FAHAMU MAKALA BORA ZA KISAYANSI ZILIZOSAIDIA JAMII 2017
Karibu ndugu msomaji wa VENANCE BLOG. Leo nimekuletea makala fupi zakisayansi ambazo zilipata umaarufu kwa mwaka huu kwa ufupi sana, na tuanze sasa
Biashara ya siri kuuzwa sokwe Afrika Magharibi
![]() | |||||||
David Shukman na Sam Piranty walifanya utafiti mrefu Afrika Magharibi na BBC kugundua mipango ya siri inayohusiana na uuzwaji wa wanyamapori hasa sokwe. Hii ilisaidia kunusurika kwa sokwe aitwaye Nemley Jr ambaye alikuwa na umri wa mwaka mmoja.
Mtambo wa Kupunguza Kabonidayoksaidi angani

Katika mwaka 2017, riport zilionesha kwamba kuna mrundikano mwingi wa gesi ya kabonidayoksaidi angani mpaka kufikia wingi huo kuvunja rekodi huku juhudi za kimataifa zikishindwa kutatua changamoto hiyo ili kuepuka hatari ya kuongezeka kwa joto duniani. Je teknolojia hiyo inaweza kuondoa gesi hiyo ya kabonidayoksaidi ili kujibu maswali mengi ambayo juhudi za kimataifa zimekua zikishinwa kujibu? Hii iliandikwa na Matt McGrath.
Misheni ya Anga ya Cassini kuitafiti sayari ya Sarateni ilivyokamilika

Misheni ya anga ijulikanayo kwa jina la Cassini space missionilifikia tamati mwezi Septemba 2017, baada ya kutumia miaka13 kuchunguza sayari ya Sarateni (Saturn) pamoja na mwezi wa sayari hiyo. BBC iliweza kuonesha makala ya utafiti huo wa anga na jinsi utafiti huu wa anag unaharibu tabaka la hewa la sayari hiyo, lakini pia walihakikisha misheni hiyo walipata nafasi ya kuelezea uzoefu wao kuhusu utafiti huo wa aga. Makala hii iliandikwa na Paul Rincon.
Jinsi dunia yetu inavyofanya kazi zake kijiolojia

Je, ni mambo gani ungeyaweka katika orodha ya mambo makubwa ya kisayansi yaliyowahi kutokea katika karne ya 20? Ugunduzi mkubwa zaidi ni ule unaofahamika kisayansi kama plate tectonic. Nadharia hii ina miaka 50 sasa, ni nadharia iliyotoa majibu ambayo kwa kiasi kikubwa yanaelezea sababu za kutokea kwa volkano na matetemeko ya ardhi. Makala hii iliandikwa na Jonathan Amos.
Ugunduzi ma utengenezaji wa Mtandao (Internet) wa kizazi kijacho

Kompyuta zenye kasi zaidi zinagunduliwa na kutengenezwa mahali kote duniani. Lakini je, ni kwa nanmna gani kizazikijacho kitatumia komputa hiyo? Wanasayansi tayari wameanza kufikiria namna ya spidi ya mtandao (internet) abayo itaendana na kompyuta hizo. Makala hii iliandikwa na Mary-Ann Runson.
Trump kujenga ukuta mpakani na Mexico kunaharibu uoto wa jangwani mahala hapo pakijengwa

Rais wa Marekani Donald Trump aliahidi kujenga ukuta ambao ungetumika kama mpaka kutenganisha nchi hiyo na Mexico, lakini ahadi hii bado inakua ngumu kutekelezeka katika utawala wake huu. Wanasayansi tayari wameanza kuzungumzia madhara ya kiikolojia yatakoyotokana na ujenzi wa ukuta huo. Ujenzi huo utaathiri uoto wa jangwa. Wasayansi hao wanafanya utafiti katika jangwa la Sonoran ambalo tayari lina mpaka unaolitenganisha Marekani na Mexico.Makala hii iliandikwa na Victoria Gill.
Mapinduzi katika ugunduzi wa kupata taarifa za kigenetiki (urithi) kuwafikia watu bilioni1 nchini India

