TATHIMINI KWA UFUPI CHELSEA vs EVERTON KABLA YA MECHI SAA 2:30 EAT

Timu hizi mbili zimekutana katika michezo 49 ambapo Chelsea imeshinda mechi 22 na Everton imeshinda mechi 10 na kudroo mechi 17. Chelsea imeshinda nyumbani mechi 13 wakati Everton imeshinda mechi 9. Nje, Chelsea imeshinda mechi 9 wakati Everton imeshinda 2.

Katika mechi 3 zilizopita Chelsea ilifungwa na Everton magoli 2 kwa nunge, hii ilikuwa mechi ya Machi 12, 2016. Lakini pia mechi ya Januari 16, 2016 timu hizi zilitoka sare ya magoli 3. Na ile ya Septemba 12, 2015 Chelsea alipigwa magoli 3 kwa 1.

Katika msomu huu Chelsea ipo katika nafasi ya 4 wakati Everton ipo nafasi ya 6 kwenye msimamo wa Ligi. Chelsea imeshinda 70% ya mechi ilizocheza huku Everton ikishinda 50%. Mechi za nyumbani Chelsea ina asilimia 80% dhidi ya mpinzani wake Everton 50% huku mechi zilizopigwa nje Chelsea ana 60% na Everton 40%. Chelsea ina wastani wa 2.1 katika magoli iloshinda wakati Everton ana wastani wa 1.5 Lakini pia Chelsea imefungwa wastani wa 0.9 wakati Everton ina 0.8.

TAHLISO YATOA WIKI MOJA KWA SERIKALI KUTOA MIKOPO

Shirikisho la serikali za wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Tanzania (TAHLISO) limetoa muda wa wiki moja kwa wanafunzi waliokosa mikopo licha ya kuwa na vigezo vyote ikiwemo uhitaji kusikilizwa na serikali kabla hatua nyingine hazijachukuliwa.


Tamko hilo limetolewa leo na Mwenyekiti wa shirikisho hilo Bwana Stanslaus Peter, katika kikao cha pamoja kilichohusisha marais wa vyuo vyote nchini, waliokutana Jijini Dar es Salaam leo, kujadili sintofahamu inayowakumba wanafunzi wanaojiunga mwaka wa kwanza katika vyuo mbalimbali nchini.


Stanslaus amesema kuwa kuna kundi kubwa la wanafunzi ambao wameondolewa kwenye orodha ya wanufaika, na wengine kunyimwa kabisa ama kwa visingizio au bila sababu, jambo linalowafanya waishi katika mazingira magumu na kuhatarisha hatma yao kimasomo.


Amesema wamekubalina kuwa, endapo serikali haitafanyia kazi ombi hilo ndani ya wiki moja, basi shirikisho hilo litachukua hatua ikiwa ni pamojana kuhamasisha wanafunzi wa mwaka wa pili na wa tatu kuungana na wale wa mwaka kwanza katika kudai haki hiyo.


Chanzo: EATV

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

Google Inc. kupitia teknolojia yao ya Android wanakuja na Version nyingine 7.0 na 7.1 Android Nougat.


Katika historia ya version za Android zilizowahi kuwagunduliwa version ya Kwanza ilikuwa Android Alpha 1.0 ya mwaka 2007. Hapo katikati zikaletwa Zombie Arts, Jeally Bean, KitKat, Lollipop na Mashallow. Sasa ni zamu ya Android Nougat.


TUANGALIE SIFA ZA ANDROID NOUGAT 7

Android Nougat ipo kwa ajili hako. Ina njia nyingi za kufanya uhisi teknolojia hii ni ya kwako. Kwa mujiu wa Android, Nougat ni toleo zuri kuwahi kutolewa katika teknolojia hii.

1. Ni Mfumo wa Uendeshaji (Operating System, OS) unaotumia lugha yako. Inayasogeza karibu maneno ya lugha yako ikiwa na emoj mpya na uwezo wa kutumia lugha 2 kwa wakati mmoja. Ina zaidi ya emoj 1500 ikijumuisha emoj mpya 72.



2. Inakuruhusu kufanya mambo 2 kwa wakati mmoja. Sasa unaweza kutumia vitumizi viwili (applications) kwa kugusa mara mbili (double trap) na kutumia vitumizi viwili pande mbili. Kwa mfano, unaweza kuangalia muvi na kutuma ujumbe.



3. Jionee Android yako katika ubora mpya. Version hii inakuja na Graphics za Vulkan™ API ambayo ina muonekano bora zaidi katika michezo ya simu (games). Inatumia Three Dimension (3D). Graphics hizi zina sifa ya eye-candy effects.



