularly in this phase of the GE Propelling hard to the populations; the electorates Populations frequently size them lyrics Whichever the runners’ dogmas or troop expression. It is the blustery weather since it blows to constituents The dogmatic blustery weather will measured in the poll Majority, make it take place on October Be pacific under open and just environments. ALL RIGHTS RESERVED. Venance Gilbert © 2015

DOWNLOAD WIMBO MPYA: TOFA EMCEE-KUNG FU PANDA

Anaitwa Christopher Robert jina la kazi ya sanaa 'Tofa Emcee'.  Tofa Emcee katika picha. Picha kwa hisani ya Facebook account Christoper TofaEmcee Robert Donload Kung Fu Panda kwa kubofya HAPA.

BEN POL AELEZEA ALIVYONUSURIKA KIFO KATIKA AJALI YA BOTI

Msanii wa Bongo Fleva,Ben Pol amesimulia alivyonusurika kifo baada ya boti waliokuwa wakisafiria wakitokea visiwani Mbudya,jijini Dar kuzima ghafla katika ya bahari na kukaa kwa muda wa saa nzima bila kupata msaada. Ben Pol alisema kuwa baada boti kuzima maji yalianza kuingia ndani  na engine ya boti ikazimika na boti hiyo ikaanza kuzama kilichowaokoa walikuwa wamevaa makoti ya kuogelea ‘life jackets’. ‘’Baada ya kukaa kwa saa nzima baharini kwa bahati nzuri ilipita boti ya wavuvi ikatuona ikatuokoa ila mmoja wetu hakuwepo kati ya tuliokolewa na hatujamuona ambao ni wanawake watatu, watoto hao walikuwa watatu, wanaume tulikuwa nane, lakini mmoja ndiye hatujui alipo.’alisema Ben Pol.

VAN VICKER AKUMBWA NA MAFURIKO AKIELEKEA KWAKE

Mafuriko makubwa yaliyoikumba jiji la Accra nchini Ghana usiku wa kuamkia juzi na kuleta maafa ya kuua watu 175 wakiwa wamejihifadhi kwenye kituo cha mafuta baada ya kituo hicho kulipuka moto,yamemkumba pia Staa wa filamu nchini humo Van Vicker akiwa barabarani akielekea nyumbani kwake. Kupitia akaunti yake Instagram Van Vicker aliandika kuwa ameshuhudia mafuriko kwa macho yake (live),huku taa za barabarani zikiwa haziwaki,kuna mashimo,matakataka,umeme ukiwa umekatika na barabara zilikuwa zimefurika maji, na magari yalikuwa yameharibika. Pia aliongeza kuwa waliokuwa wakitembea barabarani walikuwa wakitafuta pa kujihifadhi,madereva walipaniki na bado wakati huo mvua ilikuwa ikinyeesha na pia foleni ilikuwa kubwa na barabara ni ndogo. Ambapo alisema kuwa kawaida huwa inamchukua dakika 45 kwenda nyumbani kwake lakini siku hiyo ilimchukua masaa sita kufika nyumbani kwake. Chanzo; Udaku Specially

URUSI NA QATAR HUENDA ZISIANDAE KOMBE LA DUNIA

Mkuu wa kamati ya uhasibu wa shirikisho la soka duniani FIFA Domenico Scala amesema huenda Urusi na Qatar zikapoteza nafasi za kuyaandaa mashindano ya kombe la dunia mwaka 2018 na 2022 mtawalia iwapo ushahidi utaonyesha kulikuwa na ufisadi katika shughuli ya kinyanganyiro cha kupata kibali cha kuandaa mashindano hayo. Scala hata hivyo amesema mpaka kufikia sasa hawajapokea ushahidi wowote wa kudhihirisha kuwa nchi hizo mbili zilitoa hongo. Matamshi yake ndiyo ya kwanza kutolewa na afisa wa ngazi ya juu wa FIFA kuwa kuna uwezekano nchi hizo zikapokonywa uenyeji wa mashindano hayo. Maafisa wa idara ya mahakama wa Uswisi tayari wameanzisha uchunguzi kuhusu kutolewa kwa kandrasi hiyo ya kuandaa mashindano ya 2018 na 2022 kama sehemu ya uchunguzi wa madai ya ufisadi katika FIFA.  Chanzo: DW

