SERIKALI ya Jamhuri ya Watu wa China imetangaza kuwa, kwa mara ya nne katika kipindi kifupi inapeleka msaada wa dawa, vifaa na mahitaji mengine ya tiba yenye thamani ya dola za Marekani milioni 85 kukabiliana na ugonjwa wa ebola kwa nchi tatu za Afrika Magharibi, ambazo zinapambana na ugonjwa huo, ambao mpaka sasa umeua zaidi ya watu 4,000. Aidha, China imetangaza kuwa itajenga kituo kikubwa cha afya na tiba katika nchi ya Liberia, kama sehemu ya kukabiliana na ugonjwa huo. Msaada huo mwingine wa China umetangazwa na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, XI Jinping katika mazungumzo yake rasmi na Rais Jakaya Kikwete. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kwenye The Great Hall of the People mjini Beijing, ikiwa ni sehemu ya ziara rasmi ya Rais Kikwete, Rais Jinping alisema: “Hali katika Afrika sasa ni ya utulivu lakini yapo matishio ya mara kwa mara mengine ya ndani ya Afrika na mengine ya nje na mojawapo ya matishio hayo ni ugonjwa wa ebola.” Aliongeza Rais Jinping: “Mpaka sasa, ...