4. Furahia vitumizi vyako (applications) pendwa katika hali inayokaribia uhalisia. Hii itakupeleka katika ulimwengu mpya.


5. Endelea kufurahia ama kutumia simu yako yenye betri imara. Version hii inakuja na feature mpya inayoitwa Doze (hii ni sawa na Battery Saver). Hii itakusaidia kutunza chaji wakati simu yako ikiendelea kutumika ama inapokuwa mfukoni mwako.



6. Inakufanya uende na wakati. Android Nougat inakurahisishia kukufanya uende na wakati ikiwa na mipangilio iliyoboreshwa zaidi na taarifa. Unaweza kupangilia mipangilio yako ya taarifa za haraka ili kupata unachokipenda kwa haraka. Pia sasa unaweza kujibu taarifa moja kwa moja bila kufungua kitumizi chochote. Inakusanya taarifa nyingi kwa wakati mmoja kutoka katika vitumizi vyako vyote hivyo unaweza kugusa na kupanua wigo wa kuangalia taarifa bila kufungua kitumizi (application).



7. Ina njia nyigi za kufanya uhisi Android ni ya kwako. Inakufungulia njia nyingi za kuipangilia simu yako. Pangilia ni kwa jinsi gani data zako zitatumika, jinsi unavyotaarifiwa na jinsi muonekano wa simu yako utakavyokuwa. Ina Data Saver na Notification Controls kama zilivyo version zilizopita Na sasa unaweza kubadili muonekano wa icons zako kwa kubadili ukubwa wake.


8. Usalama wa simu yako ni mahsusi kabisa. Kama ilivyo kwa version zilizopita usalama wa simu yako ni muhimu. Nougat 7.0 na 7.1 zinakuhakikishia usalama wa taarifa zako binafsi na safari hii inakuja maboresho zaidi.


Hii ndiyo Android Nougat 7 na kwa kuanza itapatikana katika simu ya LG V20. Hii itakwa smartphone ya kwanza kutengenezwa ikiwa na Android Nougat 7. Itakujia hivi karibuni.




Chanzo: Android.com

BATCH 4 WALIOCHAGULIWA MZUMBE (DEGREE, DIPLOMA, CERTIFICATE & TRANSFER)

Yafuatayo ni majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu Mzumbe kwa awamu ya 4 kwa mwaka 2016/2017. Pia yapo na majina ya waliohamishwa kutoka kwingineko kwenda Mzumbe.


👉BOFYA HAPA KUONA NA KUPAKUA MAJINA HAYO👈

SIMBA YAZIONYA AFRICAN LYON NA PRISONS

Nahodha wa Simba, Jonas Mkude amesema ari waliyokuwa nayo hivi sasa ana uhakika wa kupata pointi sita nyingine kwenye mechi mbili zilizobaki kabla ya kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mkude alisema pointi sita walizozipata Shinyanga dhidi ya Mwadui na Stand United, zimedhihirisha ubora waliokuwa nao msimu huu na atahakikisha wanaendelea na kasi hiyo ili kutimiza kile ambacho wamekikusudia.

“Lengo ni ubingwa na kwakuwa tunautaka ubingwa kwanza lazima tumalize kinara kwenye mzunguko wa kwanza kwa kuchukua pointi zote sita kwenye michezo yetu miwili iliyobaki na baadaye tujipange kwa ajili ya mzunguko wa pili,” alisema Mkude.

Simba imebakiwa na mechi dhidi ya Africany Lyon na Prisons. Mkude alisema anafurahi kuona kila mchezaji ndani ya kikosi chao akicheza kwa kujituma na kufuata kikamilifu maelekezo kutoka kwa wakuu wa benchi lao la ufundi na anaamini ari hiyo itaendelea hadi mwishoni mwa msimu huu na hatimaye kuwa mabingwa.

“Hatujafungwa hata mchezo mmoja katika michezo 13 ambayo tumecheza hadi sasa hii ni rekodi nzuri lakini tunatakiwa kuiendeleza kwenye mechi zijazo ili tuweze kufanya vizuri zaidi na zaidi kwakuwa bado tuna safari ndefu hadi kufikia mwisho wa ligi,” alisema Mkude.

Nahodha huyo amewataka mashabiki na wanachama wa timu hiyo kuendelea kuwasapoti katika mechi zao ili kushinda mtihani uliopo mbele yao ambao ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la FA, baada ya kufanya vibaya kwa misimu mitatu iliyopita jambo ambalo lilipoteza heshima yao.

Simba inatarajia kucheza na African Lyon keshokutwa na tayari imesharejea kutoka Shinyanga na kuweka kambi Ndege Beach. Simba inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 35 baada ya kucheza mechi 13.

