MALAWI IMETEKETEZA TANI 2 ZA PEMBE ZA NDOVU KUTOKA TANZANIA


Malawi imeteketeza tani 2.6 ya pembe za ndovu ambazo zilinaswa na maafisa wa usalama zikitokea nchi jirani ya Tanzania.

Meno hiyo 781 ya tembo ambayo inakisiwa kugharimu takriban dola milioni tatu ilipatikana baada ya operesheni dhidi ya ulanguzi na uwidaji haramu.

Mkurugenzi wa idara inayosimamia mbuga za wanyama pori Bright Kumchedwa, amesema kuwa hiyo ni ishara ya kwanza na dhabiti kutoka kwa Malawi kuwa haitaruhusu tena ardhi yake kutumika kulangua bidhaa za uwindaji haramu.
Hafla ya hiyo ya kihistoria ilifanyika katika eneo la Mzuzu kaskazini mwa nchi hiyo.

Kenya inatarajiwa kutekeleza hatua kama hiyo mwishoni mwa mwezi huu.

Kenya imekamata takriban tani 120 ya meno ya ndovu.

Chanzo: BBC

ZITTO KABWE: RAIS AMELIINGIZIA TAIFA HASARA YA TSH. BILIONI 36

Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa Rais John Pombe Magufuli ameliingizia taifa hasara ya bilioni 36 mpaka sasa toka alipoingia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

 Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook aliandika kuwa kitendo cha Rais Magufuli kushindwa kuchukua hatua juu ya malipo ya IPTL ambayo yanalipwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kila mwezi yamepelekea sasa hivi kufikia jumla ya bilioni 36. 

 "Tshs bilioni 8 kila mwezi TANESCO bado wanalipa IPTL. Rais haijampendeza kumaliza ufisadi huu. IPTL nadhani ni Jipu la Mgongoni (kwa kutumia maneno ya Hidaya wa Richard Mabala ). Rais, kwa kutochukua kwake hatua, ameshaliingizia taifa hasara ya tshs 36 bilioni toka aingie madarakani" aliandika Zitto Kabwe. 

Wakati Rais John Magufuli anatimiza siku 100 toka kutangazwa kama Rais Zitto Kabwe alitoa tathimini yake na kugusia sakata la Escrow pamoja na kampuni ya IPTL na kusema kuwa pesa ambazo wamelipwa IPTL/PAP kwa siku 100 tu zingeweza kununua CT Scan kwa hospitali zote za mikoa nchini.

 "Mkataba wa IPTL bado unaendelea kunyonya Nchi na Serikali inatazama tshs 8 bilioni zinalipwa Kwa matapeli wa IPTL na PAP kila mwezi. Katika siku 100 tangu Rais Magufuli aingie madarakani, jumla ya tshs 30 bilioni zimeshalipwa Kwa IPTL/PAP ambazo zingeweza kununua CT scan Kwa hospitali zote za mikoa nchini. Fedha hii ni zaidi ya mkopo ambao Serikali imechukua kutoka Benki ya Dunia ili kujenga ' fly over ' ya Ubungo jijini Dar Es Salaam" Alisema Zitto Kabwe.



 Chanzo: East Africa Television

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU MAREKANI: TRUMP NA RUBIO WATOFAUTIANA KUHUSU UISLAM

Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican Marco Rubio amemshtumu Donald Trump kwa kusema kuwa Uislamu unachukia Marekani katika mjadala uliokuwa moja kwa moja runingani. Bwana Rubio ambaye anakabiliwa na ushindani wa maisha yake katika jimbo la Florida siku ya Jumanne amesema kuwa Uislamu una tatizo la itikadi kali lakini akaongezea kuwa Waislamu wengi wanapenda Wamerekani. ''Marais hawawezi kusema kile wanachotaka ,kuna madhara'',alisema huku raia wakimpigia makofi. Wagombea hao wanne wa chama cha Republican walisikia maombi kutoka kwa viongozi wa chama hicho kuwa na mjadala wa amani. Ikilinganishwa na mjadala uliopita ambao ulikabiliwa na na matusi ya kibinafsi mjadala huu ulikuwa na muongozo mzuri huku wagombea wote wakitoa malengo ya sera zao. ''Kufikia sasa siamini vile tumekuwa watulivu hapa'',bwana Trump alinukuliwa akisema. Lakini katika swala la Uislamu,kulikuwa na tofauti kubwa kati ya Trump na wagombea wengine huku wenzake wote wakitofautiana naye kwamba familia za magaidi ziangamizwe. Chanzo: BBC

