Posts

Showing posts from September, 2017

MSHAMBULIAJI WA MANCITY SERGIO AGUERO AJERUHIWA KATIKA AJALI

Image
Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero amejeruhiwa katika ajali ya barabarani mjini Amsterdam, saa chache baada ya kuhudhuria tamasha. Raia huyo wa Argentina, mweny e umri wa miaka 29, anaarifiwa kuwa ndani ya taxi akielekea katika uwanja wa ndege baada ya kuhudhuria tamasha la muimbaji Maluma. City imesema "alikuwa Uholanzi katika siku yake ya mapumziko na amepata majeraha". Image caption Sergio Aguero Aguero anatarajiwa kurudi Manchester Ijumaa na atakaguliwa na kikosi cha madaktari wa City kabla ya kuelekea kwa mchuano wa Premier League watakapokaribishwa na Chelsea Jumamosi. Polisi Amsterdam wameithibitishia BBC kwamba watu wawili walikuwa ndaniya taxi iliyohusika katika ajali katika eneo la De Boelelaan mjini humo. Chanzo: BBC

MTANDAO WA TWITTER KUONGEZA MANENO HADI 280

Image
Mtandao wa Twitter kwa sasa upo katika majaribio ya kuongeza maandishi yake kutoka 140 hadi 280 hii ikiwa ni mara mbili ya hayo ya awali. Sababu za kuongeza idadi hiyo ya maneno ni kwamba kuna wakati mtu unaweza kuwa na hoja fulani inayozidi ukomo wa maneno lakini ukashindwa kuiandika ama ukapunguza idadi ya maneno ambayo wakati mwingine huwa ni ya muhimu sana katika tweet husika. Huu ni mfano wa vile tweet ya sasa ilivyo na vile ambavyo ongezeko litakuwa kwa maneno 280. Afisa Masoko Aliza Rosen wa Twitter na Mhandisi wa Twitter Japan  Ikuhiro Ihara wamesema kuwa katika mchakato wa kuruhusu jambo hili watu wachache watachaguliwa kwa majaribio na pia watakuwa wakikusanya maoni na kupata mrejesho kutoka kwa watumiaji wa Twitter kabla hawajafikia uamuzi wa kuruhusu ongezeko hilo la maneno. Jinsi tweet za Kiingereza na Kispanyola zinavyokuwa ukilinganisha na Kijapan. Zipo lugha ambazo hazitahusika kabisa katika jaribio ambazo ni Kichina, Kijapan na Kikorea sababu ni kwamba...

IRAN IMEFANYA JARIBIO LA KOMBORA LA NYUKLIA

Image
Iran inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la Khorram-shahr. Kombora hilo lilionyeshwa hadharani katika maonyesha ya kijeshi jana Ijumaa. Iran imesema kuwa kombora hilo linaweza kusafiri mwendo wa kilomita 2,000. Kituo cha runinga cha taifa hilo kilionyesha picha za sherehe hizo. Kombora la kwanza la Khorram-Shahr lilirushwa angani Januari lakini likalipuka katikati ya mwendo. Jaribio hilo lilifanywa siku chache baada ya Rais Trump wa Marekani kushambulia Iran katika hotuba yake katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Rais wa Iran, Hassan Rouhani, ametetea hatua ya taifa lake kuimarisha zana zake kwa lengo la kujitetea. Chanzo

AUDIO | HUNTER & D FLEVA FEAT BARNABA-FURSA | DOWNLOAD

Image
Ngoma mpya kutoka kwa Hunter & D Fleva wakimpa shavu Baarnaba Boy Classic. Ngoma imefanyika Combination sound ukiwa ni mono wa fundi Man Water. VENANCE BLOG inakupa nafasi ya kudownload na kusikiliza. DOWNLOAD

KAMPUNI YA ACACIA KUPUNGUZA SHUGHULI NA WAFANYAKAZI NCHINI

Image
Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia imesema itapunguza wafanyakazi na shughuli zake za migodini ikiwa ni sehemu ya athari ya uzuiaji wa usafirishwaji wa makinikia uliowekwa na serikali ya Tanzania mwezi Machi mwaka huu. Kampuni hiyo inasema wakati baadhi ya shughuli ndani ya mashimo yake ya dhahabu zitasimama, ndani ya wiki nne, uchenjuaji wa makininia pia nao utasimama. "Kwa masikitiko, mpango huu utapelekea kupunguzwa kwa ajira kati ya wafanyakazi 1,200 waliopo hivi sasa na wanakandarasi 800" kampuni hiyo imesema kwenye taarifa. Hata hivyo Acacia hawajasema ni wafanyakazi wangapi hasa watakaopunguzwa kazini. Kampuni hiyo ambayo imeorodheshwa katika soko la hisa la London nchini Uingereza inasema kusimamishwa kwa usafirishwaji wa makinikia kumekuwa kukiikosesha takribani $15 milioni (Dola milioni kumi na tano) kwa mwezi. Acacia wanasema hali hiyo imesababisha uendeshaji wa siku hadi siku wa moja ya migodi yake mikubwa Bulyanhulu kuathiriwa kwa kiasi kikubwa. ...