FAHAMU MAMBO HAYA 20 KUHUSU TANZANIA
Leo nakufahamisha baadhi ya mambo ambayo huenda hukuyafahamu ama ulichukulia kawaida tu. Mambo hayo ni hapahapa Tanzania. Tanzania ina eneo la kilomita za mraba 945,087. Ina jumla mikoa 31 kote bara na visiwani. Mpaka kufikia mwaka 2017 idadi ya watu nchini ilikadiriwa kuwa milioni 52.554 kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya takwimu. Twende sasa tuanze kuhesabu moja baada ya jingine #1 . Wimbo wa taifa "Mungu Ibariki Tanzania" ni wimbo unaofanana na nyimbo za mataifa ya Afrika Kusini na Zambia. Wimbo huu ulitungwa na Enock Sontonga kwa lugha ya Xhosa "Nkosi Sikelel iAfrika" . Wimbo huu pia uliwahi kutumiwa na nchi za Zimbabwe na Namibia. Enock Sontonga mtunzi wa wimbo Mungu Ibariki Afrika #2. Ni Tanzania pakee ambako kunapatikana Simba wenye uwezo wa kupanda juu ya miti. Simba hawa wanapatikana katika hifadhi ya taifa ya Ziwa Manyara. Simba wenye uwezo wa kupanda miti hifadhi ya Ziwa Manyara. #3. Tanzania ni nchi ambako fuvu la mtu wa kale z...