JANET JACKSON AAHIRISHA KUFANYA ZIARA YA MUZIKI ULAYA KUFUATIA MAUZO MABAYA YA TIKETI

Janet Jackson amefuta ziara yake kimuziki 'Unbreakable' barani Ulaya kufuatia mauzo mabaya ya tiketi barani humo. 'Alikuwa anaelekea kushindwa vibaya' kilisema chanzo cha habari. Muuza tiket mkuu alimuandikia barua pepe Janet mapema wiki hii kuhusu kurudishwa kwa hela za watu waliokuwa wamenunua tiketi. Hii ni wiki tatu kabla Janet alikuwa aende kufanya onesho jijini London, 'haitawezekana kwa sasa kusema ni lini tutapanga tena tarehe mpya ya onesho kwa hiyo tunarudisha hela kwa wale waliokuwa wamenunua tiketi' iliandikwa hivyo barua pepe hiyo. Upande wa Janet haukuzungumzia kuhusu kufutwa kwa onesho hilo lakini chanzo cha habari kilisema kuwa ni kufuatia mauzo mabay ya tiketi. 'Alikuwa anaelekea kushindwa vibaya, msanii anapofuta au kuahirisha ziara ya muziki sababu huwa ni mauzo mabaya ya tiketi' kilisema chanzo hicho na kuongeza 'ni bora kuahirisha kuliko kufanya onesho ukumbi ukiwa haujajaa watu haswa kwa msanii Janet Jackson'. Chanzo kutoka kwa waandaaji wa onesho la Janet, Live Nation kilidai kuwa mauzo ya tiketi hayakuwa mazuri 'bado hatuelewi japokuwa bado tuna matazamio mazuri ya onesho hili, lakini isingekuwa na maana kuendelea kusisitiza tarehe hizi . Ana mipango mingi kwa hiyo kunapokuwa na mambo mengi, kunakuwa na mgogoro kuhusu onesho'. Jana, Janet Jackson aliandika kwenye mtandao wa Twitter, 'najua mnanikumbukka, nawakumbuka pia. Nitapanga upya ziara ya Unbrekable Ulaya muda si mrefu kadiri ya uwezo wangu'
Janet Jackson alilazimika kuahirisha maonesho mbalimbali nchini Marekani kufuatia upasuaji aliokuwa amefanyiwa.Taarifa zinasema kuwa Janet atakamilisha maonesho hayo Marekani na anaweza kuongeza siku pia. Producer wa siku nyingi wa Janet, Jimmy Jam amesema kuwa Janet alikuwa anamalizia kurekodi baadhi ya nyimbo zake ili kuweka mambo sawa kwenye albamu yake. Janet anatarajia kufanya onesho kwenye Kombe la Dunia la Dubai tarehe 26 mwezi huu Machi. Anataraji kurudi Marekani kufanya maonesho kuanzia mwezi Mei hadi Septemba. Chanzo: Page Six

MECHI KATI YA LEICESTER NA WEST BROM FAHAMU HAYA

Mchezo wa leo kati ya Leicester city na West Bromwich Albion utapigwa katika dimba la King Power Stadium, ambapo Leicester watakuwa ni wenyeji wa dimba hilo. Mtanange utaanza saa 4 na dakika 45 usiku saa za Afrika Mashariki.

Novemba 1, 2013, West Brom alimfunga Leicester goli moja bila katika dimba la King Power Stadium.

Mwaka 2015, April 11 West Brom wakiwa wenyeji katika dimba la nyumbani, The Hawthorns walipigwa bao tatu dhidi ya mbili na Leicister city.

