Posts

Showing posts from June, 2015

BEN POL AELEZEA ALIVYONUSURIKA KIFO KATIKA AJALI YA BOTI

Image
Msanii wa Bongo Fleva,Ben Pol amesimulia alivyonusurika kifo baada ya boti waliokuwa wakisafiria wakitokea visiwani Mbudya,jijini Dar kuzima ghafla katika ya bahari na kukaa kwa muda wa saa nzima bila kupata msaada. Ben Pol alisema kuwa baada boti kuzima maji yalianza kuingia ndani  na engine ya boti ikazimika na boti hiyo ikaanza kuzama kilichowaokoa walikuwa wamevaa makoti ya kuogelea ‘life jackets’. ‘’Baada ya kukaa kwa saa nzima baharini kwa bahati nzuri ilipita boti ya wavuvi ikatuona ikatuokoa ila mmoja wetu hakuwepo kati ya tuliokolewa na hatujamuona ambao ni wanawake watatu, watoto hao walikuwa watatu, wanaume tulikuwa nane, lakini mmoja ndiye hatujui alipo.’alisema Ben Pol.

VAN VICKER AKUMBWA NA MAFURIKO AKIELEKEA KWAKE

Image
Mafuriko makubwa yaliyoikumba jiji la Accra nchini Ghana usiku wa kuamkia juzi na kuleta maafa ya kuua watu 175 wakiwa wamejihifadhi kwenye kituo cha mafuta baada ya kituo hicho kulipuka moto,yamemkumba pia Staa wa filamu nchini humo Van Vicker akiwa barabarani akielekea nyumbani kwake. Kupitia akaunti yake Instagram Van Vicker aliandika kuwa ameshuhudia mafuriko kwa macho yake (live),huku taa za barabarani zikiwa haziwaki,kuna mashimo,matakataka,umeme ukiwa umekatika na barabara zilikuwa zimefurika maji, na magari yalikuwa yameharibika. Pia aliongeza kuwa waliokuwa wakitembea barabarani walikuwa wakitafuta pa kujihifadhi,madereva walipaniki na bado wakati huo mvua ilikuwa ikinyeesha na pia foleni ilikuwa kubwa na barabara ni ndogo. Ambapo alisema kuwa kawaida huwa inamchukua dakika 45 kwenda nyumbani kwake lakini siku hiyo ilimchukua masaa sita kufika nyumbani kwake. Chanzo; Udaku Specially

URUSI NA QATAR HUENDA ZISIANDAE KOMBE LA DUNIA

Image
Mkuu wa kamati ya uhasibu wa shirikisho la soka duniani FIFA Domenico Scala amesema huenda Urusi na Qatar zikapoteza nafasi za kuyaandaa mashindano ya kombe la dunia mwaka 2018 na 2022 mtawalia iwapo ushahidi utaonyesha kulikuwa na ufisadi katika shughuli ya kinyanganyiro cha kupata kibali cha kuandaa mashindano hayo. Scala hata hivyo amesema mpaka kufikia sasa hawajapokea ushahidi wowote wa kudhihirisha kuwa nchi hizo mbili zilitoa hongo. Matamshi yake ndiyo ya kwanza kutolewa na afisa wa ngazi ya juu wa FIFA kuwa kuna uwezekano nchi hizo zikapokonywa uenyeji wa mashindano hayo. Maafisa wa idara ya mahakama wa Uswisi tayari wameanzisha uchunguzi kuhusu kutolewa kwa kandrasi hiyo ya kuandaa mashindano ya 2018 na 2022 kama sehemu ya uchunguzi wa madai ya ufisadi katika FIFA.  Chanzo: DW

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

Image
Viongozi wa nchi tajiri zaidi duniani zinazounda kundi la G7 wanatarajiwa hii leo kutoa msimamo wa pamoja dhidi ya vitisho vya kiuslama vinavyoikumba dunia vikiwemo kitisho cha makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali hadi kile Rais wa Marekani Barack Obama amelaani na kuutaja kama uchokozi wa Urusi nchini Ukraine. Kwa mara ya tatu mfululizo, viongozi hao wamemtenga Rais wa Urusi Vladimir Putin kutoka mkutano huo ulioanza hapo jana na unaokamilika hii leo katika mji wa Elmau nchini Ujerumani na badala yake wamewaalika viongozi kutoka kwingineko akiwemo waziri mkuu wa Iraq Haider al Abadi na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ambao wote wawili wanakabiliwa na kitisho kutoka makundi ya wanamgambo. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Ufaransa Francois Hollande wanatarajiwa kuangazia masuala ya mazingira katika mkutano huo hasa kuongezeka kwa viwango vya joto duniani na athari zake. Chanzo: DW

KOMBE LA DUNIA KWA WANAWAKE

Image
Michuano ya kombe la dunia la wanawake,inaendelea huko canada katika miji tofauti tofauti.michuano hiyo ya kombe la dunia kwa wanawake liliendelea tena hapo jana kwa michezo miwili kupigwa kati ya Norway waliopepetana na Thailand. Ujeruman ilioonesha kazi pwani ya samawati naizungumzia Ivory Coast na matokeo yalikuwa hivi Norway waliibuka na mtaji wa magoli manne huku Thailand wakikubali matokeo na kutulia na yai. Kwa upande mwingingine kwenye mechi ya pili Ujerumani walijizolea magoli yao mawili na kuwaacha Ivory Coast mikono mitupu. Chanzo: BBC

WATU 400 WAFARIKI KATIKA MTO YANGTSE

Image
Meli iliyozama China Msemaji wa serikali nchini China anasema kuwa karibu watu 400 wanahofiwa kuaga dunia wakati feri ilipozama kwenye mto Yangtze siku ya jumatatu. Idadi hiyo imeongezeka kwa haraka baada ya makundi ya uokoaji kusaka vyumba vya feri hiyo. Kwa sasa meli hiyo imendolewa majini kwa kutumia mitambo mikubwa. Jumla ya watu 456 walikuwa ndani ya feri hiyo wakati ilipokumbwa na dhoruba ambapo ni watu 14 tu walioripotiwa kuponea ajali hiyo. Ajali hiyo inaripotiwa kuwa mbaya zaidi nchini humo tangu miaka 60 iliyopita. Chanzo: BBC