Skip to main content

Posts

WATU 23 WANADAIWA KUUAWA NA WAASI WA UGANDA HUKO DRC

Maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanasema kuwa watu ishirini na watatu wameuawa kikatili na wanaodaiwa kuwa waasi wa Uganda. Wanane kati ya waliofariki ni wanajeshi wa DRC. Shambulizi hilo lilifanyika Jumatano usiku. Waasi wengi wao wakiwa wa Allied Democratic Forces (ADF) wamefanyana mashambulizi kadhaa kusini mwa mji wa Beni katika siku za hivi karibuni. Umoja wa mataifa unasema kuwa huenda walifanya makosa ya uhalifu wa kivita na vitendo vinavyokiuka ubinadamu . ADF imewaua mamia ya watu wakati mwingine na ndo, panga na visu. Chanzo: BBC

MVUA ZINAZOENDELEA DAR ES SALAAM KUPUNGUA MAKALI JUMAMOSI HII

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua za mfululizo zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zitaendelea kunyesha na kwamba zinatarajia kupungua mwishoni mwa wiki hii. Taarifa hiyo inaweza kuwa habari njema kwa wakazi wa Dar es Salaam na miji mingine iliyoathirika kwa kiasi kikubwa na mvua hizo zilizonyesha mfululizo na kusababisha vifo, uharibifu wa mali na miundombinu, huku hali ya usafiri, upatikanaji wa bidhaa hasa za vyakula ikiwa ngumu katika maeneo mengi. Akizungumza na gazeti hili jana, Mkuu wa  Huduma za Hali ya Hewa kwa Jamii wa TAM, Hellen Msemo alisema mvua hizi zinatarajia kupungua mwishoni mwa wiki hii; lakini sio kuisha kabisa na kwamba kwa sasa wananchi waendelee kufuatilia taarifa zinazotolewa. “Mvua hizi zitaendelea kunyesha mpaka Ijumaa ya wiki hii na tunaweza kuona jua kidogo Jumamosi lakini sio mvua za kukatika kabisa zitaendelea kunyesha kidogo kidogo,” alisema Msemo. Shule zajaa maji Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msasani ‘B’, Jan...

IN THE NEXT - A POEM BY VENANCE GILBERT

Poem: IN THE NEXT   Poet:  Venance Gilbert   Composition: December 19, 2014  First published on the blog: December 29, 2014 The system has turned to uplift us, From nothing to something mammoth, Look at them brother, look them twice more, They have our consent in authority, Having our consent to share our sufferings, For self into their bellies, Look brother, feel pitty for ourselves, The cultural similarity is credited, Now brother tell them involved, Go into details to them, In the next to put their money where their mouth are, Let them experience a miss in the next, To re-drink the milk of human kindness. All rights reserved. Venance Gilbert © 2014. IF YOU HAVE ANYTHING TO COMMENT DON'T HESITATE TO CONTACT ME THROUGH: Facebook: VENANCE BLOG Twitter: @Venancetz Instagram: venancegilbert Mobile: 0753400208 Email: venancegilbert@gmail.com. VENANCE BLOG WISHES YOU A HAPPY NEW YEAR 2015!!

KOREA KASKAZINI YAMTUSI OBAMA

Korea kaskazini imeilaumu Marekani kutokana na mataizo ya mtandao ambayo yameikumba siku chache zilizopita. Tume ya taifa ya ulinzi nchini Korea Kaskazini inasema kuwa Marekani inavuruga mifumo ya mitandao ya nchi hiyo huku ikimfananishi rais wa marekani Barack obama na tumbili wa misitu ya tropiki mbali na kumshutumu kwa kuhusika katika kuonyeshwa ka filamu yenye utata inayojulikana kama The Interview. Filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Sony ambayo ni ya ucheshi inayoonyesha kuuawa kwa kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong Un. Korea kaskazini imekana kuhusika kwenye uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony uliosababisha kampuni hiyo kusitisha maonyesho ya filamu hiyo.

KUMBUKUMBU YA MIAKA 10 TANGU JANGA LA TSUNAMI MWAKA 2004

Mataifa yaliyoathirika na janga la Tsunami yameandaa ibada za kuwakumbuka watu 220,000 waliouawa wakati mawimbi makali yalipoyapiga maeneo ya pwani ya Bahari Hindi mwongo mmoja uliopita. Mnamo Desemba 26 mwaka wa 2004, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 9.3 katika upande wa magharibi wa Indonesia lilianzisha msururu wa mawimbi makali ambayo yaliupiga mwambao wa mataifa 14 ikiwa ni pamoja na Indonesia, Thailand, Sri Lanka na Somalia. Miongoni mwa wahanga waliopoteza maisha yao ni maelfu ya watalii waliokuwa wakisherehekea siku kuu ya Krismasi katika eneo hilo, na kulipeleka janga la maafa ya asilia ambayo hayakuwa yametarajiwa hadi majumbani kote ulimwenguni. Maelfu ya watu wameimba wimbo wa taifa wa Indonesia kama mwanzo wa kumbukumbu ya janga hilo, kwenye ibada iliyoandaliwa Banda Aceh - mji mkuu wa mkoa ulio karibu na kitovu cha tetemeko la arshi ambalo lilisababisha mawimbi hayo makali. Mapema leo misikiti pia iliandaa maombi kite katika mkoa huo, wakati watu w...

