Posts

Showing posts from September, 2023

DIRISHA LA UFADHILI WA MASOMO "SAMIA SCHOLARSHIP" 2023/2014 LIMEFUNGULIWA

Image
TANGAZO LA SAMIA SCHOLARSHIP MWAKA 2023/2024 UFADHILI KUPITIA SAMIA SCHOLARSHIP KWA WAHITIMU WENYE UFAULU WA JUU KATIKA MITIHANI YA KIDATO CHA SITA MWAKA 2023 KATIKA TAHASUSI ZA SAYANSI 1.0 UTANGULIZI Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatangaza programu ya Ufadhili iitwayo SAMIA SCHOLARSHIP kwa masomo ya shahada ya kwanza kwa wanafunzi waliopata ufaulu wa juu katika mitihani ya Kidato cha Sita mwaka 2023 iliyoendeshwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika Tahasusi za Sayansi (PCB, PCM, PGM, CBG, CBA, PMC na CBN).  SAMIA SCHOLARSHIP itagharamia kwa asilimia mia moja (100%) masomo ya Elimu ya Juu kwa wanafunzi hao ambao wamepata udahili katika fani za Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na Tiba. 2.0 SIFA ZA KUPATA UFADHILI Ufadhili huu utatolewa kwa wahitimu wa kidato cha sita wenye sifa zifuatazo: 1. Awe Mtanzania; 2. Awe na ufaulu wa juu kwenye mitihani ya taifa ya kidato cha sita mwaka 2023 iliyoendeshwa na NECTA katika tahasusi za sayansi; 3. Awe amepata ...

NExT-GPT: MFUMO WA LUGHA WA AKILI BANDIA UNAOKUPA MAJIBU KWA MAANDISHI, PICHA, SAUTI NA PICHA MJONGEO

Image
Picha hii imetengenezwa kwa Akili Bandia na Decrypt. Katika uwanda mpana wa teknolojia unaotawaliwa na makampuni makubwa kama OpenAI na Google, NExT-GPT ambao ni mfumo huria wa lugha pana ya Akili Bandia (AI) [Large Language M odel (LLM)] unaweza kuwa na kile kinachohitajika ili kushindana na miamba hii miwili katika teknolojia. ChatGPT imeusisimua ulimwengu kwa uwezo wake wa kuelewa maswali katika lugha asilia na kutoa majibu kama ya binadamu. Lakini wakati Akili Bandia inaendelea kusonga mbele kwa kasi ya umeme, watu wametaka kuwepo na maendeleo zaidi. Zama za maandishi pekee zimekwisha sasa mifumo ya lugha ya Akili Bandia imeanza kuwa mingi kuleta ushindani. NExT-GPT imetengenezwa kwa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha taifa cha Singapore (NUS) na Chuo Kikuu cha Tsinghua. Inaweza kuchakata na kutoa majibu kwa kuchanganya maandishi, picha, sauti na picha mjongeo (video). Hii inaruhusu majibizano ya asili zaidi kuliko miundo ya maandishi pekee kama ilivyo kwenye ChatGPT. T...

GOOGLE INAADHIMISHA MIAKA 25

Image
Ni miaka 25 tangu kuzaliwa kwa Google. Kwa kusema hivi namaanisha Google Inc. ambayo kwa sasa inafahamika kama Google LLC. Google ilianzishwa Septemba 4, 1998, lakini imekua ikisherekea kumbukumbu ya kuanzishwa kwake tarehe tofauti tofauti hadi Septemba 27 mwaka 2005 ilipoanza kusherekea katika siku hii. Miaka 25 ya Google imekua ya muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku hapa duniani kutokana na kuwepo makampuni mama amabyo yanashirikiana Google kuhakikisha huduma za mtandao zinakuwa sehemu ya kurahisisha maisha ya kila siku katika nyanja tofauti tofauti. Google pia imeunda Doodle maalum kwa ajili ya siku yake ya kuzaliwa. Doodle ni ile picha ambayo huwa unaiona pale juu kabisa ukiwa utafuta kitu kwa kutumia Google Search. Tazama kwenye picha hapa chini. Aida, imeonesha mabadiliko ya muda ya nembo ya kawaida ya Google ambayo mtambo wa kutafuta, mabadiliko hayo hufanywa kwa likizo, matukio mbalimbali kama kumbukizi ya siku ya uhuru wa nchi fulani mathalani T...

ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO AWAMU YA PILI 2023

Image
Wizara ya Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetangaza orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo kwa kidato cha tano katika michepuo/tahasusi mbalimbali kwa awamu ya pili. Majina hayo yanapatikana kwa kubofya 👉🏿  HAPA

MFAHAMU WOLE SOYINKA GWIJI WA FASIHI YA KIAFRIKA MWENYE TUZO YA NOBEL KATIKA FASIHI 1986

Image
Picha kwa hisani ya Oasis Magazine Bila shaka jina la Wole Soyinka sio geni masikioni mwako kwa sababu wengi wetu tumesoma tamthiliya (play) yake ya The Lion and The Jewel sekondari hasa kidato cha tatu na cha nne na The Trials of Brother Jero kwa wale waliosoma miaka ya nyuma. Hapa nitamzungumzia Wole Soyinka, mwafrika wa kwanza kushinda tuzo ya Nobel katika fasihi. Haya ni mambo ambayo huwezi kufundishwa kwenye mitaala ya shuleni, hivyo unapaswa kuyafahamu nje ya mtaala wa shule kwa muda wako mwenyewe. Awali ya yote, ni kwamba wasifu huu niliuandika kwa mara ya kwanza katika mtandao wa Twitter Julai 13, 2020 kabla sijaamua kuuleta hapa. MAISHA YA MWANZO Soyinka alizaliwa Julai 13, 1934 huko Abeokuta jirani na Ibadan nchini Naijeria. Majina yake halisi ni Akinwande Oluwole Babatunde Soyinka lakini anafahamika sana kama Wole Soyinka. Alisoma Fasihi, Ibadan. Mwaka 1954 alijiunga na Chuo Kikuu cha Leeds nchini Uingereza mara baada ya kumaliza masomo yake katika Chuo cha Serikali, Ibadan...