Je, jitihada inaweza kutumika nchini India kukusanya taarifa hizi za kijenetiki kutoka katika idadi yake ya watu bilioni 1 ili kuboresha huduma za afya nchini humo? Hii iliandikwa na Kat Arney.
Ndege waliokuwa wanaimba vizuri zaidi yani sauti zao zinavutia wamekuwa wakikamatwa kwenye misitu huko Indonesia na kuuzwa. Hali hii inahatarisha uwepo wa viumbe hawa. Makala hii iliandikwa na Victoria Gill.
Oktoba 15, 1987 kituo cha hali ya hewa cha nchini Uingereza kupitia BBC kilikanusha taarifa za kuwepo kwa kimbunga hatari cha Hurricane ambacho kingeikumba Uingereza. Usiku ule, nchi ilikumbwa na upepo mkali uliosababisha watu 18 kufariki. Katika kumbukumbu ya miaka 30 ya tukio hilo David Shukman aliangalia ni kwa namna gani teknolojia ingeweza kubadilisha utabiri wa hali ya hewa.
Huwezi kuamini katika fikra zako kwamba kuna viumbe hatari sana ambao bado wanaishi mpaka sasa. Dr. Ronald anasoma kwa karibu tabia za viumbe anaoishi nao hasa wale wenye sumu za hatari kwa maisha ya binadamu. Hii ni makala iliyoandikwa na Jonathan Amos.
Ndege wanaoukamwatwa na kuuzwa kwa kuwa na sauti zinavutia

Mapinduzi katika utabiri wa hali ya hewa baada ya mwaka 1987

Binadamu anayeishi na viumbe wa ajabu na hatari zaidi

Jinsi mtafiti wa mimea wa Uingereza alivyoisadia Sayansi

Katika miaka ya mwanzoni mwa karne ya 20, muwindaji maarufu nchini Uingereza aliyekuwa akiwinda kwa kupanda juu ya miti alihatarisha maisha yake kwa kuingia nchini China kuchunguza mimea iliyokuwa nchini China kwa mgongo wa Sayansi. Kumbukumbu aliyoicha baada ya utafiti huo inapatikana katika bustani zilizopo nchini Uingereza. Makala hii iliandikwa na Helen Briggs.
Utafiti mpya kuhusu ugunduzi wa kufahamu uwezekano kuweko na maisha kwingineko

Baada ya miongo miwili (miaka 20) na kushindwa kukamilisha tafiti, wanasayansi hatimaye walifanikiwa kuitafiti bahari ya Europa. Je, huu utakuwa ni utafiti ambao unaweza kujibu maswali kwamba kuna uwezekano wa kuwepo na maisha katika sehemu nyingine tofauti na duniani? Makala hii iliandikwa na Paul Rincon.
Je, nguo zetu zinachafua mazingira?

Utafiti wa kisayansi ulionesha kuwa nguo za material ya polyster na acrylic zinatoa material ya plastiki ambayo wakati wa kufua husababisha uchafuzi wa mazingira hasa bahari. Je, tunawezaje kuzuia tatizo hili la uchafuzi wa mazingira. Makala hii iliandikwa na Victoria Gill.
Utafiti mpya kuhusu ndege jamii ya Dodo kuandikwa tena

Wanasayansi wapo katika hatua za mwisho kutengeneza makala ya kibailojia ambao ilipelekea ndege hawa aina ya Dodo kutoweka duniani. Uandishi huo utakuwa ni muendelezo wa utafiti wa mtafiti wa kifaransa aliyewatafiti ndege hao alipokuwa katika safari zake bahari ya Hindi. Makala hii iliandikwa na Rolly Galloway.
Jaribu kukamata nzi yeyeote na utagundua kwamba wao huwa na haraka kuliko wewe. Haraka zaidi. Lakini je ni kwa namna gani viumbe hawa wadogo ubongo wao huweza kuhisi hatari mapema sana na kukimbia? Huu ni utafiti wa kisayansi uliofanywa na Rolly Gallway.