BOTI YAZAMA NA WATU 36 JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO

Ripoti kutoka kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo zinasema kuwa mashua moja iliyokuwa imebeba bidhaa na abiria imezama na karibu watu 36. Maafisa wanasema kuwa zaidi ya watu 100 wamenusurika. Inaripotiwa kuwa ajali hiyo ilitokea siku ya Jumatatu umbali wa kilomita 30 kutoka mji wa kisangani na kusababisa maandamano yaliyofanywa na vijana wenye hasira kwenye mji wa Isangi ambapo mashua hiyo ilikuwa ikielekea nyumba kadha za serikali zinaripotiwa kuchomwa. Chanzo: BBC Swahili WASILIANA NAMI:  Facebook: VENANCE BLOG Twitter: @Venancetz  Instagram: venancegilbert Simu: +255712586027/753400208  Email: venancegilbert@gmail.com

VENANCE BLOG INAWATAKIA HERI YA CHRISTMAS 2014

VENANCE BLOG inapenda kuwatakia heri ya Christmas kwa mwaka huu 2014 tusherekee kwa amani na upendo huku tukimtanguliza Mungu katika kila jambo kwani yeye ndo muweza wa yote. Heri ya Krismas na pia Heri ya Mwaka mpya 2015!! WASILIANA NAMI:  Facebook: VENANCE BLOG  Twitter: @Venancetz  Instagram: venancegilbert Simu: +255712586027/+255753400208  Email: venancegilbert@gmail.com

VIDEO MPYA: BRACKETS-ALIVE FT DIAMOND & TIWA ICHEKI HAPA NA KUDOWNLOAD

Alive -“Hii ni hadithi ya kweli ya Vast Bracket, safari yake hadi alivyopona kansa mwaka 2013. Huu ni wimbo wa shukrani kwa kumfanya mshindi aliyeishinda kansa.” Hayo ni maneno yanayoonekana mwanzoni mwa video ya wimbo mpya ya kundi la Bracket kutoka Nigeria iliyotoka wiki hii, ambao wamemshirikisha Diamond Platnumz na Tiwa Savage. Kipindi Vast anaumwa kansa Memba wa kundi hilo aitwaye Vast, mwaka 2013 alikuwa akipigania uhai wake baada ya kuugua kansa ya damu ambayo baadae alifanikiwa kupona, ndio sababu ya kundi hilo kuamua kurekodi wimbo huu ‘Alive’ kwaajili ya kumshukuru Mungu kutokana na kumuwezesha msanii huyo kupona. Vast ni yule ambaye anaimba vesre ya kwanza na kwenye video anaonekana yupo hospitali. Video hii hapa Vast aliwahi kuelezea jinsi alivyougua hadi kupona katika mahojiano mbalimbali aliyofanyiwa 2013: “It all started when we went on an American tour and I started feeling feverish. I found myself taking my bath with hot...

KUREJESHWA KWA ADHABU YA KIFO AFGHANSTAN KWAWAPA WASIWASI AMNESTY

Waziri Mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif ametangaza kurejeshwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa, kwa watakaokutwa na hatia ya ugaidi ingawa Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International linapinga sheria hiyo. Pakistan imetoa uamuzi wa kurejesha sheria ya kunyonga watakaokutwa na hatia ya ugaidi. Hatua hiyo ilitangazwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Nawaz Sharif, siku moja baada ya mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa Taliban na kusababisha vifo vya watu 150, wakiwemo wanafunzi 135. Mashambulizi hayo yalitokea tarehe (16.12.2014), katika shule inayomilikiwa na jeshi ilioko mjini Peshawar. Lakini makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kurejeshwa kwa adhabu ya kifo, hakutaisaidia Pakistan kupambana na Ugaidi. Azimio hilo lilipitishwa bila ya pingamizi tarehe (17.12.2014), katika mkutano uliojumuisha vyama vyote vya siasa vya nchi hiyo. Pakistan imesema kuwa kurejesha kwa sheria ya kunyonga walio na hatia ya ugaidi ni hatua muhimu, kwani katu haiwezi kuonye...

MMAREKANI MWEUSI AWAUA ASKARI WAWILI WA MAREKANI NA BASTOLA NA KISHA KUJIUA MWENYEWE

Mtu mmoja nchini Marekani amewaua askari wawili waliokuwa kaka patrol wakiwa wamevalia nguo za kazi. Inadaiwa kuwa mtu huyo aliwalenda askari hao na kuwafatulia risasi na baadae kujiua mwenyewe.  Hii ni bastola iliyokutwa eneo la tukio. Inasemekana kuwa mwanaume huyo aliwahi kumjeruhi mpenzi wake wa zamani kwa kumfyatulia risasi iliyomsababishia majeraha. Áidha inasemekana pia kuwa kabla hajatenda tukio hilo aliandika kwenye mitandao ya kijamii ujumbe ambao si mzuri kwa polisi. Pia aliweka picha ya bastola hyo katika akaunti yake ya Instagram na kuañdika kuwa hiyo ndio itakuwa post yake ya mwisho. Aidha mtu huyo ambaye ni Mmarekani mweusi ametajwa kwa jina la Ismaail Brinsley miaka 28 na maofisa hao kuwa ni Liu Wenjin na Raphael Ramos. Mauàji hayo yametokea kufuatia kuwepo na mauaji ya watu weusi Marekani wanaouawa na maaskari weupe wa Marekani na kutochukuliwa hatua zozote na nchi hiyo.. Rais Obama wa Marekàni aliye katika jimbo la Hawaii kwa mapumziko ya sikuk...