SERIKALI IMEPELEKA TSH. BILIONI 177 KWENYE HALMASHAURI ZA WILAYA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali imepeleka katika halmashauri nchini Sh bilioni 177 Oktoba mwaka huu kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.

Aidha, amempongeza Rais John Magufuli, kwa kufikisha siku 365 za kuwapo madarakani na mafanikio makubwa ya utawala wake tangu alipopewa na Watanzania ridhaa ya kuwa Rais wa Tano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana.

Licha ya pongezi zake, amewaomba Watanzania waendelee kumuunga mkono Rais Magufuli ili afanikishe zaidi dhamira yake njema ya kuwatumikia wananchi. Majaliwa aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma ambapo alizungumzia mambo mbalimbali katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu.

Akizungumzia suala la fedha kupelekwa katika halmashauri, alisema serikali imechukua muda kupeleka fedha mara baada ya bajeti kupitishwa na Bunge kwa kuwa ilitaka kufanya mambo muhimu ya kujiridhisha.

Aliyaja maeneo muhimu ambayo serikali ilitaka kuyafanyia kazi kabla ya kupeleka fedha kuwa ni kujiridhisha kuwepo kwa takwimu muhimu za mapato na matumizi na kupeleka watumishi watakaosimamia shughuli za ukusanyaji wa mapato na matumizi katika halmashauri zote nchini.

Alisema pia serikali ilitaka kuratibu na kutathmini miradi yote iliyokuwa imeanza na haikuwa imeendelezwa kabla ya kuanza miradi mipya ili kutambua thamani zake.

“Baada ya kuwa tumejiridhisha, sasa tumeanza kupeleka fedha kwenye halmashauri zote nchini na kwa mujibu wa kumbukumbu zangu kutoka Hazina wakati napewa taarifa ofisini kwangu, kufikia Oktoba tumeshapeleka zaidi ya Sh bilioni 177,” alisema Majaliwa.

Alisema fedha hizo ni za miradi ya maendeleo kwenye halmashauri zetu nchini na alisema kudhihirisha hilo, aliwaambia wabunge ni shahidi wameanza kuona katika wiki tatu kwenye magazeti kumekuwa na matangazo ya zabuni. Alisema hali hiyo inadhihirisha kuwa miradi iliyokuwepo na inayoendelea imeshaanza kutengewa fedha na kuanza kutekelezwa.

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Munde Abdallah (CCM), alimuuliza Majaliwa katika maswali ya papo kwa hapo, kwamba serikali ina mpango gani wa kupeleka fedha katika halmashauri kutekeleza miradi.

Mbunge huyo alisema miradi mingi imesimama na akitolea mfano wa mkoa wa Tabora anakotoka, akisema halmashauri zote saba hazijapata fedha hizo na kwa nini katika robo ya mwaka wa utekelezaji wa bajeti fedha hazijapelekwa.

“Kabla ya kujibu Mheshimiwa Naibu Spika uridhie niwakumbushe Watanzania kuwa Rais John Magufuli amefikisha siku 365 kwa mafanikio makubwa, tumuombee aendelee vizuri, kila mmoja kwa dhehebu lake amuombee nchi ipate mafanikio makubwa,” alisema Majaliwa kabla ya kujibu swali hilo.

Baada ya kumpongeza Rais Magufuli ambaye aliapishwa Novemba 5 mwaka jana kuwa Rais wa Tanzania baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huo, alijibu swali la Abdallah alisema ni kweli baada ya bajeti serikali inapaswa kupeleka fedha katika halmashauri.

Alisema baada ya tathmini tayari fedha zimeanza kupelekwa katika halmashauri hizo. Akijibu swali la Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) kuhusu mgawanyo wa fedha za Mfuko wa Bunge kuchelewa kufika na kueleza kuwa ni dalili za serikali kufilisika.

Waziri Mkuu alisema serikali haijafilisika na katika kipindi cha mwaka bado kuna miezi saba ya kuzipeleka fedha hizo zinazopelekwa mara moja kwa mwaka.

Aidha, akijibu swali la nyongeza la Waitara kwamba Segerea inapata fedha nyingi (Sh milioni 33) ingawa ina watu wachache wakati Ukonga inapata Sh milioni 16 pekee, Majaliwa alisema atalishughulikia kwa kuwa jimbo lenye watu wengi linapaswa kupewa fedha nyingi.



Chanzo: Habari Leo

WAHAMIAJI 239 WAHOFIWA KUZAMA KATIKA AJALI YA MELI WAKITOKEA LIBYA

Wahamiaji 239 wamehofiwa kuzama katika ajali ya meli wakitokea nchini Libya. Hii ni kwa mujibu wa habari kutoka shirika la Wakimbizi UNHCR.