Mapema mwezi wa nane mwaka huu viumbe hawa walivamia hafla iliyokua imeandaliwa na August Bank nchini Uingerza kuliko hata ambavyo mawaingu yangetanda kuashiria mvua. Profesa Adam Hart mwanasayansi wa Uingerza anasema kwamba licha ya kuwa hatari sana, wadudu hawa ni muhimu sana katika ikolojia.
Kuna ugumu gani kumkata nzi?

Jaribu kukamata nzi yeyeote na utagundua kwamba wao huwa na haraka kuliko wewe. Haraka zaidi. Lakini je ni kwa namna gani viumbe hawa wadogo ubongo wao huweza kuhisi hatari mapema sana na kukimbia? Huu ni utafiti wa kisayansi uliofanywa na Rolly Gallway.
Wadudu hatari ambao pia ni muhimu katika mazingira

Mapema mwezi wa nane mwaka huu viumbe hawa walivamia hafla iliyokua imeandaliwa na August Bank nchini Uingerza kuliko hata ambavyo mawaingu yangetanda kuashiria mvua. Profesa Adam Hart mwanasayansi wa Uingerza anasema kwamba licha ya kuwa hatari sana, wadudu hawa ni muhimu sana katika ikolojia.
Nitumie maoni yako kupitia Whatsapp 0712586027 ama barua pepe venancegilbert@gmail.com. Facebook VENANCE BLOG na Twitter @Venancetz.
MAKALA HII IMEANDALIWA KWA HISANI YA SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA NCHINI UINGEREZA; BBC. PICHA KWA HISANI YA GETTY IMAGES, NASA, CLIMEWORKS, THE GEOLOGICAL SOCIETY; MCKENZIE ARCHIEVE, JULIAN HUME, ROYAL BOTANIC GARDEN; EDINBURGH AND RHS, MET OFFICE, NHM, JPL CATECH, SETI INSTITUTE NASCIENCE PHOTO LIBRARY
ZIFAHAMU GAUNI BORA 20 ZA MWAKA 2017
Uhali gani msomaji wa VENANCE BLOG? Natumai u mzima, leo nakukaribisha kuzifahamu gauni 20 bora za mwaka 2017 zilizovaliwa na nyota wa fasheni na mitindo uli mwenguni. Tuanze uchambuzi wetu.