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

Viongozi wa nchi tajiri zaidi duniani zinazounda kundi la G7 wanatarajiwa hii leo kutoa msimamo wa pamoja dhidi ya vitisho vya kiuslama vinavyoikumba dunia vikiwemo kitisho cha makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali hadi kile Rais wa Marekani Barack Obama amelaani na kuutaja kama uchokozi wa Urusi nchini Ukraine. Kwa mara ya tatu mfululizo, viongozi hao wamemtenga Rais wa Urusi Vladimir Putin kutoka mkutano huo ulioanza hapo jana na unaokamilika hii leo katika mji wa Elmau nchini Ujerumani na badala yake wamewaalika viongozi kutoka kwingineko akiwemo waziri mkuu wa Iraq Haider al Abadi na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ambao wote wawili wanakabiliwa na kitisho kutoka makundi ya wanamgambo. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Ufaransa Francois Hollande wanatarajiwa kuangazia masuala ya mazingira katika mkutano huo hasa kuongezeka kwa viwango vya joto duniani na athari zake. Chanzo: DW

KOMBE LA DUNIA KWA WANAWAKE

Michuano ya kombe la dunia la wanawake,inaendelea huko canada katika miji tofauti tofauti.michuano hiyo ya kombe la dunia kwa wanawake liliendelea tena hapo jana kwa michezo miwili kupigwa kati ya Norway waliopepetana na Thailand. Ujeruman ilioonesha kazi pwani ya samawati naizungumzia Ivory Coast na matokeo yalikuwa hivi Norway waliibuka na mtaji wa magoli manne huku Thailand wakikubali matokeo na kutulia na yai. Kwa upande mwingingine kwenye mechi ya pili Ujerumani walijizolea magoli yao mawili na kuwaacha Ivory Coast mikono mitupu. Chanzo: BBC

WATU 400 WAFARIKI KATIKA MTO YANGTSE

Meli iliyozama China Msemaji wa serikali nchini China anasema kuwa karibu watu 400 wanahofiwa kuaga dunia wakati feri ilipozama kwenye mto Yangtze siku ya jumatatu. Idadi hiyo imeongezeka kwa haraka baada ya makundi ya uokoaji kusaka vyumba vya feri hiyo. Kwa sasa meli hiyo imendolewa majini kwa kutumia mitambo mikubwa. Jumla ya watu 456 walikuwa ndani ya feri hiyo wakati ilipokumbwa na dhoruba ambapo ni watu 14 tu walioripotiwa kuponea ajali hiyo. Ajali hiyo inaripotiwa kuwa mbaya zaidi nchini humo tangu miaka 60 iliyopita. Chanzo: BBC

RAIS KIKWETE AELEKEZA NGUVU KATIKA ELIMU YA KIDATO CHA 5 & 6

Rais Jakaya Kikwete akipokea tuzo maalum kutoka kwa Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi, Dk.Shukuru Kawambwa kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza na kuboresha elimu nchini wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya elimu yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma jana. Picha na Ikulu Rais Jakaya Kikwete jana alitumia kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Elimu kuaga wadau wa sekta hiyo, akisema sasa nguvu zielekezwe katika kujenga majengo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu ya sekondari. Rais Kikwete, ambaye alikiri kuwapo udhaifu katika kipindi cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne, alisema mafanikio pia ni makubwa kiasi kwamba sasa hakuna wanafunzi wanaokosa nafasi ya kwenda sekondari baada ya kufaulu na hivyo nguvu sasa inatakiwa kuwekwa katika kuongeza miundombinu ya kidato cha tano na sita. Kikwete alitoa kauli hiyo jana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa alipohutubia maelfu ya wakazi wa Dodoma, wakiwamo wanafunzi wa shule za sekondari na msing...