Msemaji wa UNHCR mjini Roma Italia amesema kuwa taarifa hizo zimethibitishwa na manusura wa ajali walipofikishwa katika ukingo wa bahari katika kisiwa cha Lampedusa.

Mpaka sasa hakuna ambaye amekwishapatikana katika hao 239.

Sami alisema kuwa watu 31 wamenusurika katika ajali za meli mbili zilizopata ajali baharini kufuatia dhoruba kali.

Walisema kuwa watu 29 walinusurika katika meli ya kwanza huku wengine 120 hawajulikani walipo.

Katika jitihada za kuokoa watu, wanawake 2 waliokuwa wakiogelea kujinusuru waliwambia waokoaji kuwa watu hao 120 walikufa katika meli hiyo.

Katika matukio yote mawili, wengi wa wahamiaji hao wanaonekana kuwa ni raia kutoka eneo la Jangwa la Sahara.

Leonard Doyle, msemaji mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) amesema kuwa watu 4,220 wamepoteza maisha katika mwaka huu 2016 kwenye ajali za meli katika bahari ya Mediterania wakijaribu kuvuka kwenda barani Ulaya. Idadi hii ni kubwa kuwahi kurekodiwa.

Zaidi wa watu 330,000 wamevuka bahari ya Mediterania mwaka huu ikilinganishwa na watu Milioni moja waliovuka mwaka jana 2015.


Vyanzo: Al Jazeera & BBC World News

OBAMA AWATAHADHARISHA WAPIGA KURA KUHUSU TRUMP

Rais Barrack Obama amewahimiza wafuasi wa chama cha Democratic kumpigia kura Hillary Clinton na kuonya kwamba Donald Trump ni tishio kwa haki za kijamii, taifa la Marekani na dunia nzima kwa ujumla.


Rais wa Marekani Barrack Obama amewahimiza wafuasi wote wa chama cha Democratic kumpigia kura kwa wingi Hillary Clinton siku ya uchaguzi wiki ijayo na kuonya kwamba Donald Trump mgombea urais wa chama cha Republican ni tishio kwa haki za kijamii ambazo ziliafikiwa kupitia hali ngumu , taifa la Marekani na dunia nzima kwa ujumla.

Akigusia chaguo la rais siku ya Jumanne wiki ijayo, rais Barrack Obama alimpuuzilia mbali Trump kuwa mtu asiyestahili kabisa kuwa rais.

Kufikia sasa Clinton bado anaonyesha uwezekano wa kuwa rais wa 45 wa Marekani lakini huku zikiwa zimesalia siku sita kabla ya uchaguzi huo mkuu, wafuasi wa chama cha Demokratic bado wako chonjo hasa kutokana na mienendo ya Trump isiyotabirika.

Obama aliwaambia wapiga kura katika mji wa Chapel Hill kuwa hatima ya taifa hilo imo mikononi mwao . Aliongeza kwa kusema, „"hatima ya dunia inawategemea nyinyi, wapiga kura wa North Carolina itawabidi kuhakikisha munachukuwa hatua katika mwelekeo bora."

Mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton

Wikileaks yaendelea kutoa barua pepe

Huku kampeini hizo zikipamba moto, barua pepe nyingine za siri zinazomhusu Hillary Clinton zilitolewa hapo jana na mtandao wa wikileaks unaofanya udukuzi na kuchapisha taarifa za siri, hizi zikiwa sehemu ya barua pepe zinazotolewa na mtandao huo kila siku tangu mwezi uliopita.

Mtandao huo umesema kuwa unanuia kutoa barua pepe hizo zilizoibwa kutoka kwa akaunti ya mkuu wa kampeini ya Hillary Clinton , Podesta kila siku katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Hata hivyo msemaji wa wizara ya mashauri ya kigeni ya Marekani John Kirby alisema hapo jana kuwa wizara hio haitatoa taarifa yoyote kuhusiana na madai hayo ya stakabadhi zilizoibwa lakini akasema kuwa juhudi za wizara hiyo za kutoa taarifa sahihi kwa vyombo vya habari kuhusiana na kipindi cha kuhudumu kwa Hillary katika wizara hiyo mara nyingine ilihitajika kuwasiliana na waakilishi wake kuhakikisha kuwepo kwa usawa.

Kundi la kampeini la Clinton hata hivyo limekuwa likionya kuwa mtandao huo wa wikileaks umeharibu barua pepe zilizoibwa na wadukuzi ambao huenda wanafanyia kazi serikali ya Urusi.

Chanzo: DW