Huyuy ni Natalie Potman. Muigizaji maarufu katika kiwanda cha filamu Marekani Hollywood. Huenda miezi tisa ya ujauzito huwa migumu sana lakini Natalie hakuchoka katika hilo. Gauni hili ni ubunifu wa Prada na alilivaa katika tuzo za Golden Globe Awrds, unaweza kuona gauni lilivo zuri na kumpendeza mjamzito na mimba yake hapo juu. Unapenda fasheni na mitindo? Basi hili litamfaa zaidi mjamzito.
Mwingine huyu. Anaitwa Brie Leson muigizaji mwingine kutoka kiwanda cha filamu Marekani. Brie alivaa gauni hili katika katika tuzo za 89 za Academy Awards. Ni ubunifu wa mwanamitindo Oscar de la Renta. Unaionaje gauni hiyo? Bila shaka kimpasuo hiko kidogo kinapendeza sana pamoja na mchanuo ule wa nyuma kama maua. Haya kazi kwako kupendeza na mtindo huu kwenye red carpet.
Huwezi kushindwa kumtambua mdada huyu mpenda fasheni na mitindo. Anafahamika kama Rihanna. Mtindo huu unafahamika kwa jina la Kawakubo. Nadhani unaona jinsi ulivyompendeza Rihanna pamoja na kiatu chake. Je, unaweza kuuvaa mtindo huu? Haya jibu liwe siri yako.
Mwanamitindo wa Uingereza Bella Hadid pia yupo katika orodha yetu. Mwanamitindo huyu alitimiza miaka 21 mwaka huu. Gauni hii imebuniwa na Ralph & Russo. Imekaaje hii gauni kwa upabde wako? Unaweza kuvaa? Bila shaka jibu lako ni ndio na mazingira yake pia unayafahamu.
Anaitwa Gigi Hadid. Huyu ni ndugu na mwanamitindo wetu hapo juu, Bella Hadid. Ana miaka 22. Ni ubunifu wa Mary-Kate na Asley Olsen. Haya kazi kwako mpenda fashion.
Anafahamika kama Isabelle Huppert. Kama unavyoona hapo katika red carpet, mdada huyu alipendeza katika gauni lake alipokuwa akifanya promo ya tangazo la Elle. Chukua nyingine hiyo.
Huyu ni Natalie Dyer. Unaambiwa vazi hili linafaa kwa mtoko na mpenzi wako. Ni vazi la mchanganyiko wa rangi za pinki na nyekundu. Unapotoka na mpenzi wako kwa mara ya kwanza kabisa baada ya makuba baada ya kukaa muda mrefu bila kutoka, gauni hili litakupendeza sana.
Wanafahamika kama The Dutches of Cambridge. Gauni hili ni ubunifu kutoka McQueen na lilivaliwa katika tuzo za Bafta. Nadhani unaona hapo rangi nyeusi inavyopendeza. Kiujumla couple hii ilipendeza sana.
Anaitwa Penelope Cruz. Huu ni ubunifu wa kampuni maarufu ya nguo duniani Versace. Penelope alipendeza katika red carpet ya British Academy Film Awards.
Unapenda gauni za kubana juu bila kuwa na mikanda ya kukushikilia kwenye mabega? Hii inakufaa sana. Rangi ya pinki nzuri sana kwa wadada. Anaitwa Lily-Rose Depp. Hkika gauni hii inapendeza sana sio siri. Ubunifu huu unaitea The Channel.
Muigizaji Kristin Scott Thomas pia alipendeza na ggauni hili. ilikuwa ni katika kusherehekea miaka 70 ya Cannee. Make up aliyofanyiwa siku hii pamoja na gauni lake vilimfanya apendeza sana.
Sienna Miller pia amehusika katika orodha yetu kwa gauni lake hili la ubunifu wa Gucci. Hii ilikuwa mapema sana mwezi Januari katika uzinduzi wa gauni la Alessandro Michelle. Gauni lake hilo lenye muundo wa mawimbi fulani na lipsi nyekundu vilimfanya apendeze sana.
Claire Foy pia anahusika katika orodha yetu. Gauni hili lenye mkia nyuma pamoja na utepe hapo kiunoni ilimfanya apendeze sana. Claire amekuwa moja ya waigizaji na wanamitindo aliypamba katika ukurasa wa mbele wa jarida maarufu la mitindo nchini Uingereza la Vogue. Ubunifu huu ni maarufu kama Erdem. Hii ilikuwa ni katika jukwaa maarufu la maonesho la The Crown.
Hakika red carpet inapendeza sana. Unamuoana Elle Fanning alivyopendeza? Ni katika anniversary ya Cannes. Gauni hili limetengenezwa kwa vito pamoja na material za almasi. Nadhani unafahamu kwamba madini ya almasi hung'aa sana.
Bila shaka unaona rangi hii sio ya kizungu zaidi. Anaitwa Ruth Negga ni muigizaji anaykuja vizuri katika tasnia ya filamu nchini Uingereza bila shaka na duniani kote. Muigizaji huyu ni raia wa Uingerza mwenye asili ya Ethiopia na Ireland. Bai gauni lake hili ni ubunifu wa Louis Vuitton. Hii ilikuwa ni katika tuzo za Golden Globe Awards.
Anaitwa Emma Stone. Ubunidu guu unajulikana kama Givenchy Haute Couture ambao ni hatimiliki ya mbunifu Riccardo Tisci. Ubunifu huu ulimfanya Emma awe na muonekano mzuri.
Unamuona Marion Cotillard, yupo katika ubunifu wa Halpern. Mwaka 2017 ni mwaka ambao Halpern amehitimu kutoka Central Saint Martins ambako alikuwa akisomea mabo ya mitindo hasa hasa ubunifu wa kumpendezesha mtu kwenye red carpet. Gauni hili hili limewapa sifa mbunifu pamoja Marion kiasi cha kufanya mbunifu Halpern kuchukua tuzo yake ya kwanza katika masuala ya fashion.
Anaitwa Cara Delevingne. Huu ni ubunifu wa Iris van Heprn.Bila shaka unafahamu kwamba unapotakiwa kufanya tangazo la kitu chochote lazima uonekane vizuri. Hapa Cara alikuwa katika tangazo la Valerian.
Emma Watson alihitajika katika kutengeneza muvi ya Disney ambayo ina maudhui ya karne ya 21. Ili kupata vazi linaloendana na maudhui ya muvi iliwapa Emma na team yake kuandaa documentary ya The Press kwa ajili ya upatikanaji wa nguo hii ambapo alishinda mwanamitindo Emilia Wickstead kwa ubunifu huo unaouona hapo pichani.
Tumalize na Keira Knightley. Hii ni kutoka katika collection maarufu ya mavazi ijulikanayo kama Spring/Summer 2018 Colletion. Keira pia aliamua kupanda kwenye red carpet kwa gauni hili mapema mwezi hu. Gauni hili ni maarufu kwa jina la Valentino.
Kama una maoni kuhusu makala hii na mengineyo, nitumie kwa WhatsApp namba 0712586027, ama barua pepe venancegilbert@gmail.com, pia Facebook VENANCE BLOG pamoja na Twitter @Venancetz. Usisite kutembelea VENANCE BLOG wakati wowote.
MAKALA HII IMEANDALIWA KWA HISANI YA JARIDA MAARUFU LA MITINDO NCHINI UINGEREZA LA THE VOGUE NA KULETWA KWAKO NA VENANCE GILBERT. PICHA ZOTE NI KWA HISANI YA GETTY IMAGES.
TETESI ZA UHAMISHO ULAYA: NANI WANATARAJIWA KUHAMIA KLABU MPYA JANUARI?
Ni wakati mwengine wa mwaka ambapo
uvumi utaanza kusambaa. Uhamisho wa mwaka uliopita haukuwa na changamoto
nyingi kutoka kwa timu sita bora katika ligi ya Uingereza huku timu
zote za ligi hiyo zikitumia £215m mwezi Januari.
Wakati huu itakuwaje, Je timu kubwa zitagharamika kununua wachezaji?
Barani Ulaya...
Dirisha
la uhamisho katika ligi tano kuu litafungwa kwa wakati mmoja. Dirisha
la uhamisho la klabu za Uingereza, Ufaransa , Ujerumani , Italia na
Uhispania litafungwa Desemba 31 mwaka huu
DIEGO LOPEZ (klabu: Espanyol; Safu: kipa; Umri: 36)

