MECHI YA ATLETICO & REAL MADRID KULINDWA NA POLISI 2,000
Polisi wa kukabiliana na fujo walikabiliana na mashabiki wa Bayern Munich mnamo 18 Aprili Walinzi zaidi ya 2,000 watatumiwa kudumisha usalama na kudhibiti mashabiki wakati wa mechi ya nusufainali ya mkondo wa kwanza kati ya Real Madrid na Atletico Madrid katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Mechi hiyo itakayochezewa Santiago Bernabeu siku ya Jumanne imeorodheshwa kama yenye "hatari kubwa" na usalama "utaimarishwa", maafisa wasimamizi wa jiji la Madrid walisema Ijumaa. UEFA wameamrisha usalama katika mechi za klabu Ulaya uimarishwe baada ya shambulio kwenye basi la timu ya Borussia Dortmund mnamo 11 Aprili. Atletico watakuwa na mashabiki 4,000 katika uwanja huo wa Real unaotoshea mashabiki 80,000. Kawaida ni mashabiki wachache sana husafiri kuhudhuria mechi za ugenini Uhispania. Idadi ya walinzi tarehe 2 Mei itakuwa ya juu zaidi ya waliokuwepo wakati wa mechi iliyopita ya Real Ulaya dhidi ya Bayern Munich polisi wa kuk...