Lakini pia October 31, mwaka jana 2015, West Brom akiwa mwenyeji kwenye dimba la The Hawthorns alifungwa na Leicester city magoli 3 kwa mawili kama mechi iliyopita.

Leicester City inaongoza ligi ikiwa na pointi 56 ambapo imecheza mechi 27 imeshinda mechi 16, imetoka sare mechi 8, na kupoteza mechi 3 ikiwa na magoli ya kifunga 20.

Kwa upande wa West Brom wao wapo katika nafasi ya 13 wakiwa wamecheza mechi 27, wameshinda mechi 9, sare mechi 8 na kupoteza mechi 10 wakiwa wmemfungwa magoli10. West Brom wana pointi 35 ambapo wanahitaji kushinda mechi zaidi ili kuepuka kikombe cha kuporomoka nafasi waliopo kushuka daraja.

Leicester inaingia dimbani ikiwa na majeruhi wawili, Matthew James na Jeffrey Schlupp.

West Brom ina majeruhi watano, Johhny Evans, Gareth McAuley, Craig Dawson, James Morrison na Callum Mcmanamam.

MAMBO YA KUFAHAMU KATI YA CHELSEA NA NORWICH CITY

Chelsea imeshinda mechi saba na haijapoteza katika mechi tisa ilizokutana na Norwich City kwenye EPL.

Norwich City imefenikiwa kuifunga Chelsea magoli manne tu na kushindwa katika mechi nne ambazo walikutana mara ya mwisho na The Blues.

Steven Naismith wa Norwich City amefanikiwa kuifunga Chelsea magoli sita katima mechi saba walizokutana na The Blues EPL.

Norwich City imeshinda mechi nne tu, sare nne na kupotezaechi nane katika mechi 16 ilizocheza katika dimba lao la nyumbani, Carrow Road. (W4 D4 L8).

Norwich City imepata magoli 10 tu katika dimba lao la nyumbani, hii ni baada ya kushinda mechi mbili kati ya tano za EPL katika dimba hilo.

Katika mechi 7 za EPL na kufunga magoli 7 pamoja na kuwa na jumla ya magoli 19 kwenye ligi.

Chelsea imeshuhudia wachezaji wake 15 wakiifungia magoli timu hiyo msimu huu. Rekodi ambayo ni ya juu zaidi katika mashindani msimu huu.


Guus Hiddink amepoteza mechi moja tu kati ya mechi 23 kama kocha na meneja wa klabu katika ligi ya Uingereza msimu huu. Pia ametoa sare mechi 7 na kushinda 15. (W15 D7 L1)


Norwich City imekuwa na rekodi dogo ya kugusa box la goli msimu huu ambapo imesogeza jumla ya shuti 426 tu katika mechi zilizopita.

Chelsea wanataka kushinda mechi tatu mfululizo kwa mara ya kwanza yangu mwaka jana April, 2015.

Norwich inaingia uwanjani ikuwa na majeruhi mmoja tu, Andre Wisdom aliyeumia goti katika mechi ya tarehe 27 Februari mwaka huu.

Kwa upande wa Chelsea majeruhi ni John Terry,  Kout Zouma na Radamel Falcao García Zaráte.

Katika mechi tano zilizopita, Octoba 6, 2012, Chelsea alishinda Norwich magoli 4 dhidi ya moja  kwenye dimba la Stamford Bridge.

Desemba 26, 2012, Chelsea alimfunga Norwich goli moja bila katika uwanja wa Norwich Carrow Road.

Mwaka 2013 Octoba 6, Norwich alifungwa na Chelsea magoli 3 kwa moja, Carrow Road.

May 4, 2014, Norwich na Chelsea walitoka sare ya bila kufungana katika dimba la Stamford Bridge.

Novemba 21, mwaka jana 2015, Chelsea ilishinda goli moja bila dhidi ya Norwich katika dimba la nyumbani, Stamford Bridge.

Mtanange wa Leo utapigwa katika dimba la Norwich City, Carrow Road majira ya saa 4 na dakika 45 usiku saa za Afrika Mashariki.