Anahusishwa na uhamisho wa :Crystal Palace.
Ni
kipa anayejulikana kwa kupigania nafasi ya kipa na Iker Casillas katika
klabu ya Real Madrid, alikuwa katika benchi wakati Reala Madrid
iliposhinda kombe la vilabu bingwa 2014 na amekuwa mchezaji wa Ziada wa
Espanyol kwa kipindi kirefu cha msimu. Pia aliichezea Villarreal,
Sevilla na AC Milan.
KEVIN TRAPP (Paris St-Germain; kipa; 27)

Anahusishwa na uhamisho wa : Crystal Palace, Borussia Dortmund, Liverpool.
Mkufunzi
wa PSG boss Unai Emery ana mpendelea sana kipa Alphonse Areola, na
kipa raia wa Ujerumani Trapp ameanza kukerwa kutokana na ukosefu wa
fursa ya kuiwakiulisha timu yake hususan wakati huu ambapo wachezaji
wanajianda kuziwakilisha timu zao za kimataifa katika kombe la dunia
DANIEL OPARE (Augsburg; Beki; 27)

Anahusishwa na uhamisho wa : West Ham, Stoke City, Everton, Swansea.
Mchezaji
huyo wa kimataifa wa Ghana ana uwezo wa kucheza kama beki wa kulia ama
kushoto na anasakwa na baadhi ya vilabu vya Uingereza.Amekamilisha
kandarasi yake na Augsburg na huenda klabu hiyo ya UJerumani inataka
kumuuza.
LEON GORETZKA (Schalke; kiungo wa kati ; 22)

