TANGAZO LA AJIRA 289 ZA WATUMISHI KADA ZA AFYA KUTOKA WIZARA YA AFYA
Wizara ya Afya kupitia Kibali cha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb. Na. FA.97/128/01/” B”/75 cha tarehe 04 Mei, 2023 na Kumb. Na FA.97/128/01”B”/78 cha tarehe 09 Agosti, 2023; Inatangaza nafasi za kazi 289 za Kada za Afya. Muda wa kutuma maombi haya ni ndani ya wiki mbili tangu tarehe ya kutoka kwa Tangazo hili. Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa ajira wa Wizara unaopatika kupitia tovuti ajira.moh.go.tz . Waombaji wote mnakumbushwa kuwa makini mnapowasilisha maombi kuhakikisha umejaza vizuri vipengele vyote vinavyotakiwa kwenye mfumo ikiwa ni pamoja na kuambatisha nyaraka zote zinazohitajika. Unaweza kutazama tangazo hilo kwa kubofya HAPA ama kwa kulidownload moja kwa moja kwa kubofya HAPA ama kwa kusoma hapa chini nafasi zilizotangazwa: 1. Daktari wa Meno Daraja la II – TGHS E (NAFASI 3) SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya Udaktari/Udaktari wa Meno ku...