ACTION MUVI MPYA INATOKA AGUST 2, SNIPER: GHOST SHOOTER
Muvi inaitwa Sniper: Ghost Shooter inatarajiwa kuingia sokoni tarehe 2 Agost mwaka huu (siku chache kutoka leo kama siku 5 mbele). Imechezwa na Chad Michael Collins, Billy Zane, Dennis Haysbert na wengine wengi. STORI KWA UFUPI Masnaipa wenye akili Chad Collins (katika muvi hii ameigiza kama Brandon Beckett) na Billy Zane (katika muvi hii anaitwa Richard Miller) wanapewa jukumu la kulinda bomba la gesi ili lisiharibiwe na magaidi. Wanapokuwa katika mambano na maadui inapelekea masnaipa wenzao wengine kuuawa na adui asiyefahamika alipo lakini yeye akiwa anafahamu wao (Richard na Brandon) walipojificha. Hofu inazidi kutanda hadi kufikia safu ya ulinzi kushutumiwa kushirikiana na maadui. Kuna mmoja kati yao anashirikiana na upande wa maadui? Je, mpango ni mwanzo wa mpango mwingine kumjua msaliti? Je, Kanali atatumia muda mwingi kuamua nini kifanyike? Haya yote utayapata katika muvi hii Sniper: Ghost Shooter kuanzia Agost 2, mwaka huu katika tovuti na application za kupakua muvi...