Anahusishwa na uhamisho wa: Manchester United, Arsenal, Barcelona.
Alikuwa
katika kikosi cha Ujerumani kilichoshinda kombe la shirikisho ,Goretzka
anafananishwa na kiungo wa kati wa zamani wa Manchester United Paul
Scholes. Anakamilisha kandarasi yake mna yuko tayari kuondoka ili kupata
changamoto mpya.
STEVEN NZONZI (Sevilla; kiungo wa kati; 29)

Anahusishwa na uhamisho wa: Everton, Arsenal.
Mchezaji
huyo wa zamani wa Stoke na Blackburnalihusishwa na uhamisho wa kurudi
katika ligi ya Uingereza baada ya kudaiwa kuzozana na mkufunzi wa zamani
wa Sevilla Eduardo Berizzo, ambaye alifutwa kazi mnamo tarehe 22
Disemba. Uzoefu wake wa soka ya Uingereza kunaweza kumfanya kuwa kiungo
muhimu.
ARDA TURAN (Barcelona; kiungo wa kati ; 30)

Anahusishwa na uhamisho wa : Arsenal, Trabzonspor.
Mchezaji
huyo wa Uturuki hajaichezea Barcelona tangu mkufunzi Ernesto Valverde
kuchukua usimamizi wa klabu hiyo. Ametngaza wazi kwamba anataka kuondoka
Nou Camp mnamo mwezi Januari.
JEAN MICHAEL SERI (Nice; kiungo wa kati ; 26)

Anahusishwa na uhamisho wa : Barcelona, Manchester City, Liverpool.
Mchezaji
huyo wa Ivory Coast alikuwa akiwindwa na Barcelona katika dirisha la
uhamisho lililopita, lakini Nice ilikataa ombi la viongozi hao wa La
Liga . Nice imaimarika baada ya kupata matyokeo mabaya , na huku uwezo
wa klabu hiyo wa kufuzu kushiriki katika kombe la vilabu bingwa ukiwa
mchache , Seri anaweza kutaka kuondoka mwezi Januari.
JAVIER PASTORE (Paris St-Germain; kiungo wa kati mshambuliaji ; 28)

Anahusishwa na uhamisho wa klabu za: Liverpool, Sevilla, Inter Milan.
Mchezaji
mwenye kipaji ambaye hajathibitishiwa kuwa ataorodheshwa katika kikosi
cha kwanza cha PSG , Pastore alitajwa kuwa mchezaji bora duniani na
Eric Cantona, ambaye anasema angependelea iwapo Patore angesajiliwa na
man United .Mchezaji huyo wa Argentina anapigiwa upato kuwa mchezaji
muhimu katika kombe la dunia.
GELSON MARTINS (Sporting Lisbon; Winga; 22)

Anahusishwa na uhamisho wa : Liverpool.
Sporting Lisbon inahitaji kitita kikubwa , na Martins anasemekana
kuwa dau la kuondoka lakini mchezo wake katika ligi ya Ureno umevutia
maoni yasio ya kawaida.
THOMAS LEMAR (Monaco; Winga/kiungo wa kati mshambuliaji; 22)

Anahusishwa na uhamisho wa : Arsenal, Chelsea, Liverpool.
NI
miongoni mwa nyota wa klabu ya Monaco ilioshinda ligi msimu uliopita ,
na sasa ameorodheshwa katika kikosi cha Ufaransa ambapo amefunga mabao
mawili dhidi ya Uholansi katika mechi ya kirafiki mnamo mwezi Novemba.
Arsenal na Liverpool zilijaribu kumsajili katika dirisha la uhamisho lililopita.
HATEM BEN ARFA (Paris St-Germain; Winga/mshambuliaji /kiungo wa kati ; 30)

