KUELEKEA KOMBE LA DUNIA: ZAIDI YA TIKETI MILIONI 3 ZIMENUNULIWA MTANDAONI

 The World Cup trophy is seen on stage
Zikiwa zimesalia siku takribani 143 kuelekea michuano ya kombe la Dunia la FIFA nchini Uursi mwezi Juni, FIFA imesema tayari kumekuwa na uhitaji wa tiketi za michuano hiyo kwa mashabiki walioko nchini Urusi na wale walioko nje ya Urusi.

Takribani tiketi 3,141,163 mpaka kufikia tarehe 31 Desemba mwaka jana zilikuwa tayari zimeombwa na msahabiki kwa nia ya mtandao. Mashabiki wote wa mpira wa miguu wenye uhakika wa kuhurhuria michuano hiyo nchini Uurusi, wanaweza kupata tiketi kwa kutembelea tovuti ya FIFA, FIFA.com/tickets

Mpaka kufikia sasa, mashabiki wa mpira walioweka oda ya tiketi wanatokea nchi za Uursi, Ujerumani, Ajentina, Mexico, Brazil, Peru, Colombia, Marekani, Hisipania, Poland, na China. Nchi hizi nyingine tofauti na Urusi zinatengeneza jumla ya asilimia 38 ya waombaji wa tiketi hizi za FIFA kimataifa huku asilimia iliyosalia 62 ni raia wa nchinI Urusi. Mashabiki wanaweza kununua tiketi kwa mechi zote isipokua mechi ya ufunguzi na finali

Aidha FIFA imesema kuwa kuna tiketi kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa viungo vya mwili na wanaweza kuweka oda ya tiketi hzo kwa  kubofya hapa.

Njia za Kufanya Malipo ya Tiketi
Tiketi zinaweza kulipiwa kwa njia ya mtandao kupitia  kadi za malipo za Visa ama Visa Checkout. Visa ni mshirika rasmi wa FIFA katika michuano hii ya Kombe la Dunia. Kufahamu namna ya kulipia kwa njia nyingine, bofya hapa.

VITAMBULISHO VYA MASHABIKI
Serikali ya Urusi imeomba mashabiki wawe na kadi maalumu za utambulisho wao wa ushabiki kwa wote watakaohudhuria michuano ya Kombe la Dunia kwa mwaka huu nchini humo. Vitambulisho hivyo vitatolewa bure. Mashabiki wanakumbushwa kuomba vitambulisho hivyo kwa utaratibu utakaotolewa mara baada ya kupokea barua pepe za uthibitisho wa manunuzi ya tiketi. Vitambulisho hivi vitatumika wakati wa kuingia viwanjani pamoja na tiketi za mechi. Matumizi ya kitambulisho hiki yatampa shabiki ofa mbalimbali zitakazotolewa nchini Urusi ikiwemo kusafiri bure kwa usafiri wa umma nchini humo kwa siku za mechi. Kufahamu namna ya kupata kitambulisho hicho bofya www.fan-id.ru
FIFA inakumbusha kuwa haihusiani na utolewaji na matumizi ya vitambulisho hivi kwa namna yoyote ile.

Comments

Popular Posts

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

BIBI WA MIAKA 85 AKAMATWA KWA KUIBA HERENI

MAMBO YA MUHIMU KUFAHAMU NA KUZINGATIA KABLA YA KUCHAGUA KOZI (TAALUMA) CHUO KIKUU