Posts

Showing posts from May, 2022

UDAHILI WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2022/2023 UMEFUNGULIWA

Image
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (NACTVET) limefungungua rasmi dirisha la uombaji wa nafasi za masomo kwa mwaka 2022/2023 ngazi ya Astashahada (Certificate) na Stashahada (Diploma), katika ujumbe huo tangazo linasomeka kama ifuatavyo: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU WAOMBAJI WA UDAHILI WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2022/2023 Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi linapenda kuufahamisha umma kuwa Udahili wa wanafunzi kwa Ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa kozi/programu zote zinazotolewa na Vyuo mbalimbali umefunguliwa rasmi kuanzia tarehe 24 Mei, 2022 hadi tarehe 30 Julai, 2022 katika awamu ya kwanza. Wahitimu wote wa Elimu ya Sekondari na Vyuo wenye sifa za kujiunga na kozi za Astashahada na Stashahada, wanashauriwa kufanya maombi yao kwa umakini ili kupata nafasi ya kujiunga kozi/programu wanazozipenda na ambazo wanatimiza vigezo/sifa za kujiunga nazo kwa mwaka wa masomo 2022/2023. Maombi ya kujiunga na k...