Anahusishwa na uhamisho wa : Leicester City.
Baada
ya msimu mzuri na Nice msimu uliopita 2015-2016, uhamisho wake hadi
PSG haikuingiliana. Soka yake imekwama chini ya usimamizi wa Emery,
ambaye haonekani kutakab kumpatia fursa ya kucheza katika kikosi cha
kwanza. Meneja wa Ben Arfa's katika klabu ya Nice alikuwa Claude Puel,
na huenda kuna uvumi kwamba huenda wakakutana tena katika klabu ya
Leicester.
MAKALA HII NI KWA HISANI YA BBC.
UNICEF: WATOTO WALISHAMBULIWA KWA KIWANGO KIKUBWA SANA MWAKA 2017
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF, limesema
mwaka 2017 ulikuwa miongoni mwa miaka mibaya zaidi kwa watoto wanaoishi katika
maeneo ya vita na mizozo duniani.
Ripoti ya shirika hilo la UNICEF imesema pande zinazozozana katika vita
duniani zilikiuka wazi wazi sheria za kimataifa linapokuja suala la
kuwalinda watozo. Mkurugenzi wa UNICEF kuhusu mipango ya dharura Manuel
Fontaine amesema watoto walilengwa na kuwekwa katika hatari ya
mashambulizi wakiwa nyumbani, shuleni na wakicheza.
Fontaine
ameongeza kusema ulimwengu haupaswi kuyafumbia macho mashambulizi haya
akisisitiza maovu dhidi ya watoto hayapaswi kuwa matukio ya kawaida
katika ulimwengu wa sasa.
Maovu dhidi ya Watoto ni makubwa
Watoto
katika mataifa yanayoshuhudia vita wamekuwa waathirika wakubwa
wakiuawa, kulemazwa, kusajiliwa kwa lazima kuwa wapiganaji, kuolewa kwa
lazima, kutekwa nyara, kutumikishwa na kubakwa.
Wapiganaji watoto wa Sudan Kusini. |
Wengi wa watoto hao wanaathirika katika mataifa ya Syria, Yemen,
Nigeria, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Myanmar.
Mamilioni ya watoto wengine wanakumbwa na utapia mlo, magonjwa, msongo
wa mawazo na kukosa mahitaji ya kimsingi kama chakula, maji, na huduma
za afya.
Ripoti hiyo ya shirika la Umoja wa Mataifa la
kuwashughulikia watoto limetoa takwimu kuhusu jimbo la Kasai katika
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambako ghasia zimesababisha takriban
watoto 850,000 kuyahama makazi yao na wengine 350,000 kukumbwa na utapia
mlo mbaya. Shule 400 nchini Congo zilishambuliwa kimakusudi.
Nchini
Nigeria na Cameroon, waasi wa kundi la Boko Haram waliwatumia kiasi ya
watoto 135 kama washambuliaji wa kujitoa muhanga kwa mabomu, hiyo ikiwa
mara tano ya idadi ya watoto waliotumika na waasi hao mwaka jana.
Wengi wanakumbwa na utapia mlo
Sudan Kusini, zaidi ya watoto 19,000 wamesajiliwa kwa lazima kuwa wapiganaji kuanzia mapigano yalipozuka nchini humo mwaka 2013.
Nchini Yemen, vita vilivyozuka mwezi Machi mwaka 2015 vimesababisha
watozo 5,000 kupoteza maisha yao au kujeruhiwa, huku idadi kamili
ikihofiwa kuwa hata juu ya hiyo. Uhaba mkubwa wa chakula nchini humo
umesababisha takriban watoto milioni mbili kukumbwa na utapia mlo mbaya.
Mtoto anayesumbuliwa na utapiamlo nchini Yemen. |
Nchini
Iraq na Syria, takribani watoto 700 wameuawa mwaka huu na UNICEF
imeripoti kuwa katika baadhi ya visa watoto nchini humo walitumika kama
ngao vitani. Zaidi ya watoto milioni 11 wanahitaji kwa dharura misaada
ya kibinadamu.
Ripoti hiyo ya UNICEF inalenga kuufanya ulimwengu
kuangazia masaibu wanayopitia watoto walioko katika maeneo ya mizozo
duniani na Jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua kuwalinda watoto.
MAKALA HII IMELETWA KWAKO KWA HISANI YA DW.